Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
TCRA imetoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu Radio Free Africa na Radio One Stereo kwa kukiuka kanuni za utangazaji viliporusha kipindi cha Amka na BBC ambapo Tundu Lissu aliituhumu serikali kuwazuia viongozi wa Chadema kumuaga Hayati Rais Benjamin Mkapa.

Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kosa la ngono kamati imetoa onyo na faini ya milioni 5 itakayolipwa TCRA.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Aidha, Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi

EfYRukoXkAAyCIw.jpg

EfYRukrXgAEaDA3.jpg

EfYRuksWAAA73n8.jpg

EfYRuktXYAA5D2-.jpg
 
Forex 6 months' heavy padlock, media 3 months' heavy padlock, Tanzania Daima permanently padlocked, you know what? If you pray for our popular media freedom, vote out of office the tyranny who is aiming at silencing and financially suffocating voters during the 2020 elections campaign period! Get rid of him!
 
Wakuu,

Nimeona kupitia nipashetz Instagram account kuwa TCRA wameipiga kufuli hicho kipindi kwa kukiuka maudhui ya utangazaji. Pia hawatakiwi kuwa na kipindi Chenye maudhui hayo kuanzia leo.

Poleni sana kwa Clouds fm kwa pigo hili ingawa hatujui chanzo halisi ni nini.

Ushauri nyakati hizi Jahazi haipo turudisheni burudani za zamani, maneno kidogo muziki mzuri unatawala dizaini ya mid morning jams ile ya dj boogie Master.

Pendekezo: Itapendeza mkimpa space John Dilinga na mtu wa sports kidogo lakini mziki mzuri ukitawala na maneno kidogo.

Kuwa na kipindi kisicho na maudhui ya Jahazi kwa jioni ni mtihani. Kila lakheri kwenu.
 
Ila makufuli yanatembea si kawaida
Kosa lao ni>>Kamati ya Maudhui ya TCRA imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Aidha, Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi
 
Back
Top Bottom