Clouds FM yafagilia Walanguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Clouds FM yafagilia Walanguzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KunjyGroup, Dec 7, 2009.

 1. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Clouds FM yatusaliti!

  The whole week PJ wa Power Breakfast (clouds FM) alikua anatembelea migodi ya Barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:

  1. Mikataba ya migodi ni mibovu
  2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini
  3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa
  4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua.

  Leo hii PJ na Power Breakfast, niseme Cluods FM wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu?

  PJ, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana Barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo. Mimi na wewe PJ tutabaki hapa hapa TZ. Hiyo cheap PR unawapa haitafautiani na ile ya Richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!

  Ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia Kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na Liyumba je? Anashutumiwa kuiba Tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi?

  Sasa nikuulize PJ, hao jamaa zako wa Barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba BOT tuka invest katika migodi yetu?


  Huu ni ujinga watu kama PJ na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa.

  Ombi langu kwako PJ na wana Clouds wenzako nikwamba, waTZ waleo sio mbumbumbu. Tunaelewa. Tunachambua na tunatafari. Huwezi tupumbaza kamwe.

  Mjadala unaendelea.
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Kaka umesema yote nakushukuru kwa moyo wa ujasirimali
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo

  Waandishi habari na watangazaji Tz ni lazima wawe makini. Kama unavyosema kunjygroup hawa Barrick wameanzisha PR nzito baada ya vifo vya mgodi wa North Mara ambao mpaka leo serikali imekaa kimya juu yake. Je PB waliuliza maswali yanayostahiki? Barrick wanachuma kiasi gani kila mwaka, na hizo $200, 000 kwa mwaka wanazotoa kwa city council ni asilimia gani ya mapato yao?
   
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ulitegemea nini kutoka kwa ma-check bob?! Wanachojali wao ni starehe na kustarehesha tu. Sidhani kwamba wana muda wa kufikiria kwa kina nchi inavyokwenda.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,254
  Trophy Points: 280
  Nilikisikiliza hicho kipindi kilichorushwa tarehe nne mwezi Disemba mwaka huu wa elfu mbili na tisa.

  Kwa kweli nlistaajabishwa sana na taarifa hizo za kuwatetea wezi wa rasilimali zetu, nkajiuliza hivi kweli huyu ni mzalendo? Hakika niliumizwa sana na ripoti yake.

  Naomba kilauzi fuemu waache kuwatetea mafisadi
   
 6. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa hapo kwenye nyekundu nani wa kulaumiwa? sheria ya madini ndo inasema ivyo kwamba watalipa si zaidi ya $200,000 maana wana weza wakakutpa hata buku kumi tu na usiseme chochote!!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kimey,
  Sheria za madini ziliandikwa na Barrick wenyewe. Wakawahonga viongozi wetu wakaweka saini hata bila ya kuzisoma. Hivi kwa nini serikali haitaki hiyo mikataba iwekwe hadharani eti ni siri ya serikali na wawekezaji? Jiulize.
   
 8. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu sana JF
  Karibu sana kwenye jukwaa la Siasa. Hapa ni Taifa kwanza.

  Twendelee na mjadala.
   
 9. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  Arghhhhh...hivi wana JF wenzangu hao clouds fm mnawajua au mnawasikia????....msemaji wa barick tewel teweli by far ni smart mara 1000 ya huyo pj...sasa unategemea nini?...Pj hana chchote cha kuuliza wala kuhoji kwa teweli teweli au barick kwa ujumla...

  hiyo tisa ..kumi ..wanavyopenda vijirushwa vya kijinga ndio usiseme...pj na watangazaji wa radio nyingi za fm hapa mjini wanaishi kwa sh 10,000 za wanamziki wa bongo flava ..sasa kwa fungu alilonalo teweli teweli la kuisafisha barick hasa kwa scandal ya north mara si ndio hata clauds wataipa kipindi kizima cha kuisifia barick...

  pole sana pj nakuhurumia you are caught in the middle of the situation..ila ni kwa mapungufu ya upeo wako wa kuelewa na njaa yenu kwa ujumla (ila sio kwa wanahabariu makini na smart)...na siamini kama kweli pj aliamka asubuhi akasema naenda kutembelea north mara na barick kkwa ujumla bila boss wake kusaga kujua (au kuingia mkataba na barick wa kuisafisha na scandalls zinazoikabili)....pj mie navyoamini hawezi, hatoweza na wala hakuwahi kufikirian kuwahoji barick except kwa orders toka juu...

  pole sana kijana..ila anyway naamini ulikaribishwa na ku-kirimiwa vizuri sanaaaa...ndio maana umewasifia sanaaa...naomba nikuulize maswali haya
  1- barick wanatumia maji ya mto tigite?...kama hawatumii kwann hukuwauliza sababu za kutoyatumia kwa vile ni safi na salama
  2-wananchi wanaozunguka mgodi wanasemaje..au uliishia kumsikiliza boss wako tewel tewel na kurudi kuisifia barick hapa dar???
  next time usiingie kwenye matatizo bila kujua .... pole sana anyway
   
 10. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Clouds FM yatusaliti!
  The whole week PJ wa Power Breakfast (clouds FM) alikua anatembelea migodi ya Barrick. Akaja na bla bla bla kwamba wamepeleka maendeleo katika vijiji vilivyo zunguka migodi. Mie nimemuona yeye na waliemtuma kwamba ni wa puuzi. Sababu ni hizi:
  1. Mikataba ya migodi ni mibovu - Nani analaumiwe kwa mikataba mibovu? Barrick au serikali yako na Bunge lako ''tukufu''? Mikataba yao hata kama ni mibovu lakini iko kwa mujibu wa sheria ya madini ya mwaka 1998 iliyopitishwa na mbunge wako. Barrick hawakuingia Bungeni kupitisha sheria hiyo!

  2. Tunapata ONLY 3% from revenue ya madini - Nani wa kulaumiwa? Barrick au serikali yako? Na je wajua kwamba kampuni ya Alex Sterwart inalamba 1.7% out 3% tunayokusanya kwa kukagua mauzo ya dhahabu!? Nao huo si mkataba mbovu kati ya serikali yako na Alex Sterwart?

  3. Migodi imetililisha sumu katika mito kama Tighitte na watu pamoja na mifugo imekufa - Je serikali yako imechukua hatua gani katika kuwawajibisha wahusika wa hili>? Kama ushahidi upo kwanini wasifikishwe mahakamani?

  4. Watu waliwahi miminiwa risasi na walinzi wa migodi na wengine waliuwawa na hamna aliekamatwa kwa kuua - Kama walikiuka sheria za ulinzi wa migodi ulitegemea nini? Kumbuka pale kuna dhahabu kwa hiyo ulinzi mkali wa kutumia silaha unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria. Na je walikuwa raia wema au majambazi? Kama kuna ushahidi kwanini kesi hiyo isipelekwe mahakamani?

  Leo hii PJ na Power Breakfast, niseme Cluods FM wamesimama na kufagilia migodi ya walanguzi. Hii ni haki? Si ni usaliti huu?
  PJ, unadhani hatujui kwamba ulikaribishwa na wana Barrick, ukalipiwa malazi na ukapandishwa ndege yao, unategemea sisi tutaamini kwamba utawaponda? Unatakiwa kumwomba radhi PJ kwa kumdhalilisha kiasi hiki. Sidhani kama yeye ni masikini kiasi cha ''kununuliwa'' kwa kupandishwa ndege, kupewa chakula na malazi ya mgodini ili kumsafisha mtu au taasisi iliyo ovu. Yeye ametoa maoni yake kulingana na aliyoyaona!

  Hao jamaa wanafanya PR ili tuwaone niwasafi na wanatusaidia. Hamna kitu. Ni capitalist wanataka kupata faida lukuki ya madini na watimke baadae na kutuachia mashimo - Huo ndio ukweli japo ni mchungu sana! Hakuna bepari yeyote duniani anayefanya kazi bila kutegemea faida kubwa. Msingi wa ubepari ni mtaji unaozaa faida. Suala la kuachiwa mashimo ni kuzungumza wewe na mbunge wako!

  Mimi na wewe PJ tutabaki hapa hapa TZ. Hiyo cheap PR unawapa haitafautiani na ile ya Richmond kuweka matangazo katika magazeti na kudai ni kampuni halali. Nani aliamini? Wapo watu wenye upeo mdogo wakuchambua mambo wakaamini. Na wewe unatakata tukuamini? Mimi nitoe!


  Ukasema tena kwamba eti hatuwezi kuiendesha migodi sababu gari moja inayobeba mchanga wa madini linaizwa $1,000,000. Tujilize, walieba hela kupitia Kagoda waliiba liasi gani? Tsh. 40billion. Hizo hela zinaweza nunua migari haina hiyo mingapi? Na Liyumba je? Anashutumiwa kuiba Tsh. 220billion, nae angenunua migari mingapi? Sasa nikuulize PJ, hao jamaa zako wa Barrick, hizo investment wanatoa mifukoni mwao au wanakopa? Sisi hatuwezi kukopa au kuiba BOT tuka invest katika migodi yetu? - Hapa sasa ndipo unapothibitisha kwamba serikali yako imeoza na haiwezi kufanya chochote kwa sababu ya wizi na ubadhirifu wa mali ya umma. Tanesco hiyo hapo mbona inawashinda kuendesha? Mashirika ya umma mbona yaliwashinda kuendesha? ATCL, TRL mpaka kesho yamewashinda! Mgodi wa Mwadui mliampora mkoloni mbona umeshinda kuendesha? Hao wezi wa BoT si ndio hao hao wangekwenda kuiba huko migodini?

  Huu ni ujinga watu kama PJ na watawala wengine wanataka tuamini kwamba hatuna uwezo wakuchimba madini yetu. Nakataa. - Hakika ninakuambia leo hii, mimi siwatetei Barrick au wachimbaji wengine hata kidogo. Ninachosema, bora wao wanaendesha uchimbaji huu kwa ufanisi na matunda yake tunayoaona kutokana na kodi, ajira na mirahaba wanayolipa. Jukumu hili ingeachiwa serikali yako ungeshangaa migodi imekufa, faidi haijulikani imekwenda wapi na hakuna wa kuwajibiswa! ''I see the glass half full while you see the glass half empty''
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  tusije shangaa hizi radio ni za Freemansons ambao ndio wanaongoza kwa ufisadi na ndio wenye mapesa hapa nchini na huko ughaibuni,just thinking aloud!
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  PJ Huwa anatafuta sifa tu kwamba yeye ni mtu media. Naona kile kipindi chao kimeanza kukosa mashamsham.Ni afadhali kusikiliza leo tena maana najua kule kumejaa mauzauza ya hekaheka na burudisho la taarabu nijue moja
   
 13. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Jamani wengine tumeondoka kitambo kidogo nyumbani, pj ndio nani ? Je anacredential gani inapokuja kwenye suala la migodi ?
   
 14. D

  Dear Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Asante sana kwa kuwaanika hawa watangazaji feki,
  Unajua wao PB wanajionaga wana misingi mizuri ya uandishi kumbe ni weupe kupita maelezo,
  Mimi nilisikiliza akitete huo mgodi tena zaidi ya mara moja,na huku wakiwakebehi wananchi wa kijijini hapo.
  Hawa wote ni waganga njaa na waangamiza NCHI,Kikwete FUNGA HII RADIO ni moja ya ufisadi BUBU
   
 15. Laface77

  Laface77 JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 1,301
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  Sioni hata kwa nini tunakaa kujadili research iliyofanywa na waropokaji wa clouds fm. tatizo lao ni kuwa hawafuatilii vitu na pindi wakiingia studio wanaongea kitu chochote kinachokuja katika akili zao. PJ haya hajui alikuwa ameenda huki kufanya nini na taarifa anayoitoa ina madhara au faida gani kwa wale watakaoisikia.
   
 16. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani msimlaumu bure PJ au timu nzima ya Power Breakfast am Clouds fm yote. Hawa watu upeo wao ni mdogo sana. Wanachokiweza hapa mjini ni kuwanyofoa elfu kumi kumi wasanii wa bongo flava na kuandaa matamasha ya muziki.

  Hebu niambieni wana JF kweli tunaweza kujadili ripoti ya PJ au ya Clouds FM kuhusu athari za Mgodi wa North Mara hapa????

  Je PJ ana elimu na uzoefu gani wa kufanya utafiti yakinifu katika eneo hilo??

  Naamini tutapoteza muda kuijadili ripoti yake achilia mbali yeye mwenyewe. Ninachosikitika tu ni kwamba kuna kundi kubwa la watanzania ambao huwa wanaamini chochote kinachotangazwa ama kuandikwa kwenye vyombo vya habari bila kufikiri wala kufanya uchambuzi.

  Clouds na watangazaji wake ni waganga njaa hapa mjini. Hata ukisikia namna wanavyotangaza matangazo ya biashara huwa inashangaza sana. Kuna wakati huwa nafikiria hii mamlaka ya kulinda haki ya walaji ama FCC au TCRA wanafanya nini??? Mbona wanashindwa ku regulate hii sector????

  Huwezi kuruhusu matangazo ya biashara yanayopotosha umma namna hii. Walichikifanya Barrick ni PR, wamewalipa Clouds pesa ili wafanye huo upuuzi.

  Nchi zingine zenye Serikali sikivu, huwezi kufanya PR ya kizandiki kama hii ya Barrick!!

  Kweli njaa mbaya!!!
   
 17. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145

  PJ ni Paul James, mropokaji (sidhani kama ni mtangazaji) wa Radio Clouds FM.

  Hana credential yoyote katika masuala ya migodi/madini. Kama kumbukumbu yangu ni sahihi, ana ki-certificate cha journalism toka pale chuo cha uandishi wa habari cha TIMES (sidhani hata kama kimesajiliwa na TCU achilia mbali NACTE) kipo maeneo ya Ilala Bungoni.
   
 18. B

  Bobby JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Dear umemaanisha hayo uliyoandika? Huyo unayemwambia afunge radio unajuwa yuko upande gani? Angekuwa upande huo unaohisi yupo chenje, idriss, kaaa la maji na mafisadi wengine wote leo wangekuwa segerea. Unamwonea bure na huo ushauri unaompa kwani hana hiyo jeuri kabisaaaaaaaaaaaaaa.
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Tukikubali kuwaachia waingie mikataba mibovu kama hiyo ya madini TUTAVUNA MABUA, kwani tunachofanya ni KUMCHEKEA NYANI!

  NYANI hachekewi, hata siku moja!
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Naona waanze kujituma kuongezea maarifa na ujuzi maana ni bado vijana. Kukaa kwenye kipaza sauti na kuropoka tu ukifikiri ndio unajua sana unaweza kuwa kichekesho bure
   
Loading...