Clouds FM wamburuza mahakamani Lady JayDee, kesi yapigwa kalenda hadi Mei 27...

Bado hiyo thread ni utata, "

Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo"
.

Sasa swali linakuja yeye kafunguliwa kesi then yeye mwenyewe akakabidhi hati ya mashtaka inakuwaje hapo?

La pili

"Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu ,Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu".

Katika kesi za madai tuhuma huwa hazisomwi mahakamani labda km kesi ni ya jinai, kwa faida ya wengine kesi za madai huwasilishwa mahakamani kwa kutumia hati ya madai(PLAINT), Baada ya kuwasilishwa WITO hutolewa na mahakama kwa mdaiwa na unaweza kuwa wito wa kufika mahakamani au wito wa kujibu madai.

Na kama ni wa kufika mahakamani basi akifika atapewa hati ya madai iliyowasilishwa na atapewa siku 21 za kuwasilisha majibu ya mdai baada ya hapo kesi itaendelea kwa hatua zingine km vile pre-trial conference ambapo ktk hatua hii nyaraka zote za kesi zinakuwa zimekamilika,hakuna nyongeza,mashahidi wangapi kila pande inategemea kuwaita,na ndio wanapanga kesi itachukua muda gani kumalizika then itafuata mediation ikishindikana wanaenda katika full hearing. Hakuna kusomewa hati ya mashtaka!
 
Tena kesi amepewa Nyamlani..yule jamaa wa TFF na rafiki wa kina Joe...baada ya Tamasha la "Made in Tanzania" lililoudhuliwa na Waziri Mkuu!kutofautisha unyonyaji wa Clouds na Ma-CCM ni ngumu sana
 
na walishamjibu na sie waelewa tulimuelewa vizuri ruge...

wamepima wakagundua yale maelezo yao ya PB didn't work-out

bado mashabiki wana hasira nao,ili kutozidisha nikupeleka court ili kumfunga mdomo asiendelee kuwalipua
 
Kwani swala lililopo mahakamani ni lipi la mdhulumiwa kumtaja mdhulumu wake hadharani ama? Naona wazee wa magorofani wanajipanga kudhurumu mpaka kiduchu cha wasanii

hahahaha,Ila ukweli wasanii wengi hawajitambui,nimesikia Mpoto jana kamponda jide.
 
Huyo binti kayataka mwenyewe. Timbwili kalianzisha, ya nini unamuonea huruma?

Na Jide hana support ya watu kama ambavyo unadai ingawa mtu kama dunia yako yote ni JF waweza kudhani hivyo.

Uliona nyomi lile Dodoma? Kama Clouds ni wabaya hivyo na hawakubaliki iweje nyomi lote lile lijitokeze kuunga mkono event ya Clouds?

Watu walijitokeza kwa wingi Dodoma ili wapate fursa ya kuwaona wasanii ambao katika hali ya kawaida sio rahisi kupata fursa ya kuwaona.

Pia kuna taarifa za ndani kuwa clouds fm walitumia mkakati wa kiccm wa kujaza watu uwanjani na mji wa Dodoma kwa ujumla kwa kusafirishwa watu kutoka mikoani na wilayani kwenda Dodoma mjini ili kuinogesha event yao.

Btw, kama kweli cloudsfm (naomba kukuvika uwakilishi wao hapa JF) wanaamini kwamba raia wengi wako nyuma yao tofauti na Jide, kwanini sasa wameamua kukimbilia mahakamani? Hiyo si dhahiri kuwa wanamuogopa kwamba atawafungua macho watanzania kwakuwa alikuwa ameahidi kupasua nazi tarehe 15/05/2013?? Mi naona wanapoteza muda kujaribu kumtikisa Jide lakini hawatamuweza kwakuwa watu wengi sana wanamuunga mkono Jide na hatimaye clouds fm wataaibika tu.
 
Nasikia Nyani Ngabu ni mtumishi pale Clouds sijui hizi kama zitakuwa ni habari za kweli, kama zitakuwa ni habari za kweli indirectly lazima Jidy na Nyani ngabu wawe kwenye Bifu, kama unadhani hakuna uhusiano wowote jaribu kumsema vibaya Ruge au Joseph K mbele ya Kibonde utaona matokeo yake.

kwan kibonde ndo mpambe na kibarak wa maboss wa clouds?
 
Last edited by a moderator:
Tena kesi amepewa Nyamlani..yule jamaa wa TFF na rafiki wa kina Joe...baada ya Tamasha la "Made in Tanzania" lililoudhuliwa na Waziri Mkuu!kutofautisha unyonyaji wa Clouds na Ma-CCM ni ngumu sana

hahahaha,hiyo kwangu ni breaking newz
 
Huyo binti kayataka mwenyewe. Timbwili kalianzisha, ya nini unamuonea huruma?

Na Jide hana support ya watu kama ambavyo unadai ingawa mtu kama dunia yako yote ni JF waweza kudhani hivyo.

Uliona nyomi lile Dodoma? Kama Clouds ni wabaya hivyo na hawakubaliki iweje nyomi lote lile lijitokeze kuunga mkono event ya Clouds?

Wale wanafuata starehe tu,ambayo inatolewa bure!hawaifuati Clouds...wengine wanataka kumuona Ben pal au godzila..ni passion ya muziki,si mapenzi kwa wamiliki..tofautisha haya mambo!!
 
naona hii ndio shukrani ya ruge baada ya kummega vya kutosha huyu jide....
 
Sina bifu naye. Ni kwamba tu naona kanunua bifu ili kupromoti album yake mpya.

Sasa ili apate free publicity akaamua ku pick fight na Goliath, so to speak.

Kwa vile Clouds ni chama kubwa nadhani calculations zake ni kwamba umma utamuonea huruma, utakuwa upande wake, na kununua album yake mpya.

Her beef ain't genuine. It's phoney baloney coconut bacon.

Unauhakika maneno yako ni ya kweli kwa kiasi gani???
 
Watu walijitokeza kwa wingi Dodoma ili wapate fursa ya kuwaona wasanii ambao katika hali ya kawaida sio rahisi kupata fursa ya kuwaona.

Lakini hiyo fursa si ilisababishwa na Clouds....unabisha?

Pia kuna taarifa za ndani kuwa clouds fm walitumia mkakati wa kiccm wa kujaza watu uwanjani na mji wa Dodoma kwa ujumla kwa kusafirishwa watu kutoka mikoani na wilayani kwenda Dodoma mjini ili kuinogesha event yao.

Hizo taarifa kama hazina chanzo basi ni umbea, fitna, na majungu tu ambayo tumeshayazoea.

Btw, kama kweli cloudsfm (naomba kukuvika uwakilishi wao hapa JF) wanaamini kwamba raia wengi wako nyuma yao tofauti na Jide,

Kwa sababu ndiyo njia ya kistaarabu na kisheria tuliyojiwekea kutatua migogoro. Mbona yeye huyo binti hakwenda mahakamani na kufungua shauri kama kweli madai yake yana ukweli wowote? Ni kwa sababu ni mrongo. Anatafuta promo kwa njia ya mkato ya kuanzisha beef na chama la Clouds. Ona sasa hivi alivyokuwa gumzo la jiji? Hahitaji tena hata kununua matangazo popote pale ya kuuhabarisha umma kuwa ana album iliyoko njiani.

kwanini sasa wameamua kukimbilia mahakamani?

Wewe ulitaka wakimbilie wapi sasa kama wao wameona kuwa wamechafuliwa?

Hiyo si dhahiri kuwa wanamuogopa kwamba atawafungua macho watanzania kwakuwa alikuwa ameahidi kupasua nazi tarehe 15/05/2013??

Ah wapi! Hiyo ni tafsiri yako tu. Clouds wamuogope huyo binti? Ana nini hadi wamuogope? Anasababisha sunami? Anakula watu? Halafu kwani huko mahakamani ndo unadhani kila kitu kitakuwa sealed hadi watu wasijue madai ya kila upande? Hoja yako ya kwamba ni dhahiri wanamuogopa kwa sababu atawafungua macho Watanzania haina mashiko kwa sababu huko mahakamani huyo binti naye atapata wasaa wa kutoa ya upande wake. Sasa akitoa yake Watanzania hawatajua?

Mi naona wanapoteza muda kujaribu kumtikisa Jide lakini hawatamuweza kwakuwa watu wengi sana wanamuunga mkono Jide na hatimaye clouds fm wataaibika tu.

Acha wapoteze muda. Si ni muda wao bana. Kwani wanapoteza muda wako wewe? Na hiyo ya kusema wengi wanamuunga Jide mkono umeitoa wapi? Hapa JF? Facebook? Whatsapp? Twitter? Instagram?
 
Wakati anaomba wakutanishwe wayamalize alikua anatuhadaa , ameenda mahakamani kufanya nn? Ruge acheni unyonyaji wa style ya sisiemu kwa wananchi wanyonge.
 
Back
Top Bottom