Kesi ya uraia pacha kuanza kusikilizwa Mei 2

Joseph_Mungure

Senior Member
Mar 6, 2021
108
161
Kitaifa

Kesi ya uraia pacha kuanza kusikilizwa Mei 2

Jumanne, Februari 21, 2023

Wadau wa suala la uraia pacha wakitoka mahakamani, kusikiliza kesi ya uraia pacha iliyofunguliwa na Watanzania Sita wanaoshi nje ya chini, iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam.

By James Magai

Muktasari:

Mahakama imepanga kusikiliza kwanza pingamizi la awali lililowekwa na Serikali Mei 2, 2023, kabla ya kuendelea na kesi ya msingi.

Dar es Salaam. Kesi ya uraia pacha iliyofunguliwa na Watanzania sita wanaishi na kufanya kazi nje ya nchi sasa itaanza kusikilizwa Mei 2, 2023, katika hatua ya awali ya mapingamizi ya Serikali.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 18 ya mwaka 2022 imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu na Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kalemera, Nkole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo Watanzania hao wanapinga sheria ya Uraia hasa vifungu vinavyozuia huo uraia pacha hasa kifungu cha 7(1) na (2) (c), (4)(a) (6) vya Sheria ya Uraia ambavyo wanadai kuwa vinakiuka haki zao nyingine za Kikatiba

Hivyo wanaiomba mahakama itamke kuwa vifungu hivyo ni batili wakidai kuwa vinakiuka haki zao za Kikatiba kwa kuwa vinawanyanya haki ya asili isiyonyang’anyika yaani uraia wa kuzaliwa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mustafa Ismail akishirikiana na jaji Hamidu Mwanga na jaji Obadia Bwegoge imetajwa leo kwa mahakamani hapo mara ya kwanza leo Jumatatu, Februari 2023 mbele ya majaji wawili, Mwanga na Bwegoge.

Wakili wa wadai, Peter Kibatala ameieleza mahakama kuwa wadaiwa wameshajibu madai yao kwa maandishi na pia wamewasilisha pingamizi la awali.

Mdaiwa, Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewakilishwa na Wakili wa Serikali, Ayub Sanga.

Nje ya Mahakama wakili Kibatala amezitaja hoja za pingamizi hili kuwa ni pamoja na kuna kasoro za kisheria katika hati za viapo vya wadai.

Nyingine ni kwamba hati ya madai kutokusainiwa na wadai pamoja na wakili wao na kwamba kesi hiyo inakiuka masharti ya lazima ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Utekelezaji Wajibu na Haki, katika kutafuta haki za Kikatiba.

Kutokana na kuwepo pingamizi hilo la Serikali, kama ilivyo kawaida mahakama imepanga kulisikiliza kwanza pingamizi hilo kabla ya kusikiliza kesi ya msingi na imepanga kulisikiliza Mei 2, 2023, mbele ya jopo kamili, akiwemo kiongozi wa jopo ambaye jana hakuwepo.

Wakati kesi hiyo ilipotajwa, wadai ambao wote sita ambao wako nje ya nchi hawakuwepo mahakamani badala yake waliwakilishwa na Liberatus Mwang’ombe aliyesafiri kutoka Washington DC. Marekani kwa ajili hiyo, akiungana na wadau wengine wa uraia pacha walioko hapa nchini.

Kwa mujibu wa viapo vyao, hawa ni Watanzania kwa kuzaliwa walioondoka nchini na kwenda ughaibuni kwa nyakati tofautitofauti hususani katika nchi za Marekani, Uingereza na Canada wanakoishi na kufanya kazi ambako pia walishapata uraia.

Katika viapo vyao wanaeleza kuwa wameathirika sana kitendo cha kunyimwa haki mbalimbali katika nchi yao waliyozaliwa kwa kuzingatia kwamba walipata uraia wa nchi hizo kwa sababu za kiuchumi na ustaki wa kijamii tu.

Wanadai kuwa wao ni Watanzania kwa damu na kwamba wanatamani kuendelea kuwa Watanzania, lakini kwa vifungu hivyo vya Sheria ya Uraia wananyimwa haki hiyo.

Wanadai kuwa wenzao wanaotoka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Rwanda na Uganda wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuwa hati za kusafiria za Afrika Mashariki kwa kuwa nchi zao zinaruhusu uraia pacha lakini wao hawawezi kupata hati hizo.

Miongoni mwa haki wanazozikosa nchini walikozaliwa ni pamoja na kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi na kwamba wanapotembelea nchini wanaishia kuishi katika nyumba za ndugu zao au hotelini.

Wanataja haki nyingine wanazozikosa kuwa ni pamoja na kutokuchagua viongozi wala kushiriki kugombea nafasi ya umma katika uchaguzi nchini
 
Kwahiyo nikienda Marekani nikapata uraia nitashindwa kurithi hata mashamba ya baba yangu ? Khaah
 
Kama umeamua kuwa mmarekani kaa huko huko na umarekani wako

Ya nini kusumbua watu?

America yenyewe hairuhusu uraia pacha ndio maana wakati wa kuapa, ‘unasema nitailinda nchi yangu Marekani kwa kila kitu nilicho nacho na Mungu anisaidie’.
 
Tena serikali ikatae kabisa uhuni wa uraia pacha... you can not be royal to two countries, no!
 
Baada ya Vita ya wenyewe Kwa wenyewe hapo Rwanda ,Kagame akashauriwa Rudisha diaspora wako ili waje kujenga nchi Yao Leo Rwanda ile inakimbia mithili ya rocketi , diaspora ndio wanaojenga nchi Kwa Karne hii lakini CCM Kwa akili za kijamaa wamelala usingizi wa ponooooo
 
Kitaifa

Kesi ya uraia pacha kuanza kusikilizwa Mei 2

Jumanne, Februari 21, 2023

Wadau wa suala la uraia pacha wakitoka mahakamani, kusikiliza kesi ya uraia pacha iliyofunguliwa na Watanzania Sita wanaoshi nje ya chini, iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, Dar es Salaam.

By James Magai

Muktasari:

Mahakama imepanga kusikiliza kwanza pingamizi la awali lililowekwa na Serikali Mei 2, 2023, kabla ya kuendelea na kesi ya msingi.

Dar es Salaam. Kesi ya uraia pacha iliyofunguliwa na Watanzania sita wanaishi na kufanya kazi nje ya nchi sasa itaanza kusikilizwa Mei 2, 2023, katika hatua ya awali ya mapingamizi ya Serikali.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 18 ya mwaka 2022 imefunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu na Shaban Fundi, Patrick Nyelesa Nhigula, Restuta Kalemera, Nkole Muya, Emmanuel Emmanuel na Bashir Kassam dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo Watanzania hao wanapinga sheria ya Uraia hasa vifungu vinavyozuia huo uraia pacha hasa kifungu cha 7(1) na (2) (c), (4)(a) (6) vya Sheria ya Uraia ambavyo wanadai kuwa vinakiuka haki zao nyingine za Kikatiba

Hivyo wanaiomba mahakama itamke kuwa vifungu hivyo ni batili wakidai kuwa vinakiuka haki zao za Kikatiba kwa kuwa vinawanyanya haki ya asili isiyonyang’anyika yaani uraia wa kuzaliwa.

Kesi hiyo iliyopangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mustafa Ismail akishirikiana na jaji Hamidu Mwanga na jaji Obadia Bwegoge imetajwa leo kwa mahakamani hapo mara ya kwanza leo Jumatatu, Februari 2023 mbele ya majaji wawili, Mwanga na Bwegoge.

Wakili wa wadai, Peter Kibatala ameieleza mahakama kuwa wadaiwa wameshajibu madai yao kwa maandishi na pia wamewasilisha pingamizi la awali.

Mdaiwa, Serikali kupitia Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewakilishwa na Wakili wa Serikali, Ayub Sanga.

Nje ya Mahakama wakili Kibatala amezitaja hoja za pingamizi hili kuwa ni pamoja na kuna kasoro za kisheria katika hati za viapo vya wadai.

Nyingine ni kwamba hati ya madai kutokusainiwa na wadai pamoja na wakili wao na kwamba kesi hiyo inakiuka masharti ya lazima ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Utekelezaji Wajibu na Haki, katika kutafuta haki za Kikatiba.

Kutokana na kuwepo pingamizi hilo la Serikali, kama ilivyo kawaida mahakama imepanga kulisikiliza kwanza pingamizi hilo kabla ya kusikiliza kesi ya msingi na imepanga kulisikiliza Mei 2, 2023, mbele ya jopo kamili, akiwemo kiongozi wa jopo ambaye jana hakuwepo.

Wakati kesi hiyo ilipotajwa, wadai ambao wote sita ambao wako nje ya nchi hawakuwepo mahakamani badala yake waliwakilishwa na Liberatus Mwang’ombe aliyesafiri kutoka Washington DC. Marekani kwa ajili hiyo, akiungana na wadau wengine wa uraia pacha walioko hapa nchini.

Kwa mujibu wa viapo vyao, hawa ni Watanzania kwa kuzaliwa walioondoka nchini na kwenda ughaibuni kwa nyakati tofautitofauti hususani katika nchi za Marekani, Uingereza na Canada wanakoishi na kufanya kazi ambako pia walishapata uraia.

Katika viapo vyao wanaeleza kuwa wameathirika sana kitendo cha kunyimwa haki mbalimbali katika nchi yao waliyozaliwa kwa kuzingatia kwamba walipata uraia wa nchi hizo kwa sababu za kiuchumi na ustaki wa kijamii tu.

Wanadai kuwa wao ni Watanzania kwa damu na kwamba wanatamani kuendelea kuwa Watanzania, lakini kwa vifungu hivyo vya Sheria ya Uraia wananyimwa haki hiyo.

Wanadai kuwa wenzao wanaotoka katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Rwanda na Uganda wanaoishi nje ya nchi wanaruhusiwa kuwa hati za kusafiria za Afrika Mashariki kwa kuwa nchi zao zinaruhusu uraia pacha lakini wao hawawezi kupata hati hizo.

Miongoni mwa haki wanazozikosa nchini walikozaliwa ni pamoja na kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi na kwamba wanapotembelea nchini wanaishia kuishi katika nyumba za ndugu zao au hotelini.

Wanataja haki nyingine wanazozikosa kuwa ni pamoja na kutokuchagua viongozi wala kushiriki kugombea nafasi ya umma katika uchaguzi nchini
Mbona hakuna anayeanzisha kesi kuhusu Mgombea Binafsi? Pascal Mayalla
 
Kama umeamua kuwa mmarekani kaa huko huko na umarekani wako

Ya nini kusumbua watu?

America yenyewe hairuhusu uraia pacha ndio maana wakati wa kuapa, ‘unasema nitailinda nchi yangu Marekani kwa kila kitu nilicho nacho na Mungu anisaidie’.

Acha uongo, Marekani wanaruhusu uraia pacha!
 
You don’t know what you are talking about ; what is “royal “ to two countries mean?
You mean one cannot be “loyal “ to his country of birth? Why can’t one be?
Dual citizenship will allow the diaspora to reap the benefits of their host country and share those benefits with their country of birth; hence their loyalty will be with their country of birth!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom