Bado Niponipo
JF-Expert Member
- Aug 15, 2008
- 680
- 168
Maswali MANNE KWA TCRA.
1. Ni kwa nini Vodacom Foundation wakusanye michango toka kwa walalahoi na kisha itumike kama michango toka Vodacom Foundation kwenda kwa wahanga?
2. Jee Vodacom Foundation/Clouds Fm wanayo mamlaka ya kisheria kukusanya michango ya aina hii, jee sheria ya nchi inasemaje juu ya ukusanyaji wa michango ya aina hii?michango ya walalahoi iko salama kiasi gani hapa?..nijuavyo mimi Vodacom/Clouds SIYO non-profit organizations?
3. Matarajio yao ni kukusanya kiasi gani na ni nini wanatarajia kufanya na hiyo michango, na endapo kiwango walichoweka kikizidi hilo ongezeko watafanyia nini, na ni kiasi gani kimekwisha changiwa hadi hivi sasa?
4. Mchanganuo wa huo mchango wa shilingi 250/= uko vipi, Vodacom wanafaidika vipi hapa, vipi kuhusu gharama za uendeshaji wa zoezi hili mpaka kukabidhi hii michango je ni kasi gani, mnyambulisho mzima wa mahesabu ya fedha uko vipi hapa?
Clouds FM wamejiunga na Red Alert na mkurugenzi wao Joseph Kusaga yuko studio anawapigia simu watu maarufu ili wachange na tayari ameshachangisha zaidi ya 5m. Wanachangisha pia kwa njia ya sms.
Naona wanasema hawatoki studio mpaka kukamilisha kiasi cha mil 70 naona watu wengi sana wamechangia mpaka sasa - hii ifundishe wengine pia siku zijazo kutumia vyombo vya habari na sehemu zingine kwa ajili ya kutangaza vitu kama hivi naona JF na TPN walijisahau kwa kufikiri kwamba hii inajitosheleza hakuhitajika vitu kama TV na Radio kwa ajili ya kuendesha Kampeni hiyo
Leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast, watangazaji wa kipindi cha XXL wametangaza kwamba redio hiyo itasitisha kwa muda kupiga nyimbo za wanamuziki wa Tanzania ili kushawishi wanamuziki na watu wengine maarufu waweze kuchangia watu walioathirika na mafuriko ya Kilosa.
Radio hiyo ilieleza kwamba wamepanga kukusanya sh. 50 mil katika kipindi cha siku mbili au tatu kuanzia leo. Watangazaji B12 na DJ Fatty wameeleza kwamba mwanamuziki yoyote atakaye taka nyimbo yake ichezwe redioni atatakiwa kutuma meseji 10 ili kuchangia waanga wa mafuriko ya Kilosa. Si kutuma meseji tu, michango ya aina yoyote inapokelewa kama nguo, chakula, mablanketi na vitu vingine.
Katika hili Clouds FM wanastahili pongezi, naamini hii itaamsha moyo wa kusaidia matatizo yanayotokea kwenye jamii yetu ambapo ni nadra sana kwa wanamuziki wetu wa kibongo kujitokeza kusaidia.
Mzee Mwanakijiji,
Nikiwa mkongwe ningependa kutoa machache
Nimekwua nikifuatilia kampeni zote mbili,ya TPN,JF na Issa Michuzi;kampeni yenu imekuwa ni kampeni ya wazi kabisa na michango yenu inakwenda sehemu husika (red cross).Hivyo nawaunga mkono katika hilo na mmefanya kazi nzuri
2.Hili sual la Vodacom;jipya lenye lengo kama lenu(wengine wanasema wamedandia) linanipa wasiwasi sana.na ningependa upige simu Vodacom na umuulize binti wa Makamba akupe majibu ya maswali yafuatayo;
a)Je Vodacom Foundation imesajiriwa serikalini kama taasisi ya kutoa Misaaada?
b)Kama Imesajiriwa je pesa zake zinatoka wapi?
c)KWa kuwa wameamua kukusanya pesa toka kwa watanzania(siyo kibiashara);Je wapo tayari kukaguliwa hesabu zao kwa pesa zote ambazo zimechangishwa na wananchi?Rejea taarifa ambazo zipo kuwa makampuni haya yanapeleka takwimu za uongo ili walipe kodi ndogo.
d)Vodacom kama Kampuni moja ya masharti na vigezo vya uwekezaji ni kusaidia shughuli za kijamii nchini kutokaana na faida wanayopata;Je kwanini wameamua kuwachangisha wananchi tena
3.Kwa kuwa hizi namba kitaalam ambazo zinaitwa short code zinatolewa na Serikali na TCRA wanahusika na utoaji wake;kwanini seriakli isiwekeze katika kutengeneza platform ambayo itakuwa inafacilitate suala a watu kuchangia moja kwa moja serikalini?
Mwisho kabisa,wakati Rais Obama anatangaza wamerekani kuchangia HAITI alikuwa mkali na kueleza kuwa serikali itasimamia pesa yote itakayokusanywa na wananchi.Je serikali yetu kupitia waziri husika inafuatilia michango hii?
naomba kusema kwamba Vodacom kama Kampuni nyingine wanahitajika kutoa misaada ya khali na mali katika hili na serikali ilitakiwa isimamie shughuli za kuchangia kwa njia ya simu ila tatizo serikali yetu imejaa watu wasio wabunifsi na wabinafsi;
Vodacom walikurupuka na hili nahisi ni kuelekea 2010 ambapo binti wa makamba na kaka yake wote wana mipango ya kisiasa!s
BTW the line;check PM yako
Ni mzee mwenzako;
Gembe
Kwa ujmla idea ya kuchangia wahanga ni nzuri na tunatakiwa kuiunga mkono. Tatizo ni kwamba Kampuni kubwa kama vodacom badala ya kutoa fedha toka kwenye kapu lake imeamua kuchangisha, hata hivyo hatujui usalama wa michango hiyo. Pamoja na udhaifu huo, kuna kitu wanapandikiza kwa wabongo si kingine ni moyo wa kutoa misaada kwa wahanga wa majanga mbalimbali nawapongeza CLOUD FM mpaka kufikia jioni hii walikuwa wameshafikisha 27m. Kudos clouds