Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Ni juhudi nzuri kwa kweli. Hela zikishachangwa zinapelekwa kwa nani ambaye anapeleka misaada kwa wahanga?
Gazeti la Habari Leo limeuliza vizuri
Maafa ya Kilosa yasigeuzwe mtaji
Imeandikwa na Neophitius Kyaruzi; Tarehe: 27th January 2010
KWANZA nichukue fursa hii kuwapa pole waathirika wa mafuriko yaliyotokea Kilosa, Morogoro ambao sikupata bahati ya kuwasiliana nao tangu walipopatwa na maafa hayo.
Pili, nipongeze watu au taasisi zilizojitolea kwa hali na mali kuwasaidia waathirika hawa, kwani mchango wao umewarahisishia kidogo ugumu wa maisha wanaokabiliana nao hivi sasa.
Baada ya kusema hayo sasa nizungumzie jambo muhimu ambalo tunapaswa kulizingatia katika kipindi hiki na siku nyingine, iwapo Taifa letu litakumbwa na mahafa kama hayo.
Kwa wanaofutailia vyombo vya habari, bila shaka, watakuwa wamesikia juu ya njia mpya ya ukusanyaji fedha kwa ajili ya waathirika kwa kutumia simu za mkononi.
Njia hiyo ambayo inatumia teknolojia ya kisasa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu hizo inaendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
Ukweli ni kwamba teknolojia hiyo si ngeni nchini, kwani tumekuwa tukiishuhudia katika kampuni nyingi za simu zikiitumia kukusanya fedha kupitia mashindano kama vile maoni ya kipima joto, promosheni za kushindania magari, bahati nasibu ya Kismat Sms, Pata Vichekesho, Mistari ya Biblia na nyingine nyingi.
Kinachofanyika katika teknolojia hiyo ni kwamba kampuni hizo zimekuwa zikikusanya fedha kwa njia ya kielektroniki huku wateja wakipeleka fedha halisi kwenye kampuni hizo kwa kununua zaidi muda wa maongezi.
Ukweli ni kwamba njia hiyo ya ukusanyaji fedha imekuwa na mafanikio makubwa, kiasi kwamba hivi sasa hakuna biashara inayovuna fedha nyingi za walalahoi kama huduma za simu za mikononi, hasa kwa kutumia mbinu hiyo.
Kwa kutambua ukweli huo, baada ya Vodacom kuombwa na wadau wa ukusanyaji fedha kwa ajili kusaidia wathirika wa maafa, imekubali kukusanya fedha kwa njia ya wateja wake kutuma ujumbe mfupi wa maneno ambapo kwa kila ujumbe (Maafa), mteja atakatwa Sh 250 katika akaunti yake ya muda wa maongezi, hivyo atakuwa amechangia waathirika kwa njia hiyo.
Kilichonishangaza ni kwamba gharama hizo pia zinahusisha asilimia 20 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), wakati Serikali inatambua kwamba fedha zinazokusanywa ni za dharura kwa ajili ya kukabiliana na maafa.
Hivi kweli ni sahihi kutoza kodi walalahoi wanaojitolea kuwasaidia wenzao katika maafa? Kodi hii ya nini kama fedha hizo si za kibiashara?
Jambo lingine la kushangaza, ni kwamba wakati tunahamasishwa kuchangia, hakuna maelezo yanyoonesha mgawanyo wa fedha hizo na kiasi gani kinachohitajika kukamilisha sehemu ya msaada inayohitajika.
Wakati huo huo, hatujui kiasi gani kitapelekwa kwa waathirika na kiasi gani kitabaki Vodacom. Najiuliza maswali haya kwa kuwa kiasi kinachokusanywa kwa kila SMS ni kikubwa, kwani ni sawa kabisa na kiwango ambacho kimekuwa kikikusanywa katika mashindano mengi ya bahati nasibu ambayo huendeshwa na kampuni za simu ikiwamo Vodacom.
Kampuni kama Vodacom yenye wateja zaidi ya milioni saba, iwapo wateja wake milioni mbili, kila mmoja akituma ujumbe mmoja kwa siku itakuwa imekusanya Sh milioni 500 - kwa siku, ikiwa kiasi hicho hicho kitakusanywa kwa siku 30 nadhani fedha hizo zinaweza kutumika kuwajengea waathirika wote nyumba za gharama nafuu za matofali ya kuchoma na kuwapa mitaji ya kuanzia maisha.
Kutokana na ukweli huo, tunapaswa kuhoji mchanganuo wa mgawanyo wa fedha hizo, tusijikute tunafaidisha kundi fulani huku waathirika wakiendelea kukabiliwa na umaskini. Ukweli ni kwamba makusanyo mengine yamekuwa yakionekana kama yana lengo la kuisaidia jamii, kumbe mwisho wa siku yananufaisha kundi fulani tu, mifano ipo mingi, chunguzeni!