Clouds FM acheni Utoto

Clouds FM acheni Utoto

Jd ashagombana na mwanafa hata hawasalimiani. Hivyo ukiacha ugomvi wa jide na clouds bado kuna ugomvi wa jide na mwanafa. Sijui unapata picha gani hapo? Ku-mute chorus ya jide kwenye wimbo wa mwanafa ni sawa kwani jide hana mahusiano mazuri na mwenye wimbo. Tatizo mmeshupaa kubishania jambo dogo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza ukimfundisha anakuelewa. Hapa ndipo mnanikumbusha ule msemo wa prof.Kabudi wa 'tofauti kati ya mjinga na mpumbavu'.

Vp kuhusu nyimbo zengine ambazo Jay dee anatajwa jina tu huwa wanazifanye? Na maana ya kufanya vile ni nini?
 
Jd ashagombana na mwanafa hata hawasalimiani. Hivyo ukiacha ugomvi wa jide na clouds bado kuna ugomvi wa jide na mwanafa. Sijui unapata picha gani hapo? Ku-mute chorus ya jide kwenye wimbo wa mwanafa ni sawa kwani jide hana mahusiano mazuri na mwenye wimbo. Tatizo mmeshupaa kubishania jambo dogo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza ukimfundisha anakuelewa. Hapa ndipo mnanikumbusha ule msemo wa prof.Kabudi wa 'tofauti kati ya mjinga na mpumbavu'.

Hivi kuna ulazima wa wao kuchezaa huo wimbo kama wanajua wataufanyia editing wakati uko hewani? au wanaupiga kwa makusudi hayo? hopeless!
 
Umewahi kusikia wimbo wowote wa WAGOSI WA KAYA Clouds? Hawapigi

Watapiga wa nini wakati Wagosi walishatanga vita na clouds? Wagosi ni vinega, clouds walichokifanya walikata kichwa cha nyoka(sugu) na kuwaacha hao wadandiaji kwenye mataa... safi kabisa. Hiyo ndo namna nzuri ya kuwapiga wapumbavu wapenda kufata mikumbo.
 
Hao machizi karibu wote, wanapenda wasanii wanaowabusu busu mikvndu yao. Ukiwapinga ETI wanabana. Wanawaburuza kina baba Kayla na wenzake, ila wanaojitambua, hawapo huko!
 
Hivi kuna ulazima wa wao kuchezaa huo wimbo kama wanajua wataufanyia editing wakati uko hewani? au wanaupiga kwa makusudi hayo? hopeless!

Kwanza unachotakiwa kuelewa ni kuwa hata hizo nyimbo alizoshirikishwa jide hawapigi pale. Kilichofanyika juzi kati ni kuwa walikua wanatambulisha albu ya nyuma ya mwanafa ikawalazimu waweke nyimbo zake zilizohit.

Kaimbe na jide uone kama watacheza wimbo wako. Kila sehemu ina utaratibu wake wa kazi ukiwapelekea use.nge wako unakula ban. Ni haki yao wala msipende kuwapangia namna ya kufanya kazi. Nyie hamna haya mtakuja kusema mbona Gadner hachezi nyimbo za Jide kwenye kipindi chake wakati sababu zinaeleweka hata kwa mtoto wa chekechea.

Prof.Kabudi- heli uwe mjinga ukieleweshwa utaelewa, kuliko kuwa mpumbavu ukaishia KUSHUPAA.
HAPA WATU MNASHUPAA ZAIDI ILA UKWELI MNAUJUA.
 
Jd ashagombana na mwanafa hata hawasalimiani. Hivyo ukiacha ugomvi wa jide na clouds bado kuna ugomvi wa jide na mwanafa. Sijui unapata picha gani hapo? Ku-mute chorus ya jide kwenye wimbo wa mwanafa ni sawa kwani jide hana mahusiano mazuri na mwenye wimbo. Tatizo mmeshupaa kubishania jambo dogo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza ukimfundisha anakuelewa. Hapa ndipo mnanikumbusha ule msemo wa prof.Kabudi wa 'tofauti kati ya mjinga na mpumbavu'.

Wewe ni yupi kati ya mjinga na mpumbavu?
Nafikiri utakuwa njia panda.
 
Tatizo la Tanzania ni zaidi ya kwenye muziki! Hii nchi imeshakua ya mabwana na watwana! Kila sekta kama hubebi briefcase za watu hata Ualimu ukuu hupati! Kina Makonda na wale ma bar maid waliokula shavu ukuu wa wilaya! Haiwezekani watu wachache wawachagulie burudani watanzania milioni 45! Na haya ni matokeo ya Ikulu kujaza vibaka!
 
Nafikiri hujitambui. Ile kampuni binafsi ina uhusiano gani na kikwete? Si ajabu na wewe una mke na watoto wanakuita baba! Dah!! kama hulidhishwi na jinsi inavyokupa huduma unayo haki ya kuhamia kwingine. Acha kushupaa.
 
Watapiga wa nini wakati Wagosi walishatanga vita na clouds? Wagosi ni vinega, clouds walichokifanya walikata kichwa cha nyoka(sugu) na kuwaacha hao wadandiaji kwenye mataa... safi kabisa. Hiyo ndo namna nzuri ya kuwapiga wapumbavu wapenda kufata mikumbo.

Wagosi wa kaya ndiyo walikuwa wafuata mkumbo??
 
Habari ndo hiyo. Walishadadia ugomvi usiowahusu wakaacha kusululisha wa kwao. Mwenzao akasululisha akala mtonyo ugomvi ukaisha wao wakabaki kwenye mataa wanabwabwaja.
 
Habari Wanabodi,

Nipo nasikiliza Clouds FM kipindi cha XXL Segment ya "Album Review". Leo wana Review Album (2003) ya Mwana FA ya "Toleo Lijalo" yenye nyimbo kama 'Wanapendana', 'Alikufa kwa Ngoma' etc. Kwenye wimbo wa 'Alikufa kwa ngoma' ameimba na Anaconda (Lady Jay Dee) cha kushangaza kwenye huo wimbo wakati wana review ikifika sehemu ya chorus ya Jide wana-mute inasikika beat tu. Kitendo cha Clouds FM kama taasisi kampuni nzima kuweka beef na msanii mmoja inajidhihirisha Clouds FM ni radio ya wahuni tu.

Clouds FM sio mara ya kwanza kufanya upumbavu huo, nakumbuka kipindi cha nyuma Inspector Haroun alienda nao tofauti, kipindi hiko wimbo wake wa "Buzi" ndio ulikuwa una-hit basi jamaa kila ikifika pale anapochana Inspector sauti wanaondoa inasikika beat tu.

Kwenye ngoma ya Ben Pol "Jikubali" kuna moja ya mstari unaimbwa "Nampenda Lady jay Dee,namzimia Zitto" ile sehemu ya neno Lady Jay Dee wanaisugua (Scratch) na ilo neno halisikiki kabisa.

Kwenye kuadhimisha miaka 15 ya Dully sykes, kwenye promo walikuwa wanapiga nyimbo za nyuma za Dully Sykes, kuna ngoma inaitwa Bijou inavyoanza ina neno "Okay mbili sifuri sifuri nne, P-funky kinywele kimoja" ilipoanza hapo kwenye P-funky wakaikata kabisa wakaipeleka mbele.

Kwa Mchezo huo wa kitoto unaofanywa na Clouds Media inaishushia hadhi sana hiyo kampuni. Kitendo cha kampuni hiyo kufanya mambo ya utoto ni wazi redio inaendeshwa na makanjanja na sio watu wenye weledi. Clouds FM ikubali pia matakwa ya wasanii, kama msanii akikataa kufanya deal kwa sababu anaona haimfaidishi yeye ni haki yake kukataa na si kigezo cha kutopiga nyimbo zake.

Kuna watu watasema kwamba redio zipo zaidi ya 60 na TV zaidi ya 20 kwanini wasanii wailalamikie Clouds tu? Hapa tunacholalamika ni kufinya (mute) sauti yeyote iliyopo kwenye nyimbo alizoshirikishwa msanii walioenda nae tofauti. Kama wanapiga wimbo wa Ben Pol waachie wimbo kama ulivyo na si ku-mute majina ya watu waliotajwa wenye beef nao.

CLOUDS MEDIA ACHENI UTOTO.

mimi si mshabiki wa clouds, ila kwa hili nawatetea jide aliwahi kutamka kwamba sauti yake isisikike clouds akiwa hai au akifa
 
Unaijua historia ya huu mgogoro au unaongea tu? Una uhakika kisa cha kutopiga ni kv tu Jide aligombana na bosi wa Clouds?

Mkuu usiwatetee hawa clouds wanarudisha maendeleo ya wasanii.
 
Wasanii wanajirudisha nyuma wenyewe sema haya mengine ndo hivyo Watanzania kila tunaposhindwa lazima tutafute mchawi! Hivi kweli unataka kuniambia Mr. Nice alipotezwa na Clouds? Juma Nature kweli amepotezwa na Clouds? What about East Coast Team... wamepotezwa na Clouds? What about Q-Chillar na TID... Chid Benz my best Hip Hop artist unaamin kabisa kwamba drugs wanazojidunga ni kwa ajili ya Clouds? By the way, ikiwa kila siku kelele ndio zile zile kwamba wasanii wanashushwa na Clouds, kama ni kweli ni kwanini basi wasanii waendelee kuing'ang'ania Clouds wakati kuna radio stations kibao hapa mjini??

Binafsi katika maisha yangu nimekuwa na wasanii mara kadhaa... kwa mfano, nikichukulia Wanaume Family, mtu ambae alikuwa smart ni mmoja tu ndie amepotea kwenye game... huyu ni Luten Kalama... au labda na Nature... lakini hawa wote wamepotea baada ya kukosa management yenye uwezo kama Fella na hawajapotezwa na radio station yoyote!
 
Hili la Unyonyaji wa Clouds media huwezi kuliona kwa juu juu kama unavyochukulia mkuu.

Pata picha ni msanii gani amefikia mafanikio anayostahili chini ya media hii hususani kutokea pale kwenye jumba lao la THT?

Sikatai kwamba kuna wasanii wamejizika wenyewe lakini pia wapo wengi wanaliwa indirect bila wao kujua.

Unasema kwamba kwa nini wasanii wasiende radio nyingine!? Tatizo sio radio nyingine bali utambue Ruge na Kusaga ni zaidi ya clouds wanapokosana na msanii wanaziba mirija mingi na hyo ndio hofu kuu ya wasanii wetu wengi walioko chini ya hii media na ni haki yetu kuwasemea mana tunaishi nao huku mitaani tunajua jinsi gani wanalalamika lakini hofu inawatawala.

Wasanii wengi wanaogundua hili wanaongea kwa uchungu but hawana jinsi kwa sababu wameshika makali. Waliojaribu ni hao akina Jide, Wagosi, Sugu na vingega wengine lakini hawatoshi na hawana impact kubwa kwa maana waliobaki bado wanaiabudu clouds.!!

Hebu waonee huruma hawa wasanii wetu wanaolipwa kiduchu kwa kazi kubwa. Kazi anayofanya Barnaba sio wakua hapo alipo sasa stuka kaka...

Sasa hivi kuna chekeche cheke tour ya Kiba Tz nzima mtizame jasho analotoa halafu subiri akirudi kariakoo umuulize ameingiza sh ngapi kwa tour hiyo then utagundua ni kwa nini tunasema wananyonya.

Kama ni mmoja wa hapo mawingu I'm very sorry brother.
 
Umewataja waliothubutu... je, miongoni mwao nani yupo kwenye game zaidi ya Jide? Vinega gani unaowasema wewe manake ninaowafahamu ni kwamba walisharudi kujisalimisha kwa Clouds kwamba walikuwa wameingizwa chaka na Sugu... au kuna vinega wengine! Unawataja Wagosi... are serious man? Ulitarajia ile staili ya muziki wa Wagosi bado wangeendelea kutoboa wakati muziki umebadilika sana na wao hawataki kubadilika? Nani hivi sasa anaweza kukaa kusikiliza au ku-download wimbo unaozungumzia habari cjui za manesi, mwenyekiti wa mtaa cjui kafanya nini, matrafiki na mambo mengine kama hayo? Najua hata hao watatafuta mchawi kumbe mchawi ni wao wenyewe wasiotaka kubadilika kutokana na game lilivyo! Na hili la kutotaka kubadilika linawaathiri hata wanamuziki wa nje... sio Tanzania! Leo ukiangalia wanamuziki wa America wa miaka 10 iliyopita, majority hawapo kwenye game na hivi sasa kuna new faces na wale ambao bado wapo kwenye game ni kwavile wanajua soko linataka nini! Sasa ikiwa kote huko wengine wanaingia wengine wanapotea, what's so special kwa hawa wa Tanzania ambao mtu akipotea tu basi lazima atafute mchawi?? Q-Chifu alipopotea alimsingia Diamond kwamba kamroga... hao ndio Watanzania, hawakubali kwamba wana matatizo wao binafsi lakini kila linalotokea, lazima watatfuta mchawi!!!

Hip hop ambayo ameifanya mtu kama Sugu ni tofauti na hii ya sasa... so, usitarajie anakuja tena na mambo ya "Sugu moto chini, ooooo, Sugu moo chini, haaaaaa....!" halafu utarajie watu watakusikiliza na wakiacha kukusikiliza utafute mchawi! Mitoto ya zamani ilikuwa kama mazuzu, ukiiimbia kuku kapanda baiskeli, yenyewe inafurahia tu... hawa watoto wa dijitali nani umweleze habari za bata kavaa laizoni halafu ukipotezewa usingizie Clouds??

Tatizo lingine la hawa wakongwe ni kutotaka kukubali kwamba madogo wanaokuja kwenye game siku hizi wapo tight huku wao wakijivunia ukongwe! Huku mtaani unakutana na madogo wanaimba au wanadondosha ma-punch line hadi unawaogopa!

Umetaja THT... be honest! Hivi kweli unaweza kuwalinganisha wasanii wa THT na wasanii wengine ukiondoa wale ambao tayari wana majina makubwa? Au mafanikio unayosema wewe ni yapi?

Kwamba Clouds wanakata mirija yote!! Yaani unataka kuniambia Clouds wana ubavu wa kwenda kumwangia msanii kwenye radio mshindani wake? Au umesikiliza maneno ya Jay Dee? Hivi kweli unataka kuniambia yule Jay Dee wa Understand ft TID, Machoz, Malaika, n.k ndie huyu wa Joto Hasira na Yahya? Kuwa mkweli kisha ongea na nafsi yako ujitajie nyimbo tatu za JD unazozikubali kama hujakuta zote ni za miaka 5 iliyopita!!!

Yule mshikaji wake Mkoloni (jina limenitoka)! Katoa wimbo wala haeleweki ikiwa ni mdumange, mduara au ngoma za kwao Tanga! Watu wakikupotezea uwalaumu Clouds??

Tatizo wengi wenu mnasikiliza maneno ya watu ambao wameshindwa tayari na ukichunguza karibu wote ambao wanakuwa wanapiga kelele wanakuwa hawana jipya vinginevyo nitajie msanii mmoja ambae amelalamika wakati bado akiwa hot! Ngoma ikiwa hot haizuiliki hususani dunia ya leo yenye radio kila kona, social networks n.k coz' hivi sasa wanaosikiliza nyimbo kupitia radio ni wachache zaidi ukilinganisha na wale wanaosikiliza kupitia other medias!
 
Mkuu naona wewe ni miongoni mwa shareholders wa hapo mawingu. Lakini utambue hao jamaa wanawanyonya sana wasanii. Tazama jasho wanalotoa kwenye shows zinazoratibiwa na hio media na ujira wanaoupata.

Unasema tht wana music mzuri is that all about:what: Tunahitaji mafanikio beyond mkuu.!!
 
Back
Top Bottom