Clouds FM acheni Utoto

Clouds FM acheni Utoto

afu mtoa uzi hujaelewa kitu. lady jay dee aliomba mwenyewe sauti yake,jina lake au nyimbo zake zisikike clouds. sasa hapo clouds wana kosa lipi.?
Mengine sijui

kwa hiyo wanapo mute sauti ya Jay Dee wanamkomoa nani? Jay Dee au wasikilizaji wa huo wimbo na wasikilizaji wa hiyo radio?. Kwa mtazamo wangu wanawakomoa wasikilizaji na sio JAy Dee. Na bila shaka huyo Jay hata hii radio haisikilizi kabisa. kimsingi clouds lazima wajitafakari ili ugomvi wao na Jay Dee usiathiri wasikilizaji wa radio yao. Mimi kama msikilizaji wa hii radio nahitaji kupata full burudani sio hapa sauti inatoka pale una mute, unanimutia msikilizaji wako kwani mimi nimekukosea nini. Kwani kama clouds ina mgogoro na Jay Dee basi huo mgogoro na wasikilizaji wa hiyo radio lazima waathirike? Ndio maana clouds inalaumiwa kuwa kuna mambo ya kitoto. Maana wao wanamfikiria mtu mmoja tu Jay Dee, badala ya kufikiria wasikilizaji wa radio ambao ndio wanafanya radio iwe hapo ilipofikia.
 
Hapa hakuna anayekomeshwa bali wanafuata amri ya mhusika! Hapa nimeuliza mara kadhaa, hivi ni wasanii wangapi wamewahi kufuta mistari ya msanii mwenzo baada ya kuingia nae kwenye bifu? Huyu Jide na Mwana-FA wana bifu vile vile, so what if ikiwa hata Mwana-FA nae hajiskii furahaa kusikia sauti ya Jide kwenye nyimbo zake? That's one but more important, nyie watu msijitoe ufahamu... msijifanye hamkuyasikia yale matusi ya Jide... sasa pale option ni moja tu, ama usipige kabisa nyimbo ambazo zina sauti ya Jide au u-mute sehemu alizoimba yeye! Kimsingi, haiingii akilini kutpiga nyimbo za msanii mwingine kwa sababu tu kuna sauti ya Jide... hiyo itakuwa kutowatendea haki hao wasanii! Lakini uki-opt kutopiga vipande vyaa Jide, jambo la kutopiga wimbo mwanzo hadi ni mwisho ni la kawaida sana studio... mara nyingi tu kila leo nyimbo zimekuwa zikipigwa verse moja na kuhamia kwenye wimbo mwingine... ni kawaida sana sehemu za wimbo kuwa muted kwa sababu yoyote ile kv matumizi ya lugha isiyofaa n.k kwahiyo suala la ku-mute kipande cha wimbo ni cha kawaida.... msikuze mambo! Ingekuwa mnampenda sana Jide mngekuwa mnamshauri aache jeuri lakini wakat ule ndo kwanza anatamba huku mashabiki wake wakimpa kichwa kwamba anaanzisha radio yake... alisahau, na mashabiki wake walisahau kwamba kuanzisha radio station ni kitu kimoja na kuifanya iwe ni station inayobamba ni jambo lingine! Ni miaka miwili sasa... Millardo Ayo ambae wala hatukuwahi kumsikia anapiga kelele ndo tunamuona anafungua studio!
Mkuu umeeleweka hasa hapo bold pia ndio umenifanya nikuelewe zaidi maana mie niliangalia bifu kati ya taasisi na individual huku upande mwingine wa individual bifu kati ya msanii na msanii sikuliangalia. Sie wengine tupo outdated hatujui kinachoendelea kivile katika sekta ya burudani kutokana na kukosa muda wa kusikiliza radio hasa mida ya mchana japokuwa mambo mengi tunayapata kupitia kwenye mitandao ndio maana unaona tunahoji na si kwamba ninaichukia hiyo radio na si kwamba pia ninampenda JD nilichokuwa naangalia kwa jicho la mlaji (consumer) kwa kuwa pamoja na kwamba tuna radio kibao nchini hakuna radio inaweza ikamridhisha kila msikilizaji na ndio maana unaona watumiaji huwa tuna mtindo wa kuhama hama hasa pale unapoona kuna kipindi flani huvutiwi nacho.
 
Hili la kwamba ku-mute ni kutowatendea haki wasanii wengine nimelizungumzia mara kadhaa! Kwa jeuri na matusi ambayo aliyatoa JD ni ngumu kwa kituo chochote kuruhusu sauti yake iwe kwenye wimbo wote au alioshirikishwa! Sina hakika ikiwa ulifuatilia lile bifu lakini kama hukufuatilia, siwezi kukulaumu! Hao wengine unaowasikia wanaleta hoja zao tena kwa matusi ni wale ambao kwa asili ni aina ya watu wanaojawa inda wakiona wengine wanafanikiwa na wengi wao ni wale ambao wanachanganya siasa na burudani! Kama sio msikilizaji mzuri wa radio labda nikujuze ndani ya Clouds kuna Ephraim Kibonde! Huyu Kibonde ni mtu ambae kinachopita kichwani mwake anakiachia kama kilivyo! Aidha yupo Hando, huyu nae huwa haogopi kusema ukweli! Sasa basi, kwa bahati mbaya kauli za Hando na Kibonde zimekuwa mara kwa mara zikiwakera wafuasi wa chama kimoja wapo nchini! Silika ya watu hawa, ili mradi umeingia maslahi ya chama chako watakuchukia tu...! Miezi ya karibuni hao watu walishaanzisha kampeni eti ya kususia kazi za baadhi ya wasanii kv tu wamejiunga kwenye chama asimu wao! Sie wengine tunaona huu ni ujinga... huwezi kuleta mambo ya siasa kwenye platforms zingine! Ni ujinga kuichukia Clouds eti kv tu baadhi ya presenters wake wamekuwa wakiongea mambo yasiyofaa dhidi ya chama chao... HUU NI USHAMBA!

Nikirudi why huwezi kuiachia sauti ya Jide kwenye wimbo usio wake! Hapo option ni moja tu... ama usipige kabisa wimbo wowote ambao Jide ameingiza sauti yake au u-mute vipande vya Jide! Kutopiga kabisa ni kutowatendea haki wenye nyimbo zao lakini uki-mute hapo hakuna jipya coz' studio suala la ku-mute au kukata kipande cha wimbo, video or even a film ni jambo la kawaida sana... suala la ku-mute vipande vya Jide sio la kwanza na wala halitakuwa la mwisho... na Clouds sio ya kwanza na wala haitakuwa ya mwisho! Zipo sababu mbali mbali za ku-mute kipande cha wimbo au hata kukiondoa kabisa... Clouds hapa wanatumia moja ya hizo sababu na wala hakuna jipya hapo ingawaje watu wanakuza mambo!
Umeeleweka mkuu
 
kubalini kataeni. clouds ndio kituo bora cha radio. wanamapungufu ya kiubinadamu. e fm naona wanajitahidi na kufikia clouds bado sana. millardayo mwenyewe alikimbia ipp media. mbona ipp media inawanyonya sana wafanyakazi haisemwi
 
Kama clouds waki mute basi sikiliza efm wataachia clouds ni media ya mtu binafsi siyo ya serikali na ndo Ruge akiamua leo piga gospel zitapigwa gospel mwanzo mwisho ila Kama wewe pera utaskiza tuu ata ipigwe mabata madogo wanaogelea
 
Mkuu mbona hauelewi? Mie sizungumzia beef lao,sipo hapa kama mshabiki wa Jay dee na wala sina chuki na clouds. Hata hivyo ni utoto kwamba uichukie clouds kwa sababu unampenda Jay dee au umchukie Jay dee kwa sababu unapenda clouds,hilo ni beef lao.

Kwahiyo naomba kwanza utambue kuwa sipo hapa kumshabikia Jay dee na wala sina chuki na clouds.

Hebu chukua mfano kama ile nyimbo ya Nay na Diamond halafu labda clouds wana beef na Diamond kama ilivyo kwa Jay dee. Au ile nyimbo ya Ali kiba na Jay dee single boy.

Hivi hizo nyimbo ukitoa sauti ya Diamond ktk nyimbo ya Nay, au utoe sauti ya Jaydee ktk nyimbo ya Ali kiba unafikiri kutakuwa na maana gani ya kupiga hizo nyimbo? Na muathirika hapo atakuwa ni nani ktk utoto wa aina hiyo?

Acha kuwa mgumu wa kuelewa. Ikiwa nyimbo unaweza ku mute na bado ikasikilizika na kuleta maudhui yaliokusudiwa kwenye wimbo husika wata mute sauti ya JD na kupiga wimbo. Na ikiwa ukii mute inapoteza maudhui basi haitapigwa kabisa.
 
Katika suala music industry wala hakuna utakachoniambia kahiyo kama wa kunyamaza unatakiwa wewe ndo unyamaze!

Unasema sijafanya utafiti kwa hoja ipi... hebu weka hapa huo utafiti uliofanya wewe! Unaleta habari za Dudubaya hapa kwahiyo waliompoteza ndio hao Clouds au? Ina maana hamna radio station zingine ambazo zingeweza kumweka juu? By the way, kwa nyimbo zipi hasa? Zile nyimbo za kusifia manundu ndo bado ulitarajia zingemweka kwenye chati? Suala la Nature nalifahamu kuliko unavyolifahamu wewe! Ni kweli kuna wakati Nature aliwazingua Clouds na wenyewe wakamzingua baadae peace ikafanyika na akarudi kwenye game! Tunaoifahamu Wanaume tulitabiri mapema sana kwamba haikuwa na muda mrefu kuparaganyika coz' yaliyokuwa yanaendelea maskani tulikuwa tunayajua na siyo ya kusimuliwa! Na kweli. muda haukupita, Nature na wenzake wakaondoka na fito zao wakaja kutiwa kiburi na mashabiki uchwara waliodhani unaweza kumshusha mtu kwa kuwarushia chupa za maji! Baada ya hapo, Nature ikawa historia... bora hivi sasa wapo in good terms na Fela huenda akarudi upya!

Una lingine?

its more than that mzee.mimi nasimamia wasanii 2.mmoja ni mkubwa sana kuna mambo siwezi kuyaweka humu.AM IN
 
Mkuu umeeleweka hasa hapo bold pia ndio umenifanya nikuelewe zaidi maana mie niliangalia bifu kati ya taasisi na individual huku upande mwingine wa individual bifu kati ya msanii na msanii sikuliangalia. Sie wengine tupo outdated hatujui kinachoendelea kivile katika sekta ya burudani kutokana na kukosa muda wa kusikiliza radio hasa mida ya mchana japokuwa mambo mengi tunayapata kupitia kwenye mitandao ndio maana unaona tunahoji na si kwamba ninaichukia hiyo radio na si kwamba pia ninampenda JD nilichokuwa naangalia kwa jicho la mlaji (consumer) kwa kuwa pamoja na kwamba tuna radio kibao nchini hakuna radio inaweza ikamridhisha kila msikilizaji na ndio maana unaona watumiaji huwa tuna mtindo wa kuhama hama hasa pale unapoona kuna kipindi flani huvutiwi nacho.
Unajua ndugu yangu, ni kweli kabisa kwamba hapa kuna wengine hawaelewi kabisa what's going on na hata kuhoji kwao wala hakuna maana yoyote mbaya kwahiyo sitashangaa kusikia hata wewe wala hukuwa na nia mbaya yoyote! Hata mleta mada mwenyewe, wala haielekei kwamba nae ana negativity na Clouds lakini hapa jamvini pia wapo members tena wengi tu, hawa hata siku moja hutawasikia wakisema zuri la Clouds... wao mara zote Clouds ni radio ya mashoga, au hili na lile... ukiwauliza ikiwa wamewahi kum'---- prenter yeyote wa Clouds hakuna hata mwenye jibu.... mbaya zaidi wengi wao hata presenter wenyewe wanaishia tu kuona picha zao kwenye mitandao ya kijamii au sana sana kwenye tv... lakini hapa watajifanya wanawajua mwanzo hadi mwisho lakini kuwajua kwao ni upande wa uovu peke yake... sasa mtu kama huyo sidhani kama tafsiri sahihi inayomfaa zaidi ya kuwa ni mtu aliyetawaliwa chuki! Nchi kuna wengine hawapendi kabisa kumuona mwenzao anapiga hatua... mfano mzuri chukulia mfano wa mwanamuziki Diamond (ikiwa ni mfuatiliaji)! Unakuta mtu anaonesha chuki ya wazi wazi wakat hata huyo Diamond mwenyewe hajawahi kumuona zaidi ya kusihia kumuona kwenye tv!

Kwa upande mwingine kuhusu hao Clouds, hapa kuna member wa kutosha tu ambao chuki zao dhidi ya Clouds inasukumwa na ushabiki wa kisiasa... hakuna lingine! Sie wengine tunaona ni ujinga kuchanganya masuala ya siasa na burudani na ndio maana ukumbi wa Billicanas unamilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA lakini sidhani kama kuna siku umewahi kusikia wafuasi wa vyama vingine wanaipiga vita Billz kwa sababu tu mmiliki wa ukumbi huo ni mwenyekiti wa chama kingine!
 
its more than that mzee.mimi nasimamia wasanii 2.mmoja ni mkubwa sana kuna mambo siwezi kuyaweka humu.AM IN
Sijakuomba unitajie nafasi yako kwenye music industry coz' hapa tunatumia fake ID kkwahiyo haisaidii! Nilichokutaka uniwekee huo utafiti uliofanya wewe coz' nimekujibu hoja zako kuhusu akina Dudu Baya na Juma Nature! Na kama kweli unasimamia wasanii basi unafahamu jinsi wasanii wengi wa Tanzania walivyo kimeo na ndio maana huwa nashangaa sana ninaposikia kwamba eti wanapewa stress na Clouds! Kama kweli unasimamia wasanii basi unafahamu kwamba majority ya wasanii ni wavuta ganja tangu huko walikotoka! Zamani sana, mwishoni mwa miaka ya 90 nilipoenda studio kwa mara ya kwanza nilishangaa nilipokuta bonge la fuko la ganja... haikuwa ya kuuza bali watu kuvuta! Sasa watu kama hao kesho na kesho kutwa wakigeukia drugs, lawama kwa Clouds kwamba eti wanawapa stress...? Kuna mtu hapa juzi kaleta uzi kuwalaumu hao hao Clouds kwamba eti wanajifanya kutangaza kifo cha Mez B wakati walikuwa hawapigi nyimbo zake... mtu unashangaa ni nyimbo zipi hizo!!
 
Hiv mtu akishirikishwa kwenye wimbo, unakuwa wa kwake? Hiv kwamba akisema nyimbo zake zisipigwe na hizo pia kazijumuisha?

Sasa c atakuwa na bifu hadi na waliomshirikisha? Au vp, kama kuna ufafanuzi zaidi naombeni.
 
Habari Wanabodi,

Nipo nasikiliza Clouds FM kipindi cha XXL Segment ya "Album Review". Leo wana Review Album (2003) ya Mwana FA ya "Toleo Lijalo" yenye nyimbo kama 'Wanapendana', 'Alikufa kwa Ngoma' etc. Kwenye wimbo wa 'Alikufa kwa ngoma' ameimba na Anaconda (Lady Jay Dee) cha kushangaza kwenye huo wimbo wakati wana review ikifika sehemu ya chorus ya Jide wana-mute inasikika beat tu. Kitendo cha Clouds FM kama taasisi kampuni nzima kuweka beef na msanii mmoja inajidhihirisha Clouds FM ni radio ya wahuni tu.

Clouds FM sio mara ya kwanza kufanya upumbavu huo, nakumbuka kipindi cha nyuma Inspector Haroun alienda nao tofauti, kipindi hiko wimbo wake wa "Buzi" ndio ulikuwa una-hit basi jamaa kila ikifika pale anapochana Inspector sauti wanaondoa inasikika beat tu.

Kwenye ngoma ya Ben Pol "Jikubali" kuna moja ya mstari unaimbwa "Nampenda Lady jay Dee,namzimia Zitto" ile sehemu ya neno Lady Jay Dee wanaisugua (Scratch) na ilo neno halisikiki kabisa.

Kwenye kuadhimisha miaka 15 ya Dully sykes, kwenye promo walikuwa wanapiga nyimbo za nyuma za Dully Sykes, kuna ngoma inaitwa Bijou inavyoanza ina neno "Okay mbili sifuri sifuri nne, P-funky kinywele kimoja" ilipoanza hapo kwenye P-funky wakaikata kabisa wakaipeleka mbele.

Kwa Mchezo huo wa kitoto unaofanywa na Clouds Media inaishushia hadhi sana hiyo kampuni. Kitendo cha kampuni hiyo kufanya mambo ya utoto ni wazi redio inaendeshwa na makanjanja na sio watu wenye weledi. Clouds FM ikubali pia matakwa ya wasanii, kama msanii akikataa kufanya deal kwa sababu anaona haimfaidishi yeye ni haki yake kukataa na si kigezo cha kutopiga nyimbo zake.

Kuna watu watasema kwamba redio zipo zaidi ya 60 na TV zaidi ya 20 kwanini wasanii wailalamikie Clouds tu? Hapa tunacholalamika ni kufinya (mute) sauti yeyote iliyopo kwenye nyimbo alizoshirikishwa msanii walioenda nae tofauti. Kama wanapiga wimbo wa Ben Pol waachie wimbo kama ulivyo na si ku-mute majina ya watu waliotajwa wenye beef nao.


CLOUDS MEDIA ACHENI UTOTO.

Huko mimi nasikiliza kipindi cha NJIA PANDA tu vingine vyote tupa kule
 
Hiv mtu akishirikishwa kwenye wimbo, unakuwa wa kwake? Hiv kwamba akisema nyimbo zake zisipigwe na hizo pia kazijumuisha?

Sasa c atakuwa na bifu hadi na waliomshirikisha? Au vp, kama kuna ufafanuzi zaidi naombeni.

Ni kama kwamba imetokea siku wewe umegombana na jirani yako na hadi mkawa hamsalimiani, halafu rafiki zako wanapokuwa wanakuja kwako na wakamuona jirani yako(ambaye wewe umegombana nae) na wakawa wanamsalimia basi wewe hupiga kelele ili zile salamu zisisikike kwa sababu tu wewe una ugomvi na huyo jirani yako.
 
Ni kama kwamba imetokea siku wewe umegombana na jirani yako na hadi mkawa hamsalimiani, halafu rafiki zako wanapokuwa wanakuja kwako na wakamuona jirani yako(ambaye wewe umegombana nae) na wakawa wanamsalimia basi wewe hupiga kelele ili zile salamu zisisikike kwa sababu tu wewe una ugomvi na huyo jirani yako.

Hiyo nayo ni akili kweli, mtoa mada alivyosema UTOTO yupo sahihi kumbeeeee!!!
 
Hata kama Jdee alisema, Clouds sio kaz yk kujibizana ya mtaani.jenga chuki na maisha kw kufanya kazi, sio kujenga na wasanii kw kufanya uzandik wa kishamba.sio mpnz wa bongo flavr ila wanachokifanya ni uswahili, utoto, na ni primitivity.
 
Na hiyo unawatenga wasanii hakuna atakaeimba nae kwa kuhifia wimbo wake kuchezwa kutuoni hapo
 
Mi na clouds sijui vipi.? Kwanza ataiyo tv yao sijuagi wanaonyesha nini huko. Imeanzishwa mda lakin mpaka sasa haina vipindi bora vyakusema ukae chini utizame
 
Sasa anaposema nyimbo zake zisipigwe ni kwamba anawaambia akina Ruge au Joe hapo? Ruge anakaa studio? Kusaga aanakaa studio? Tangu lini Ruge au Kusaga akapiga nyimbo studio? Kwanza yeye hakusema Ruge au Kusaga wasipige nyimbo zake bali alisema Clouds wasipige... sasa Clouds ni mtu au taasisi? Alitaja majina kwenye msiba... hapa alisema wazi kwamba siku Jide akifa, Joseph Kusaga na Ruge wasikanyage kwenye msiba wake na kwamba wakienda, watu wawapige
mawe!

Alichosema nyimbo zake zisipigwe, hiyo nyimbo ya alikufa kwa ngoma ni ya Mwana FA, JD kashirikishwa tu. Unapomute chorus kwenye nyimbo unaharibu taste ya wimbo wote. Wasipige zile ambazo ni za JD mwenyewe lakini siyo zile alizoshirikishwa
 
Alichosema nyimbo zake zisipigwe, hiyo nyimbo ya alikufa kwa ngoma ni ya Mwana FA, JD kashirikishwa tu. Unapomute chorus kwenye nyimbo unaharibu taste ya wimbo wote. Wasipige zile ambazo ni za JD mwenyewe lakini siyo zile alizoshirikishwa

Jd ashagombana na mwanafa hata hawasalimiani. Hivyo ukiacha ugomvi wa jide na clouds bado kuna ugomvi wa jide na mwanafa. Sijui unapata picha gani hapo? Ku-mute chorus ya jide kwenye wimbo wa mwanafa ni sawa kwani jide hana mahusiano mazuri na mwenye wimbo. Tatizo mmeshupaa kubishania jambo dogo ambalo hata mtoto wa darasa la kwanza ukimfundisha anakuelewa. Hapa ndipo mnanikumbusha ule msemo wa prof.Kabudi wa 'tofauti kati ya mjinga na mpumbavu'.
 
Back
Top Bottom