Clip ya sauti inayodaiwa ni maongezi ya simu ya Wanasiasa William Mganga Ngeleja na Nape Moses Nnauye yavuja

wanao release hizi audio ni mabwege sana.

hawajui namna nzuri ya kucheza na audience yao.

kitendo cha ku release audio mbili ndani ya kipindi kifupi kinadhoofisha ile audio ya kwanza na kufanya series yao yote ionekane ni utoto.

wangekuwa na delay period ya kama wiki mbili au tatu igizo lingeenda vizuri sana.
πŸ˜‚πŸ˜‚ko mkuu umeifanya prison break kabxa yan
 
Sasa nimeamini kuna Ushamba somewhere

Sasa ni kwa faida ya nani kudukua simu za watu?

Ni another tactic hii ya kuwatisha Wana CCM wasijadili yanayojiri ktk chama chao!

Hapo hakuna cha demu wa Kizaramo wala nini ni vyombo vyenye power za kudukua Sauti ndo vinalikisha hizi sauti
 
NGELEJA HIVI UNAKWAMA WAPI BROTHER? WEWE NI WA KUINGIZWA MKENGE NA MAMLUKI NAPE

Unakwama wapi brother? Labda ndio swali la kuanza nalo wakati huu mfululizo wa video zilizoleak kutoka kwa Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye unavyozidi kuwaumbua vigogo.

Safari hii Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amenaswa akiteta na Nape kuhusu masuala ya chama na Serikali.

Ngeleja anasikika akiunga mkono waraka wa Kinana na Makamba uliochafua hali ya hewa nchini.

Ndio maana nauliza tena unakwama wapi brother Ngeleja?

Wewe si ndio uliaminiwa na nchi ukiwa mmoja wa vijana wadogo lakini ukapanda hadi kuwa Waziri tena wa Wizara nyeti kama ya Nishati na Madini?

Si ni wewe huyu huyu ukautumia Uwaziri wako kishamba sana ukijinufaisha na kuingia mikataba ya kipuuzi na wawekezaji wa nishati na madini?

Nakumbuka hata sakata la Dowans umo na uliitetea sana kisha ikaja Escrow umo; ambapo ulichota milioni 42. Umesahau?

Katika mazingira tata na ili kujiokoa na Segerea ghafla miaka miwili iliyopita ukatangaza kurejesha fedha za Escrow (baada ya kuzizungusha kibiashara na kuzalisha faida);

Yote haya Serikali tukufu ya Chama cha Mapinduzi imekusitiri haujaenda Segerea.

Leo unakwama wapi hadi uungane na wasaliti wa aina ya Nape kusaliti juhudi za nchi?

Brother unakwama wapi?Je, ulikuwa unajipendeleza tu kwa Nape na Kinana au au ndio kusema nawe umetumwa na mafisadi waliokuwa wanakutumikisha ukiwa Waziri wa Nishati na Madini?

Brother usifeli kirahisi na kizembe hivyo Nape ana faili lake na wewe unafaili lako.

Kila mmoja apambane na hali yake; pambana kuwa mtu wa maana na acha kupambana kuwa mpumbavu.

Yani wewe Ngeleja ni mtu wa kuwa kwenye mipango ya kutala kuipindua Serikali ya Awamu ya Tano?
Kweli?

Yaani ndio umefika hapo brother, simple tu na kizembe zembe hivyo? Dah!

Alamsiki.
Mbona unafeli...Mbona unamuogopa Mussiba
 
Ndiyo sababu huyo mpuuzi alikuwa anaachiwa kufanya upuuzi wake kwani tayari kuna mkakati mzito wa kuwachafua wale wanaompinga kwamba hastahili kupewa awamu nyingine ya 2020 to 2025.

FAKE NEWS!

Yaani flow yao imekuwa staged kabisaaa , Nape usikubali na wewe, tafuta actors uwaundie zengwe maadui zako(unawajua)
 
Kama ni makampuni ya simu yameleak hizi information.Kweli watanzania hatupo salama.Yani wazee wa kitengo wameanza kutap conversation za Meko Enemies.Dah.Hii hatari aisee.

Nimesikia hapo kwenye maongezi Mzee Kinana hatumii mitandao ya ndani.Anajua michezo wanayofanya wazee wa Kaunda suti.

Hila yote kayataka JK.
 
Back
Top Bottom