CIIE: Fursa nyingine kwa nchi za Afrika kutangaza na kuuza bidhaa zao katika soko la China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111258465519 (1).jpg


VCG111258465520.jpg

Maonyesho ya Kimataifa ya Uingizaji Bidhaa kutoka nje ya China (CIIE) yameanza mjini Shanghai, China, na nchi kadhaa zinashiriki maonyesho hayo na kutangaza bidhaa maalum za kipekee zinazopatikana katika nchi hizo ili kuweza kuvutia wateja nchini China.

Nchi za Afrika ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki katika Maonyesho hayo, lengo kuu likiwa kuingia na kuliteka soko kubwa la China lenye watu takriban bilioni 1.4. Bidhaa kutoka nchi za Afrika ikiwemo kahawa, maharage, pilipili, na matunda, zinatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika soko la China.

Inafahamika kuwa bara la Afrika limejaaliwa kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba, nguvukazi kubwa, na hali ya hewa nzuri, licha ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Lakini changamoto kubwa inayolikabili bara hilo, ni mchakato mzima wa sekta ya kilimo. Changamoto kubwa inayozikabili nchi za Afrika, ni uwezo wa uzalishaji utakaokidhi soko kubwa la China.

Nchi nyingi za Afrika bado ziko nyuma katika teknolojia ya kilimo cha kisasa, na kutokana na mahitaji makubwa katika soko la China na hata dunia, ni lazima kwa serikali za nchi husika kuwekeza zaidi katika sekta hiyo ambayo ni uti wa mgongo wa chumi nyingi za Afrika.

Bidhaa nyingi zinazotoka nchi za Afrika zinashindwa kuingia kwenye ushindani wa kimataifa kutokana na sababu ambazo zinaweza kuzuilika.

Ili kuwezesha bidhaa hizo kutoka nchi za Afrika kuingia kwenye soko la China, nchi hiyo imepunguza ama kuondoa ushuru wa forodha kwa bidhaa hizo, ikiwa ni ahueni kwa wafanyabiashara wanaotaka kuuza bidhaa zao nchini China.

China, kwa upande imechukua hatua kihalisi kuziwezesha nchi za Afrika kuingia kwenye soko lake kubwa, kinachosubiriwa ni nchi za Afrika kutumia fursa hiyo vizuri kutangaza na kuuza bidhaa zenye ubora kupitia maonyesho hayo.

Umefika wakati kwa serikali za nchi za Afrika kufanya mageuzi makubwa katika sekta hii ya kilimo, kuanzia maandalizi ya mashamba, kilimo, mavuno, uhifadhi, na ufungishaji wa bidhaa. Nchi hizo zinapaswa kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya soko kubwa la China, na hivyo kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, familia, na kuinua uchumi wa taifa.

Shime sasa kwa serikali za nchi za Afrika kuondokana na kilimo kilichopitwa na wakati na kuwekeza katika teknolojia za kilimo cha kisasa ili kuweza kushindana katika soko hili kubwa la China.
 
Umenena kweli,ila kwa afrika kulifikia soko la china inahitaji nguvu ya pamoja kati ya china na afrika,na hilo litawezekana ktk mkutano wa china na afrika ( FOCAC) utakaoanza mwezi huu.
 
Back
Top Bottom