Marekani imeamua kuwawekea vikwazo vya kiuchumi watu 17 ambao ndo wametolewa kama mbuzi wa kafara.
Humo wamo mshauri wa zamani bwana Saud al-Qahtani, mshauri mwandamizi Maher Mutreb, na balozi wa Riyadh mjini Istanbul bwana Mohammed al-Otaibi.
Lakini yule Mmatumbi meja jenerai Mohammed al-Assiri ambae aliwahi kuwa naibu mkuu wa idara ya usalama ya Saudi Arabia yeye amepona na hataguswa.
Al Assiri yupo kwenye "inner circle" ya mwana mfalme na ni mwanajeshi wa ngazi za juu kabisa kwenye jeshi la nchi hiyo.
Kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba hao wauaji walikuwa ni wafungwa wa makosa makubwa kama ya mauaji na walitumiwa kwa kazi hiyo ambayo iliratibiwa na hao niliowataja hapo juu, ingawa hakuna ushahidi.
Hivyo wafungwa hao inawezekana wanasubiri kunyongwa kabisa kumaliza kazi na maisha yataendelea.