Chuo Kikuu Dar es Salaam kinatia aibu

Chuo Kikuu Dar es Salaam kinatia aibu

Hayo mapungufu yapo Library yote. Ujengaji wa Library ya UDSM haukutia manaani kuwekwa kwa viyoyozi. Sijaingia humo ndani miaka ya karibuni tu. Kama kumebadilika basi hongera.

Naingia hofu unaposema library ya UDSM ni kubwa Afrika Mashariki na Kati. Inawezekana ni ukubwa wa majengo, lakini kma hata tukichukulia wingi wa vitabu ambavyo vipo up-to-date na majarida basi hiyo Afrika Mashariki na Kati imekwisha kabisa. Tulie tu.

Serikali ya CCM haikuwekeza kabisa kwenye kununua vitabu kwa ajili yya Library ya UDSM. Miaka michache iliyopita UDSM walikuwa wanaponea coupon za UNESCO. Sijui kama wanaendelea na hilo.

Sehemu nyingine inayoonyesha UDSM wapo hoi tabaani kitaaluma ni vitabu vya kiada(textbooks?). Zaamani tulikuwa na Bookshop pale Mlimani. Leo hii imekufa. hawa wanafunzi tunaowafundisha pale mlimani wanasoma vitabu gani?



wacha ufala ww bookshop ipo km kawaida!
povu la nn xx km huna taarifa
 
Ndio maana nikakuandikia labda Yesu ashuke, huyu aliyegomewa Havard hasira anakuja imalizia kwa vijana wengine kama hao toka kwenye hivyo vyuo tajwa.

mfano: SHule ya Sheria UDSM wanatoa LL.B na BALE huyu wa BALE hata apate GPA ya 5 kubakizwa ni ndoto kwake, wakati huo huo mtu wa LL.B anabakizwa kwa ajili ya wanafunzi wa BALE😀
hii ndio UDSM CHUO KIKUU CHA TAIFA
Kinawabagua watu wake wenyewe, ila kama mdio mentality yao!! Worry out
 
wacha ufala ww bookshop ipo km kawaida!
povu la nn xx km huna taarifa

Sijui wewe ni nani na unajua nini kuhusu Bookshop. Na inawezekana kabisa Bookshop ya Chuo Kikuu imebadilika tokea nilipoitembelea miaka kama miwili iliyopita. Nitaitembelea tena hiyo Bookshop mwezi July mwaka huu nione hayo mabadiliko. Nitakueleza tena nilichokiona.

Nilichokiona kwenye ile Bookshop miaka kama miwili iliyopita ni kutokuwepo kwa vitabu vyovyote vya maana ndani yake. Bookshop ilikuwa imejaa "Kindergarten Colouring Books". Hata hivyo vilikuwa vimezagaa tu bila kupangwa vizuri. Vumbi ndani ya hiyo Bookshop vile vile lilikuwa limezidi sana
 
Nyie mnashangaa UDSM hivi mngeenda DIT si ndio mngezimia kabisa
 
Kenyatta amesoma usa na kingereza chake kizuri lakini haoni ndani kwa magufuli kwa utendaji wenye tija kwa jamii, zuma kule afrika kusini na kingereza chake, M7 etc,
Magu kaleta tija gani? Unajua aliyofanya Kenyatta Kenya mpaka sasa? Anacholalamikiwa Kenyatta ni safari nyingi kama za JK, sasa Magu mpaka sasa alichofanya nini kumlinganisha na hao.
 
Zamani tulikuwa na chuo kimoja kwa sasa vyuo vimeongezeka vipo vinavyofanya vizuri na wengine wanaharibu elimu, kwa msingi huu wa kuwa na vyuo vingi kinachotutofautisha sokoni ni uwezo binafsi wa mtu aliopata chuo, huu si muda wa kutegemea kubebwa na jina la chuo, Atakaefanya vizuri ataenda mbele atakaesubiri kubebwa na jina la chuo Sidhani kama lina msaada kwenye competitive market.
 
karibuni Ruaha Catholic University Iringa mpate wataalamu bora na wasomi wanaokwenda na wakati acha na Udsm chuo kikongwe ambacho vifaa vya practical vimechakaa yan havifai walimu nao jipu yamebaki ma golf tuu pale ndugu amken acheni kulala.
hayo tuu kwa asubuhi hii.. Mungu awe nanyi wote.
 
Kwanini tunakuwa wakulaumu kiasi hiki.Hivi wote kwenye GPA kuwa mnataka mkafundishe vyuo halafu sector nyingine zichukue makapi? Tumeona tatizo LA ubovu Wa miundombinu kweli hili hakuna anayepingana nalo lakini ushauri Wa mini kifanyike ni kipimo cha usomi wetu.Binafsi nipo against na dhana yakufikiri kila kwenye GPA kubwa ni bora kuliko wengine Kwa hoja ya uwepo Wa bongo na unyanyasaji katika mitihani.Kwangu napendekeza kigezo hicho kiondolewe na badala take watu wapimwe Kwa content waliyo mayo na so vyeti kujaa A hata zile zakuvuliwa chupi.I still have a trust in my university which is the peak of all professions
 
Acha kuongea upupu wewe....nmesoma udom 1st degree nkasoma udsm post graduate...nlichojifunza udsm mnakalili sana...yan ww kalili tu haijarish umeelewa au lah...tena mitihan mnarudia ..kuanzia test had Ue ..yan kama ilivyo wanachange date tu
Ukweli udsm jina tu...but hakuna lolote
nmesoma hliiapo nmepata gpa/grades ambazo sijawah pata maishan...
Watu muwe na logic...afu uwez dharau chuo flan wakati huna hata experience umesoma chuo kimoja tu unaamin ndo iko iko bora..
Wanafunzi wa udsm sifa nying..
Kama wewe ni bingwa wa kukalili ukienda udsm lazima utusue! Hilo halina ubishi! Nilijifanya nataka kuelewa nilicho ambulia ni tiketi za"September conferences" za kila mwaka. Watu wanakalili hadi physics na mwisho wa siku wanapata A. Kwa wale wanaosoma masomo kama psychology ni uwezo wako wa kukalili madesa tu! Read between lines!!! Haukosi A.
 
ubaguzi je!, kutopenda kubadilika je! , kudharau wataalamu wa vyuo vingine hata kama wako vizur kuliko wa kwao je!, ukiritimba je!, chuki binafsi kuzihamishia kwenye masomo nakufelisha wanafunzi je! , kutumia mifumo ya zamani ilopitwa na wakati je! (traditional approach badala ya communicative approach) je, kufurahia wanafunzi wa masters&phd wakichelewa kugraduate hata kama wanavigezo je! ( IN LOWASSA WA UKAWA'c voice) [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Mkuu umeongea point nyingi mno. Kuna wazee pale udsm wanaona wao ndo hujua kila kitu, ukiangalia Elimu yake ya kuunga Unga diploma mpaka PhD, wengi wao wamekalili madude so wanawaforce nanyi mkalili.
CONAS inaongeza kwa ukiritimba na uonevu haswa Chem department hawa jamaa wamenicheleweshea kuanza maisha kwa kunisomesha degree miaka minne
 
Tanzania inahitaji haki elimu ya vyuo vikuu. TCU peke yao kuna vitu wanafumbia macho. Si UDSM wala vyuo vichanga vingi vina majipu yake.
 
Kwa chuo kikubwa kama UDSM n.k. kuendelea kuitegemea Serikali Kuu kufanya renovation kwenye vyoo ni utahira wa kiwango cha PhD.

Kama ningekuwa VC ningefanya yafuatayo badala ya kuendelea kusubir fedha za kukarabati vyoo zitoke hazina kuu.

1. Kutumia rasilimali zilizopo vizuri na kwa weledi. Kwa mapato yote ya ndani ningetenga asilimia kadhaa kukarabati miundo mbinu ya umuhimu kama vyoo, lecture halls, barabara na kuhakikisha mawasiliano ndani ya chuo yanakuwepo muda wote.

2. Alumni Mobilization
Chuo kama UD kina alumni all over the world. Na kuna ambao wapo tayari kukisupport chuo kisongembele. Ningehakikisha wote waliosoma UD wanakuwa na platform ya pamoja na kuanzisha mfuko maalumu wa maendeleo ya UD.

3. Matumizi yenye Nidhamu
Haingii akilini chuo kinakuwa na V8s ambazo ni gharama kuzinunua na kuziendesha halafu unakuta wanafunzi wanategemea kwenda msalani mcity. Ningebana matumizi na kufuta matumiz yasio ya lazima ili kinachobaki kikaboreshe UD kwa faida ya wengi.

4. Bulk Purchasing
Kwa mafuta ya magari, stationaries, na vitu muhimu vinavyotumika chuoni kila siku. Hii itasaidia kusave kwenye manunuzi.

Me naamini kabisa kwa hivi vyuo vyetu vikubwa vikiamua kujiendesha venyewe vinaweza kabisa. Vina Rasilimali (Watu & Asset) nyingi sana.

Uwezo Vinao, Sababu Vinayo, Nia_________
Taja rasilimali inayoweza ingizia chuo pesa ili hali watu wanasoma kwa pesa kidogo karibia na bure!. Au ubataka waanzishe mashamba ya kilimo???
 
Back
Top Bottom