Chuo Kikuu Dar es Salaam kinatia aibu

Chuo Kikuu Dar es Salaam kinatia aibu

Shikamoo Mzee Wa udsm. Kwenye swala LA GPA hapo ndipo heshima IPO.....

GPA ya SaUT ya 4.8 ni sawa na 1.8 ya udsm ha haaa,.
Wewe hata GPA hujui ni nini, utaweza kulinganisha vyuo? Waungwana wa UDSM chukueni maoni ya wanajf, fanyia kazi ili tusonge mbele ktk taaluma Tz. Hakuna chuo kusicho na mapungufu Tz. Hata vyuo vya ulaya, USA nk vina mapungufu. Toa mchango wa hoja za kujenge sio kudharau chuo, kukejeli na kutusi.
 
Hii ni kweli mtoa mada kanena, hasa upande wa siasa, maaana hata wale wote waliotokea udsm na kwenda kuwa viongozi wa nchii zao wameenda kuhalibu mambo kwa mfano museveni wote wamekuwa viongozi wasiopend mabadliko naa wababe na kujiita makombredi wa kupora madaraka kwa hila na ubabe na kuhalibu mifumo ya kidemokrasia kwa makusudi na ndio maana hata chuo chenyewe hao wanaongoza hawataki hata kubadilika na kufundisha mambo mapya yaaliyo na tija kwenye jamii.
Nawakilisha.
 
Nafkiri watoa mada wengi labda hawajasoma pale udsm pako hivi watu wanakosa muda Wa kufanya rally za usafi desa gumu na kuhusu website's in active dah...matangazo huwa ktk notice board tuu watu wapo busy sana wakiingia web ya chuo ni aris tuu kuchek matokeo. Vyoo vibovu but watu wanawai lecture asubui afanyaje ? Na kuhusu walimu kuwa walewale kinachoangaliwa ni ubora sio wingi bila 3.8 huwezi kuwa academic staff na km umetoka St.s au cjui wapi lazima wakupime kwanza na wengi hudondoka ktk hizo measures
usafi wa vyoo na kuwahi lectre vnahusiana vip ilihali usafi wanafanya wafanyakazi walioajiriwa pale?kiukweli swala la vyoo kwa udsm ni wamefail kitambo
 
usafi wa vyoo na kuwahi lectre vnahusiana vip ilihali usafi wanafanya wafanyakazi walioajiriwa pale?kiukweli swala la vyoo kwa udsm ni wamefail kitambo
What I meant is watu wako bize na desa na kitabu ni kigumu kuhusu maadili kiukweli yanafundishwa na mwanafunzi wanafundishwa ku argue ndo maana maandamano ya pale si kama ya vyuo vingine huwa yana resonable argument na kuhusu maadili yanafundishwa ingawa ni jukumu la individual kuyafuata.
 
Miaka fulani nilikuwa naona akiingia mkuu fulani magogoni anabadilsha na makamu mkuu wa chuo.
Miaka hii hivi hakuna?maana namkumbuka Yule aliyebadilishwa na mkapa,na alipoingia JK akampa huyu aliyepo.
Anko MAGU kama hajatupia jicho huko kwa kelele hizi basi amkazie afanye kweli.
 
kinachoshangaza pamoja na mambo mengine ni jinsi wahitimu wa udsm wa phd, masters, n.k. wasivyoweza kuongea au kuandika kiingereza kilichonyooka (...mfano, reajea ile horror show majuzi kule arusha).
Kenyatta amesoma usa na kingereza chake kizuri lakini haoni ndani kwa magufuli kwa utendaji wenye tija kwa jamii, zuma kule afrika kusini na kingereza chake, M7 etc,
 
Dear graduates wa udsm, msiwe diehards wa hiki chuo, tunafahamu kuwa kila mtu atatetea chuo alichosoma, ila kwa hili, mtoa mada ana nia nzuri na chuo chetu hiki, tunahitaji kuona mabadiliko. Hiki chuo kikiboreahwa kitakuwa ni bora Africa nzima,
Mazuri ya udsm yapo, ila mabaya yapo ambapo yanahitaji marekebisho,
For sure baadhi Graduates wa udsm kwenye hii thread mnatutia mashaka, this isn't what we expected from you, remember when you think you are 100% right and others are 100% wrong, u will never change anything.
 
Sa
Kutoka kwa maoni ya wachangiaji.
1. Udsm ni chuo kinacho pinga mabadiliko.
2. Kozi nyingi zimepitwa na wakati na kozi mpya zenye uhitaji ktk soko hazifundishwi.
3. Chuo kimekosa ubunifu ktk maeneo yote hasa ktk swala la mapato.
4. Miundo mbinu ni mibovu na haifai kwa matumizi ya wanafunzi.
5. Damu mpya haina nafasi ktk kuleta mabadiliko ya kweli.
6. Hakuna vitabu vya kutosha.
7. Tafiti za udsm ni tasa kwa maana hazizai chochote.
8. Utawala ni kama umekata tamaa na kuishi kwa liwalo na liwe mradi siku ziende.
9. Chuo kina ubaguzi sana hasa kwa watalaam wanao toka vyuo vingine.
10. Chuo kimepoteza mvuto kielimu.
11.
12.

mwanzo wa thread.
UDSM ni jipu na lisipo angaliwa litapasuka lenyewe . Sijui kama kuna utawala wenye dhamira ya kweli ya kuiletea Tanzania maendeleo au kuna wapiga pesa wanao furahia kutumia VX , V8 na kuchupokea mshahara kila mwezi. Hadhi ya chuo haifanani na mazingira halisi yaliyopo, sijui watu wanasomaje hapo udsm.

Mfano
Ivi udsm pamoja na kuwa chuo cha kwanza kufundisha computer science hapa nchini, kwanini imeshindwa kuwa na website inayo lingana na hadhi yake. Website haina content, ipo offline most of the time, content zake nyingi ni static, poor design etc

Nikiangalia vyuo vya level yako kama Nairobi, Makerere etc vina website nzuri zimeshiba information. Labda wahusika kama wapo hapa watwambie shida ipo wapi?

Mfano kwa muda wa wiki 3 sasa website haipo hewani, ivi wahusika wanalionaje hilo kwa nyakati za leo ambazo information ndio mtaji wa biashara huwezi kaa gizani na ukajisikia vizuri, Mnajua mmepoteza fedha kiasi gani kwa kukaa offline?

Inavyo onekana udsm ni chuo ambacho kipo static sana. hakibadiliki, hakitaki mambo mapya, sijui ni uzee wa staff au ukiritimba usio na maana. oneni wenzenu wa nairobi na makerere mambo yao yapo so dynamic hata machango wao ktk jamii unaonekana mfano mzuri ni basi linalo tumia jua lililo zinduliwa juzi.

UDSM ukiacha kuandaa wana siasa (jipu) ambao ndio wamelipoteza taifa hili na bara la africa, hakuna kitu cha maana kilicho fanyika ktk maeneo mengine. Miaka yote wasomi wamekaa hapo udsm nadhani kazi kubwa ni kupokea mishahara, matokeo ya research yapo wapi?

Chuo kimepoteza mvuto kabisa, zamani kilikua chuo pendwa africa, watu walijisikia uoendeleo kusoma udsm, leo wanaunzi wangapi toka nje wanasoma hapo udsm na hao waliopo wanajisikiaje?

Ukiangalia vyuo vya jirani zetu tuu hapo karibu wapo vizuri na wamejipanga, kozi zao wanaenda na wakati na kozi zinazo endana na soko la ajira. udsm kozi zilezile miaka nenda rudi, hii ni shida. Madudu ya chuo hiki ni mengi huwezi kuyamakiza kwa siku moja.

Binafsi wahusika wachukue hatua, udsm ni chuo chenye hadhi na kinachukua sura ya taifa letu.

Ipo siku nafasi hii itachukuliwa na chuo kingine kwa uzembe kama huu

tabutupu.
Sasa huoni ungemtafuta Mkandala umueleze hayo ingesaidia!Hapa unaleta porojo na masimango tu
 
Rushwa ya ngono na rushwa ya pesa ili mwanafunzi afauru mtihani. It's very shame no one is shouting on this. Our education soon will go to hell.
Wataalamu wa namna gani tutawatengeneza? How are they going to be competitive in East Africa and the current world market?
 
Chuo cha institute of adult education ni jipu lililoiva shemeji kasaini boom anakaaa mwezi mmmoja mpaka Leo anakamilisha hajapata boom na pesa zimeshaingia kwenye account ya chuo chao mbona udsm tuna afazari
 
BALE ni Bachelor of Arts in Law Enforcement, yenyewe inahusika na Law Enforcement tuuu,

Watu wote waliosoma LLB wanasoma law enforcement ndani ya kazi yao, hivyo mtu aliyehitimu LLB anaweza kufundisha BALE kwani kwake hiyo BALE ni km topic tu ambayo tayari ameshisoma,

Acha uongo ndugu, bale wana core course kibao ambazo hakuna hata moja ambayo inaingiliana na wale wanao soma LL.B.... tafuta Udsm Prospectus na uisome kwa umakini.

au nitajie core course sita tu za wanafunzi wa BALE ambazo mwanafunzi wa LL.B UDSM kafundishwa.
 
Website ni muhimu.

Lakini kuna vitu vingi vinavyokera UDSM na huenda vyuo vyote viko hivyo:
1. Chuo hakina Library ya maana
2. Walimu hawafundishi - wengi wao wapo kwenye miradi yao. Uhuru kwenye hili umezidi mno. Mara kadhaa kuna wanafunzi wamekuja kuniomba msaada wa dissertations zao. Ni aibu aibu aibu. Karibu wote wanalalamika kuwa Supervisors wao hawaonekani.
3. Chuo hakina Library ya maana. Vitabu ni editions za miaka nenda rudi na vimepauka kama nini. hili ni suala ambalo serikali inahusika moja kwa moja.
4. Kuchoka kwa majengo na barabara (driveways) - Hili ni suala la serikali. Serikali imeendelea kujenga vyuo vipya bila kuimarisha vilivyopo.
5. etc.
Haaaaaa umesoma/ unasoma course gani hapo udsm ambayo Library haina vitu vya maana?
haaaa nilipata itumia vyema LAW COLLECTION, na kama nikipata tatizo nilikuwa nazama FoL.
 
Kweli Library ya UDSM ni kubwa kupita zote Tanzania. Lakini ipo katika hali mbaya sana kama nilivyoeleza, makala za siku nyingi sana, uchache na uchakavu

Mimi siyo Mkutubi lakini nimejifunza kitu kimoja muhimu. Vitabu vinaharibika haraka sana vikiwekwa chumba ambacho hewa ya joto kutoka nje inaingia moja kwa moja. Vitabu vinakuwa brittle na kuwa na rangi ya Old Khaki. Ni muhimu vitabu vime kwenye chumba ambacho ni air conditioned.
Siyo Tanzania tu, ni kubwa Africa Mashariki na kati, alafu kuwa specific hayo mapungufu uliyakuta kwenye collection ipi.
 
Acha kuongea upupu wewe....nmesoma udom 1st degree nkasoma udsm post graduate...nlichojifunza udsm mnakalili sana...yan ww kalili tu haijarish umeelewa au lah...tena mitihan mnarudia ..kuanzia test had Ue ..yan kama ilivyo wanachange date tu
Ukweli udsm jina tu...but hakuna lolote
nmesoma hapo nmepata gpa/grades ambazo sijawah pata maishan...
Watu muwe na logic...afu uwez dharau chuo flan wakati huna hata experience umesoma chuo kimoja tu unaamin ndo iko iko bora..
Wanafunzi wa udsm sifa nying..
Wewe ni muongo ingawa umeongea unafki.
 
Naona mkuu unajtaidi kupigia promo makelele na Nairob nibora 2 kama unavutiwa navyo ukasome uko utuache na Ud yetu.
 
Siyo Tanzania tu, ni kubwa Africa Mashariki na kati, alafu kuwa specific hayo mapungufu uliyakuta kwenye collection ipi.

Hayo mapungufu yapo Library yote. Ujengaji wa Library ya UDSM haukutia manaani kuwekwa kwa viyoyozi. Sijaingia humo ndani miaka ya karibuni tu. Kama kumebadilika basi hongera.

Naingia hofu unaposema library ya UDSM ni kubwa Afrika Mashariki na Kati. Inawezekana ni ukubwa wa majengo, lakini kma hata tukichukulia wingi wa vitabu ambavyo vipo up-to-date na majarida basi hiyo Afrika Mashariki na Kati imekwisha kabisa. Tulie tu.

Serikali ya CCM haikuwekeza kabisa kwenye kununua vitabu kwa ajili yya Library ya UDSM. Miaka michache iliyopita UDSM walikuwa wanaponea coupon za UNESCO. Sijui kama wanaendelea na hilo.

Sehemu nyingine inayoonyesha UDSM wapo hoi tabaani kitaaluma ni vitabu vya kiada(textbooks?). Zaamani tulikuwa na Bookshop pale Mlimani. Leo hii imekufa. hawa wanafunzi tunaowafundisha pale mlimani wanasoma vitabu gani?
 
Back
Top Bottom