KERO Chuo cha Mipango Mwanza hawaja-submit matokeo yangu ya Diploma One

KERO Chuo cha Mipango Mwanza hawaja-submit matokeo yangu ya Diploma One

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanfunzi wa chuo cha mipango cumpus ya mwanza nimemaliza diploma two mwaka huu nimeshindwa kuendelea na maombi ya mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kujiunga na degree sababu NACTVET hawaoni matokeo yangu ya diploma one.

Hali hiyo imefanya nimekosa AVN na mpka sasa sijui hatma yangu ya kuendelea kusoma.

Nimewafuata ofisi ya mitihani chuoni majibu wanayonipa hayaridhishi kabsa nimejaribu kumpigia mkurugenzi wa chuo mpk leo ajapokea simu.

Serikali ya wa MISO ndo haina msaada kabsa naomba wizara ya elimu inisaidie ikiona taarifa hizi me nina hitaji kusoma, mbaya zaidi imepelekea ugomvi na wazazi wanahisi sijasoma diploma nilikiwa ninawadanganya.
 
Mimi ni mmoja wa wanafunzi niliyehitimu Stashahada ya Mipango ya Maendeleo katika Chuo cha Mipango Mwanza. Baadhi yetu hadi sasa hatujapata AVN, licha ya kutokuwa na changamoto yoyote katika matokeo yetu ya masomo.

Tulipowasiliana na NACTVET, tuliambiwa kuwa chuo hakijawasilisha taarifa zetu kwao, hivyo tukaelekezwa kuwasiliana na chuo tulichosoma. Baada ya kufanya mawasiliano na Ofisi ya Usajili pamoja na Ofisi ya Mitihani, tuliahidiwa kuwa changamoto hiyo ingetatuliwa ifikapo tarehe 7 Agosti ili nasi tuweze kupata AVN, kuomba mkopo wa elimu ya juu na kuomba vyuo kwa ngazi ya Shahada.

Hata hivyo, hadi sasa bado hatujapata AVN, huku dirisha la maombi ya mkopo likiwa linakaribia kufungwa. Kutokana na hali hii, baadhi yetu tumeamua kurudi chuoni kufuatilia suala hili, jambo ambalo limetulazimu kuingia gharama za usafiri na malazi kwa kuwa tunatoka maeneo mbalimbali. Kwa sasa tumekaa Lodge kwa wiki ya pili, lakini kila tunapokwenda kufuatilia suala hili chuoni, tunaendelea kupewa majibu yasiyoeleweka na kuzungushwa.

Mkuu wa Kitengo cha Uratibu (Coordinator) pamoja na Mkuu wa Taaluma wanafahamu kuhusu changamoto hii. Hata hivyo, hali hii imefikia hatua ya sisi kuonekana kama wasumbufu kila tunapofuatilia haki yetu ya kupata AVN. Aidha, baadhi ya watumishi wamekuwa wakitujibu kwa namna isiyofaa. Katika Ofisi ya Mitihani, kwa mfano, kuna mwalimu anayeitwa Msuya ambaye mara kadhaa amekuwa akitujibu kwa majibu yasiyoridhisha pale tunapofuatilia suala hili.

Tunaomba suala hili lishughulikiwe kwa haraka ili wanafunzi walioathirika waweze kupata AVN na kuendelea na maombi ya mkopo pamoja na masomo ya Shahada bila kuathirika zaidi.
 
Mimi ni mwanfunzi wa chuo cha mipango cumpus ya mwanza nimemaliza diploma two mwaka huu nimeshindwa kuendelea na maombi ya mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kujiunga na degree sababu NACTVET hawaoni matokeo yangu ya diploma one.

Hali hiyo imefanya nimekosa AVN na mpka sasa sijui hatma yangu ya kuendelea kusoma.

Nimewafuata ofisi ya mitihani chuoni majibu wanayonipa hayaridhishi kabsa nimejaribu kumpigia mkurugenzi wa chuo mpk leo ajapokea simu.

Serikali ya wa MISO ndo haina msaada kabsa naomba wizara ya elimu inisaidie ikiona taarifa hizi me nina hitaji kusoma, mbaya zaidi imepelekea ugomvi na wazazi wanahisi sijasoma diploma nilikiwa ninawadanganya.
Naaam
 
Back
Top Bottom