Chuo cha Acharya Institute of Management & Science (Bangalore, India) ni feki

mwenyewe

Member
Apr 18, 2008
37
3
Mnamo mwaka wa masomo 2005-2006, Serikali ya Tanzania iliwapeleka wanafunzi wapatao 60 nchini India katika chuo cha Acharya Institute of management & Science Bangalore, India. kwenda kuanza masomo ya shahada ya kwanza katika fani ya Tekenolojia, Afya na Uhandishi. kutokana na kitendo hicho, chuo hiki kilijipatia umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania.

Idadi ya wanafunzi katika udhamini binafsi ilianza kuongezeka mpaka kufikia kuwavutia hata wanafunzi wa Shahada ya juu ya masomo yani Post graduate degree. Katika mwaka wa masomo 2007-2008, idadi ipatayo wanafunzi 12 walijiunga na chuo hicho kufanya MASTERS OF BUSINESS ADMINISTRATION (MBA).

Baada ya kufanya mitihani yao ya semester ya kwanza Dec. 2007 mpaka leo hii tarehe 19 April 2008 matokeo yao hayajarudi huku ni wanafunzi 90 tu kati ya 180 ndo wamepata matokeo yao. Hali hii imetokana na chuo kuwa affiliated na Visvesvaraya Technological University(VTU) ambao VTU sheria yao ni kwamba one MBA class should not exceed 90students.

Hivyo hapa mmiliki wa chuo bwana VIJAY amewatapeli wanafunzi wapatao 120 wakiwemo watanzania 12. huyu bwana lazma atakua na link na mkubwa mmoja serikalini na ubalozini NEW DELHI,maana hata alipopata tender ya kusomesha wanafunzi wa kitanzania Chuo kilikua bado under construction bila facilities zozote. WAZAZI HUKO TANZANIA KIEPUKENI CHUO HIKI, KIMEJAA UTAPELI MTUPU.
 
Mnamo mwaka wa masomo 2005-2006, Serikali ya Tanzania iliwapeleka wanafunzi wapatao 60 nchini India katika chuo cha Acharya Institute of management & Science Bangalore, India. kwenda kuanza masomo ya shahada ya kwanza katika fani ya Tekenolojia, Afya na Uhandishi. kutokana na kitendo hicho, chuo hiki kilijipatia umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania. Idadi ya wanafunzi katika udhamini binafsi ilianza kuongezeka mpaka kufikia kuwavutia hata wanafunzi wa Shahada ya juu ya masomo yani Post graduate degree. Katika mwaka wa masomo 2007-2008, idadi ipatayo wanafunzi 12 walijiunga na chuo hicho kufanya MASTERS OF BUSINESS ADMINISTRATION (MBA). baada ya kufanya mitihani yao ya semester ya kwanza Dec. 2007 mpaka leo hii tarehe 19 April 2008 matokeo yao hayajarudi huku ni wanafunzi 90 tu kati ya 180 ndo wamepata matokeo yao. Hali hii imetokana na chuo kuwa affiliated na Visvesvaraya Technological University(VTU)ambao VTU sheria yao ni kwamba one MBA class should not exceed 90students. hivyo hapa mmiliki wa chuo bwana VIJAY amewatapeli wanafunzi wapatao 120 wakiwemo watanzania 12. huyu bwana lazma atakua na link na mkubwa mmoja serikalini na ubalozini NEW DELHI,maana hata alipopata tender ya kusomesha wanafunzi wa kitanzania Chuo kilikua bado under construction bila facilities zozote. WAZAZI HUKO TANZANIA KIEPUKENI CHUO HIKI, KIMEJAA UTAPELI MTUPU.

Bw./Bibi/Bi Mwenyewe karibu sana JF. Hayo madai yako ni mazito sana kwa Serikali ya India na Serikali ya Tanzania. Unajua Serikali zinaorodha ya vyuo wanavyoruhusiwa kusoma wanafunzi wa kigeni (from my experience). Hivyo hoja yako inaattack moja kwa moja Serikali hizi mbili.

Kuhusu kutoa wito kwa Watanzania kukiepuka Chuo hicho sawa, lakini wataamini vipi hayo unayoyasema? Vipi kama hoja zako zinatokana na chuki yako dhidi ya hicho Chuo? Maana yangu hapa ni chanzo cha hiyo taarifa.

Otherwise toa maelezo yatakayo thibitisha hayo unayoyasema ikiwa ni pamoja na jitihada zilizofanyika.

Si kubaliani moja kwa moja kwamba kusajiri Watanzania katika chuo hicho ni deal la Ubalozi wetu. Je ubalozi unataarifa hiyo? kama unataarifa umerespond vipi?

suala la matokeo ni utaratibu wa Chuo, Vyuo vingine hutoa matokeo baada ya mwaka (baada ya mitihani ya semester ya pili). Hainiingii akilini kwamba wanafunzi 90 tu kati ya 180 ndo wamepata matokeo yao bila kuwa na sababu zingine.

Haiwezekani wakatoa matoke ya wanafunzi 90 (kuacha 90 wengine) eti sheria/utaratibu unataka kuwe na wanafunzi 90 tu darasani. Sasa ni vipi mgao huo ulifanyika?

Kwa ujumla madai yako hayaniingii akilini.
 
nashukuru sana bwana nziku kwa kuchukua muda wako na kujaribu kudadavua hoja hii. yep Karibu India, si ajabu kwa wenye vyuo kusajiri wanafunzi kuliko idadi ya inayotakiwa na central university. hii inawezekana kutokana na kua na mianya mingi ya rushwa katika vyuo hivyo, hivyo kwa kesi ya Acharya college kilichotokea ni kwa mwenye chuo kumtumia mtu wake mule VTU katika kusajili na kupata namba za mitihani. bila kutegemea, uongozi wa VTU ulibadilishwa ghafla na uongozi mpya uliongia ulifanya re-view ya usajili wote wa wanafunzi.hapo ndipo ufisadi huo wa Acharya College ulipo anikwa uchi hadharani. wanafunzi wa kitanzania wamefanya juhudi za kuwasiliana na ubalozi uliopo mjini Dehli, lakini kutokana na strong bond kati ya Ubalozi na mmiliki wa chuo hicho. wamekua wakipigwa dana dana wakiambiwa wasubili huku mitihani ya second semester ikikaribia.SWALA HILI LIMELETA VURUGU NA MKANGANYIKO CHUONI ACHARYA SI KWA "FOREIGN STUDENTS" TU! WAKIWAMO WATANZANIA 12. BALI HATA KWA WANAFUNZI WA KIHINDI. Kesi imeshafunguliwa kumshtaki mmiliki wa chuo kwa kuwapotezea muda na kudai fidia kwa ajili ya Damage iliyowakuta wanafunzi.
 
Hii mbona kali kamanda,mbona sasa itakuwa balaa sana.Ninavyojua kuna lundo la "vichwa" nikiwa na maana vile vilivyopata Div 1 za pwointi 3 mpaka 5 viko chuo hicho sasa kama madai ndio haya basi mzozo mkubwa hapo.

Wewe upo chuo hicho?
 
Naam, mimi ni mmoja wa wanafunzi tuliohisi kubahatika kupata nafasi hii kusoma hapa Acharya College. pamoja na kuwasili kwa mtendeja wa ubalozi wa Tanzania nchini India anayeshughulika na maswala wanafunzi NDUGU AMOS MWAMANENGE, bado mambo si simba wala yanga. we are just playing a waiting game at the moment.
 
Back
Top Bottom