peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,254
- 23,908
Waliokuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza wameshinda kesi dhidi ya Bodi ya wadhamini ya chuo hicho baada ya kupigania haki kwa miaka 12 na Mahakama kuamuru walipwe fidia ya Sh30 milioni.
Hukumu hiyo ilitolewa Februari 24, 2023 na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania na hukumu yake kupatikana katika mtandao wa Mahakama Kuu ya Tanzania (TanzLii) jana.
Wanafunzi hao ni Robert Mhando aliyekuwa anasomea shahada ya Mahusiano ya Umma na Masoko na Tereza Manumbu aliyekuwa anasomea Shahada ya Sosholojia.
Mwaka 2011/12, walisimamishwa na mjibu maombi (St Augustine University) kuendelea na masomo na kufanya mitihani kwa tuhuma za kutolipa ada.
Wanafunzi hao walikanusha tuhuma hizo na walishikilia msimamo kuwa walikuwa wamelipa ada stahili na kupewa stakabadhi na mhasibu wa chuo hicho na wakashinikiza waruhusiwe kuendelea na masomo yao bila mafanikio.
Wakichukizwa na jambo hilo, walifungua maombi Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza wakiomba itamke pamoja na amri zingine, kuwa wao ni wanafunzi halali wa chuo hicho, wanapaswa kutambuliwa na kupewa haki zote kama wanafunzi.
Pia, waliiomba Mahakama iwaamuru wajibu maombi hao kuwaandalia mitihani maalumu (special examinations) kwa mwaka huo wa masomo, kuwalipa fidia maalumu ya Sh2.1 milioni na fidia ya jumla inayofikia Sh30 milioni.
Mahakama iliona wanafunzi hao walisitishiwa masomo bila uhalali na kuamuru iwalipe fidia ya jumla ya Sh50 milioni badala ya Sh30 milioni, lakini mjibu maombi hakuridhika akakata rufaa Mahakama Kuu iliyotengua hukumu hiyo.
Hata hivyo, hawakukata tamaa ya kupigania haki yao kwa kuwa walikata rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania ambayo imethibitisha kuwa walikuwa wamelipa ada stahiki na mjibu maombi aliwapa risiti halali iliyotolewa na chuo.
Jopo la majaji watatu likiongozwa na Jaji Augustine Mwarija, Zephrine Galeba na Pantrine Kente waliridhika kuwa wanafunzi hao walikuwa wamelipa ada hiyo ya masomo kupitia kwa mhasibu wa chuo hicho.
Katika majibu yao, bodi hiyo ya wadhamini ilishikilia msimamo wa kumtupia lawama mhasibu wa idara ya mapato kwa madai ya kupokea ada kutoka kwa wanafunzi na kuzitumia kwa matumizi yake binafsi.
Majaji hao walisema kisheria na kanuni, mwajiri anaweza kuwajibishwa kwa matendo ya mfanyakazi wake wakati akitekeleza majukumu yake, hivyo na suala la wanafunzi hao linaangukia katika sheria hiyo.