Chungu kipya divai ya zamani

Chungu kipya divai ya zamani

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari za jioni mabibi na mabwana, natumai mko poa licha ya vuguvugu la uchaguzi.

Kasie amekuwa na shughuli mob kipindi hiki japo sio za uchaguzi, mie kama kawaida yangu mwezi wa matumizi unakuja sasa nikawa nakamilisha mahesabu ili zitimie mwzi wa kumi na mbili nijirushe likizo kwa afya yangu safari hii ntasafiri ndani ya bara la Africa inshallah mola akijaalia uhai panapo afya.

Kuna dada wadada flani hivi niko nao group flan hivi huwa tunachat na tulifahamiana humu humu JF. Sasa katika moja ya chat siku mooja mmoja wa wadada hao akaanzisha habari akisema anachukizwa na tabia ya baadhi ya wanaume wa JF hasa MMU kutumia ID mpya kumchora mdada huyo, kiufupi dada alilalamika kuwa multiple ID haikatai maana watu wanaruhusiwa na wanafungua kila leo mbaya ni kuitumia vibaya.

Akaanza kuelezea alikutana na mkaka humu JF wakawasiliana hadi nje ya JF mara akaanza kuona kuna ID mpya ambayo imejiunga hivi punde ikianza kum PM na maelezo na jinsi mkaka anavotongoza ikaonesha kuwa mkaka anaonekana anamfahamu mdada. Mdada akafanya INTERNAL AUDIT yake akagundua Yule mkaka mwenye ID mpya ndo Yule Yule walikuwa wakiwasiliana zamani hata mawasiliano yakatoka nje ya JF. Akaboreka na kukata mawasiliano bila kumwambia Yule kaka ndo akaja kutuambia kwenye group (ofcourse hakumtaja ni nani). Basi tukalijadili pale likaishie pale.

Huko mtaani nako kama kawaida ya Kasie na wachumba kibao, siku hiyo nikawa na mmoja ya wachumba niliokutana nao humu JF na hapo nikajikuta katika maongezi namuelezea malalamiko ya Yule dada bila kumtaja ID yake (HESHIMA KWANZA SI VIZURI KUTAJANA ID) hivo tuliongelea mada bila kutaja wahusika, nikamwaga malalamiko kuwa mule JF wakaka wanafanya tabia mbaya ambayo inawafanya waonekane hawajiamini kwa wadada au ndo anakuwa kamchoka mdada anatafuta sababu ya kummwaga pale mdada anapoingia anga za ku flirt na Yule Yule kwenye ID mpya bila kujua au lengo ni kwenda kumtangaza kwa wenzie kuwa huyu ni mlegezo unateremka muda wowote.

Yule mkaka akafunguka kwenye maongezi (MIND U TULIKUWA KWENYE VITI VIREFU LOOH) akasema baadhi ya wadada wa JF wanajirahisi sana na hawataniwi na wengi wanaliwa kwasababu wakaka huwa wana PM kiutani au kujaribu huyu dada atajibu vipi au atamchukuliaje. Matokeo yake wadada huwa wanachukua kuwa ni dili na wanajitosa mazima na kuanza mawasiliano ya karibu hatimaye kuanza mahusiano, na akaniambia tabia moja ya wanaume ni kutokukataa chakula hata kama wameshiba au hatab kama hawana njaa.

Nikabaki nasikiliza akasema hapo hujikuta wanawatafuna waschana wengi bila kuwa na lengo lolote la kuwa na mahusiano nao, na akikuta si mschana au mdada aliyemtarajia basi huanza vitimbwi mwingie hupotea na hata mdada akituma PM hajibiwi, au mwingine ndo huyo humuanzishia ID mpya na kuanza kumtongoza upya ili amkeep busy aache kumtafuta kwa ile ID ya zamani, na maschan akijikanyaga tuu basi humwaga kwa kumwambia wewe mwingi unakubali kila PM ilikuwa nitangaze ndoa ila nimebadili mawazo kumbe hana lolote mharibifu tuu.

Huyo mkaka akaniambia tena, wadada wa JF pia na wao wanatumia ID mpya kujitongozesha kwa mkaka hasa wenye hela (hapa aliniambia hajui wadad wanajuaje wanaume wenye hela JF) ila wakishajilengesha huomba hela na wakishatumiwa wanapotea na kuanzisha ID nyingine na kuwalenga tena hivo akasema hiyo pia imefanya wakaka wa JF kuwachezea waschana wa JF.

Nikasema haya kwakuwa nimeyasikia pande zote mbili na wote wapo humu wacha niyaweke najua kila mmoja atajibu kwa wakati wake.Haya mmesikia kutoka pande zote mbili, kazi kwenu mjirekebishe muoane sio kila siku mkutane guest na kwenye magari mabovu. Wakaka na wadada wa JF muache tabia ya CHUNGU KIPYA DIVAI YA ZAMANI yaani ID MPYA MTU YULEYULE WA SIKU MINGI, ikibidi sio kwa kuleta sononeko na maafa. Nimeleta ujumbe kama nilivoagizwa.Bora Kasie mie nimejizeekea siku hizi nimepunguza kwenda club umri umesonga na choices au hobby zinaenda zinabadilika kila siku, sijui ndo menopause imeanza mmh!

Haya niwatakie Week end njema na usiku mwema.

Bibi ajuza Kasie.
 
Tatizo la kampeni za ukawa hamna malori ya kuturudisha home na hawagawi ubwabwa maharagwe. Kama Una kausafiri naomba lift boss, mkutano ndio unaisha
King'asti huku Ni mabadiliko malori mnadani,anyway njoo twende mama
 
Last edited by a moderator:
itabidi tuanze kuzikagua hizi title za junior na member... senior expert member sina wasiwasi nao
 
Jiwe kundini, atakaesema 'aaaiiiiii'....

BTW... nice message kwa walaji na waliwaji. Na hii itasaidia the 'informed hunters' wabadili mikakati ya uwindaji.
 
Uzee nao raha sana...naona vijana wanakimbizana mmu...!!
 
Kumbe kuna kutafunana humu ndani? I thot ths is just a social media!
 
Aiseeeeh.... Kumbe kuna mashughuri hivyo humu ndani.
 
Back
Top Bottom