Chunga sana ulimi wako mwanandoa

Chunga sana ulimi wako mwanandoa

Hahah nilikumbuka hilo jina + kiswahili chako fulani hivi nikajua huyu ni USA baby tu. Pole kwa ban

Hahaaa eti nina Kiswahili changu fulani hivi.....kwani Kiswahili changu kikoje, kiko tofauti? Ni cha 'Kizungu'?😉
 
Hahaaa eti nina Kiswahili changu fulani hivi.....kwani Kiswahili changu kikoje, kiko tofauti? Ni cha 'Kizungu'?😉
Sijui ndo kiswahili cha ndani ndani teh , "ghaidhi, mintarafu, mlinganyo", sio maneno ambayo wengi wetu tunayatumia
 
Kweli kabisa mkuu..hiyo nilishuhudia mwenyewe wala si kuhadithiwa,jamaa alimwambia mkewe nakupata talaka moja ukajirekebishe kwenu..mke akamwambia nipe tatu zote,jamaa akampa kweli ,baada ya siku mbili mke akarudi analia na msamaha juu kuwa zilikuwa hasira,jamaa akamwambia sheria akaolewe na mtu mwingine akishaachika ndiyo jamaa amrudie,ndoa ikaisha kama utani tu..
 
Maneno hayo machafu ,alafu akipika unakula,anaweka maji ya kuoga unaoga ,ana lala kitandani unampandia,anazaa watoto unaita jina lako aisee ndio mana mwanamke akiamua kufanya roho mbaya inakua roho mbaya kweli
Kama kuna jambo wanaume wanakosea ni kudhani wanawake ni wajinga....
 
Inawezekana ni kweli lakini sidhani kama ni kweli mara zote.

Wakati mwingine watu hutamka maneno ambayo hata hawamaanishi [ambayo yanaweza kupokelewa visivyo].

Mfano, hujawahi kuona watu waliokasirishana na kila mmoja akimwambia mwenzake 'ntakuua wewe'?

Kweli unadhani watu kama hao huwa wanawaziana kuuana ila huwa wanashindwa kuambiana hadi wapatapo fursa ya kupishana Kiswahili?

Kwa kawaida, mtu akishapandwa na ghaidhi akili huwekwa kando na hisia hushika hatamu.

Sasa katika hali kama hiyo, watu hujikuta wakiongea maneno mengi tu ambayo hata hawamaanishi lakini zipo nyakati ambazo hutokwa na maneno ambayo wanamaanisha.

Ugumu upo kwenye kutenganisha yepi ni yepi na ndo hapo jinsi ya yanavyopokelewa na walengwa kunaingia kwenye mlinganyo.

Kwa mintarafu hiyo basi, ndo umuhimu wa kuchunga kauli unapokuja maana huwezi jua mlengwa wako atapokeaje hicho ulichokilenga kwake.

Zipo kauli ambazo huweza kujeruhi na kuacha kovu la muda mrefu kwenye hisia za mtu. Na mtu akishakuwa na kovu la hisia ni vigumu sana kurudia hali iliyokuwepo kabla ya.
Kama wewe nimekuweka tu kiporo na yale maneno yako
 
Kama kuna jambo wanaume wanakosea ni kudhani wanawake ni wajinga....

Lakini mbona hata wanawake nao huwa wanakosea sana kudhani kwamba wana uwezo mkubwa wa kuwasoma wanaume ilhali nyakati nyingine sivyo kabisa.

Mwanamke unaweza ukamlengesha kudhani kwamba anakujua vizuri kwa kumpa ishara flani flani ili afikirie hivyo, na yeye kwenye akili yake akadhani kwamba hisia zake huwa ni sahihi mara nyingi kama si zote, wakati ukweli wa mambo ni wewe mwanaume ndiye uliyempa kwa makusudi viashiria vyote vya yeye kudhani hivyo.

Sasa akishadhani na kupatia anajiona mjanja...mwerevu...na kadhalika. Hajui kwamba wewe ulimrahisishia tu kazi na kama ungetaka ungeweza kuifanya iwe ngumu vilevile.

Sijui hata kama umenielewa.....
 
Labda nitakuelewa kwanzia kesho msukuma wewe
 
Back
Top Bottom