Emoj
JF-Expert Member
- Oct 9, 2015
- 839
- 1,304
"Naregret sana kukuoa, kwanza sikuwahi kukupenda nilikosea tu njia, mi nilikuwa nampenda yule dada mfanyakazi mwenzangu ila sijui hata nilitokana wapi na wewe usie na mbele wala nyuma hadi nikaachana na yule dada." sijui uliniloga?" haya ni maneno alikuwa anaambiwa jirani yangu na mume wake.
Ni kweli Ndoa zina changamoto nyingi sana tu ila ukiwa kama mwanandoa panapotokea kupishana na mume/mke wako chunga sana ulimi wako maana maneno mabaya utayosema yana nguvu sana.Yanaweza punguza au kuondoa kabisa upendo kwa mwenzako.
Ndio una hasira,mwenzio kakuudhi sana ila yakupasa uchunge maneno usemayo,ni afadhali mara mia kama una hasira usiongee kabisa.maneno kama haya "najuta kuwa na wewe "au "sikuwahi kukupenda" ni maneno ambayo yana uzito sana kiasi cha kuweza kupunguza upendo au kuondoa kabisa upendo kwa anayeambiwa.
Mwanandoa chunga sana pale unapokuwa na hasira maana hasira zinaweza kuja kukuponza.
Tunalalamika sana ndoa ni mbaya ila ni maneno mabaya tunayoambiana tukiwa ndani ya ndoa ndo yanayomaliza ndoa zetu. usitegemee eti umwambie mwenzio sikuwahi kukupenda halafu baadaye ukaja kusema zilikuwa hasira kama atakuja kuwa sawa,hata ukiomba msamaha hili neno bado litamsumbua sana ni neema tu ya Mungu ndo itakuja kumuondoa na kufanya asahau na kuwa normal.
Jamani mwanandoa pima maneno unayomwambia mwenzio wakati ukiwa na hasira.Usiropokeropoke tu.