donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,258
- 22,140
Wakuu nipo hapa DTB harbour view posta ndio tunasubiri kuingia mmoja mmoja kwenye interview (3rd interview). Kwa kweli matumaini ni madogo sana kwani wapo jamaa ninao wafahamu ambao walifanya zote tatu still wakachinjiwa baharini. Ila naomba Mungu mambo yaende sawa tu tuone tunafanya nini. Daah, kuna jamaa kaja na suti hapa yaan utadhani yeye ndio meneja uajiri na mkwara wake kwamba haelewi kiswahili vizuri. Pia kuna mhindi mmoja amevaa silver kibao, wahindi wa humu ofisini kila wakipita wanampa hi nyingi aisee sijui mtoto wa mdosi mwenzao? Huyu wanaweza wakampa kiundugu. Ngoja mimi mjukuu wa Mwangungumile Mwampuza nisubiri kuitwa. Salaam!