CHUKIi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHUKIi!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, May 16, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  GOSH!!

  Hivi jamani unaweza ukamchukia mtu mpaka ukimwona au ukimsikia hata hamu ya kula inakuisha???

  Kuna mtu mmoja maishani mwangu nampenda kiasi kwamba niko tayari hata kufa kwaajili yake...sasa haya mapenzi niliyonayo kwa huyu mtu ni sawa na chuki niliyonayo kwa mtu mwingine. Yani huyu amewahi kunifanyia vimbwanga vingi sana na pamoja na chuki niliyo nayo juu yake bado sijawahi kumtakia mabaya...infact hua namsaidia sana akiwa na tatizo.Ila kila kizuri nnachomfanyia hua kinaniletea mimi mabaya kwa namna moja ama nyingine....mpaka nafikiria labda naadhibiwa kwa kumsaidia.Sasa nimefikia mahali hata nikimwangalia nahisi moyo unaniuma...nimepata mawazo mabaya kweli juu yake jana.

  Sasa hivi nataka niweke umbali kati yangu na yeye kwa namna yoyote ile....hata ikibidi nihame nilipo niko tayari.Nadhani nahitaji maombi.....embu niombeeni wandugu!!

  Mchana mwema!
   
 2. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kabisa hata mimi yamewahi kunikuta kama yako.

  Pole nitakuweka kwenye maombi njia ya pekee ni kukaa mbali naye ndo utapata unafuu.

  Pole sana kwa mara ya pili
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Pole!
  It happens!
  Lakini usihame kisa unamchukia!
  Kuna siku atakufuata, aidha ataguswa na jambo fulani juu yako, ambapo mahusiano yako kwake yatabadilika!

  Mimi nilisoma vitabu vya kizamani sana vya hadithi, ambapo Kuna kisa cha cha Sultani na Kichaa!
  Kichaa huyu alikuwa kila asubuhi alfajiri anaenda mlangoni kwa Sultani na kutupa matakataka!
  Alifanya hivyo kwa muda mrefu, na juhudi za kumkemea na kumkataza zilishindikana!
  Lakini ikatokea kuwa kichaa huyo akafariki ghafla!
  Sultani na familia yake waliposikia kifo cha kichaa huyo walilia sana na kuhuzunika, maana at least kila asubuhi alikuwa akipita hapo kwao, japokuwa alikuwa akimwaga rundo la takataka!

  Hivyo Lizzy, japo mtu huyo ni msumbufu, ukihama kuna kitu utakikosa toka kwake...uTASAHAU KUSAMEHE!
  Lakini pia utapoteza baraka zako za KUTOA maana hutakuwa na wa kumsaidia tena!

  Right?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Dah.. Lizzy this is extreme aisee

  Wakati tunasoma somo moja hivi tulipewa case ya watu wenye extreme behaviours... I am sure huko haupo; ila inawezekana kabisa yaliyokukuta. Cha maana ni kuomba Mungu iwe temporary kwani hakuna haja ya kupand mbegu ya chuki, ni dhambi kubwa tu

  Pia chuki ikizidi inakuletea hadi depression na matatizo mengine... there are three things you can do

  1. Mwambie kabisa na aelewe unavyojisikia - this releases tension
  2. tatufa counselling ya nguvu (spiritual au clinical)
  3. Mdharau na uendelee na maisha yako - waswahili wanasema mjinga kwa kwenda, kwa kurudia anajua baya na zuri...

  the third option is very simple to implement and you will find yourself having a laughter about all situation.... :A S 103:
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Pole saana Partner.... From maelezo ulotoa inaonesha wazi kua huyo mtu ni wakaribu yako kama si ndugu na pamoja na madhaifu yake uko radhi kupotezea but haishi kukukwaza. Mi naona ni bora umuweke mbali nawewe na si lazima kujihusisha na mambo yake wakati at the end of the day yanakuletea matatizo (kama mwenyewe ulivyo admit).. Sielewi kwa undani nature ya matatizo yenu na mahala mnapoishi but ni hatari sana.. saizi inaweza onekana rahisi shida ni pale at the end inaleta/tokea tukio baya... Nashindwa kuongea zaidi for there are so many unanswered questions....
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Pole dear
  hakuna sababu ya kuhama
  kwa vile hukuwahi kumtakia mabaya ni rahisi kuondoa
  chuki uliyonayo kwa kuongea nae atambue ukweli ulionao juu yake
  chuki ikizidi inaleta uadui

   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Acha tu, hio kitu ipo nafikiri jambo la msingi ni kuomba zaidi
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  May 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Pole sana Lizzy! Haya mambo huwa yanatokea, cha muhimu ni kuendelea kuwa na uvumilivu!
  Usikimbue tatizo, tafuta suluhisho.
   
 9. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #9
  May 16, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  duu pole lizzy
  ni ndugu au mpz iv?
  woteva the case...MPOTEZEEE ...ukishampotezea na akigundua hauchoshw waka aujishugulish juu ya HILA zake m sure atajirud na apo ndo itakuwa mwsho wa mech

  ukiendelea kumwonyesha waumia juu ya mambo yake ndo unampa nguvu ya kuendelea kufanya maajabu

  mwonyeshe unamdharau na wala auchomwi tena na mambo yake

  pole
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Kwa kuwa sijwahi KUMPENDA mtu yeyote, then, naamini siwezi KUMCHUKIA mtu yeyote!
   
 11. N

  Nancy70 Member

  #11
  May 16, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana Lizzy, ila jitahidi kuondoa hasira na kujenga chuki juu yake. Wazungu wanasema..anger does more harm to the vessels in which it is stored than into vessels it is poured. At the end of the day you are the one who suffered while mwenzio anakula raha tu. Kuhama haisaidii just pray to God hakuna linaloshindikana mpendwa.
   
 12. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #12
  May 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mmh pole sana mamy,yap kama binadam ambao ni dhaifu kweli kuna mijitu unatamani kuotoa duniani thats y wanasema "SOME PIPO ARE ONLY ALIVE BECAUSE ITS ILLEGAL TO KILL THEM"
  or in all hutakiwi kumchukia binadam mwenzio kiivyo"hasira hukaa mioyoni mwa mpumbavu,bibo"mpotezee tu u beta keep mbali nae ili usikwazike zaidi lkn hapo kwenye kumpenda mtu mpaka unaweza kufa kwa jili yake duh!mm hapana jamani khaaaa,napenda ndio lkn hapo duh!sugar is sweety but when its too much its becames bitter.
   
 13. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #13
  May 16, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mm yaleyale...nimesamehe lakini sitasahau!!
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  May 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Dawa ya tatizo, sio kulikimbia bali kulikabili.
  Wewe ni mtaalau wa kutoa ushauri wa matatizo mbalimbali hapa JF
  Yapaswa uwe jasiri.

  Hapo kwenye red wengi wetu tunapashindwaga kwa hofu ya kupoteza uhusiano au kukosana.
  Upendo si kuambiana mazuri pekee, bali kuambiana na namna ya kuepuka yaliyo mabaya
  Mshirikishe mwenzako ktk matatizo yanayokukabili, mweleze jinsi yanavyokugusa, msisitizie msaada wake kwako.
  Binadamu tunaishi kwa kusaidiana, na si kukimbiana.
  Naamini kwa njia hii utaweza kuondokana na sehemu kubwa ya chuki yako kwake, na hatimaye ukazidisha upendo maradufu
   
 15. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ai nimeshangaa hii comment
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante sana mpendwa....

  PJ asante kwa maneno mazuri ila kuna watyu ni bora kua mbali nao maana ni sawa na sumu...popote walipo inasambaa!!!
  Kuhusu kusaidia si wapo wengine bwana....

  Hahaha MTM i'm not that extreme sema tu naona hii kama ni zaidi ya nilivyozea!!
  Ngoja nifikirie hiyo ya kumwambia maana siku zote hua nikisema kinachonisumbua napata unafuu...hata hapa tu nimeshapunguza mzigo kidogo!!!Alafu nikimaliza nampotezea!!

  Thanksss!!
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante partner ....mwenyewe najua sio fresh kabisa ndio maana nataka kuwe na umbali kati yetu!!

  Asante dear...na kweli huo uadui ndo siutaki maana ukishajenga uadui na mtu ndio basi tena!!Ngoja nijisogeze wakati bado mapema!

  Shea basi maexpiriens we desh desh...lasivyo sikuletee zawadi!
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Bora ume realise hilo before its too late.... Muombe na Mungu akusimamie na kukuzidishia uvumilivu na busara katika maamuzi yamuhusuyo...
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo nilipobold ni kweli tupu...kam aingekua kinyume na hapa nisingehangaika!!

  Hahhaha...angalau nimecheka kidogo....thanks dear!!Yani sijui watu wengine wakoje!!!
  Hapo kwenye kupenda we acha tu...long story!!!
  Yani unanipa live sio??Nwy sijawahi kujisikia nimepotea kama sasa hivi...siku zote hua naweza kusimama mwenyewe ila kwa mara ya kwanza naona kama nimezidiwa!!!
  Mhhh upendo maradufu???I doubt it!!Asante lakini....ngoja nitafute jinsi ya kumjulisha!!
   
 20. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Sipendi wa sichukii mtu - As simple as that!
   
Loading...