Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,041
- 1,294
Chuki ni mzigo usioonekana unaokula nafsi kimya kimya
Kuna uchungu wa aina fulani huwezi kuupiga picha. Uchungu wa mtu anayebeba chuki moyoni...
Chuki haina kelele, lakini ina sumu...
Ni moto unaowaka ndani kimya kimya, ukiunguza kila chembe ya amani uliyonayo.
Ukimchukia mtu si yeye anayeteseka ni wewe...
Yeye anaendelea na maisha yake, anacheka, anafurahi, hata hajui unavyohisi..
Lakini wewe... kila ukimuona, moyo unaenda kasi Ukisikia jina lake, hasira inakujaa.
Ukiona mafanikio yake, unajisikia uchungu na mpweke.
Chuki haimbadilishi yule unayemchukia. Inakubadilisha wewe. Inakufanya ushindwe kupumua kwa amani.
Inakufanya ushindwe kusamehe. Inakufunga kwenye gereza la hisia zako mwenyewe.
Ni kama kunywa sumu na kutarajia mtu mwingine afe.
Mioyo yetu haiwezi kuhifadhi chuki kwa muda mrefu bila kupasuka.
Kwa hiyo, unapobeba chuki ni nafsi yako unaiadhibu, naua furaha yako, unasumbua akili yako, unachelewesha safari yako.
Wengine wanaweza wasistahili msamaha wako. Wewe unastahili amani yako.
Na mara nyingine, njia pekee ya kuipata… ni kuacha kubeba chuki. isiyo na maana
Abuuabdillah ✍️
0744883353