Chuki na UDSM hakuna aliyekutuma Ufeli

Kipo Chuo Kikuu kimoja tu Tz.Na kinafahamika .You just name it with full pomposity...Udsm.
 
mnasoma nini na ajira hakuna
UDSM chenyewe wanafunzi wanasoma wanahitimu hata kuandika insha hawajui.

Hicho ndicho chuo kinagombaniwa.

Kweli ukiwa jangwani hata matope utaita maji safi.

Nilivyokuwa nasoma A Levels enzi zangu, nilikuwa napenda sana Particle/ theoretical Physics.

Nikawa naenda UDSM kuangalia library yao, imechooka, vitabu vya tangu ukoloni.

Nikaenda American Library Peugeot House nikakuta vitabu vya mwaka mmoja uliopita vyenye latest updates vipo.

Nikaona tunacheza.
 
UDSM kutupatia Kikwete na Magufuli tu tayari ni doa la kufanya mtu asitake kusoma hapo.

Kuna siku nilikuwa naangalia website yao,nilishindwa kuamua nilie au nicheke.
Heheheh,,,umenifanya nicheke na mie,,,ndio vile vyuo ukipiga simu haipokelewi wala email haijibiwii
 
Kitu cha kujifunza ndugu yangu:
Elimu na Akili siyo kusoma Chuo kama UDSM au MZUMBE..Unaweza kusoma hapo na kupata PhD lakini kwenye soko la kimataifa hata usionekane na wala usichangie lolote kwenye ulimwengu wa taaluma au kwenye jamii. Au hata kusoma Ulaya au Marekani lakini bado ukaishia kuwa zwazwa tu.

Leo hii hao wasomi unaotaka kuwasifia wameshindwa kabisa kutatua matatizo ya nchi hii na wengine hata kujikwamua kimaisha wameshindwa, lakini unakuta mfanyabishara wa kikinga pale Kariakoo aliyeishia form four au darasa la saba anasaidia jamii kwenye kodi na kutoa ajira.

Vyeti vinakudanganya sana wewe.
Badilika, UDSM ni chuo cha kawaida sana kwa sasa.
 
Uwikariri mpendwa, ukitaka kilimo huwezi kusoma udsm z
Accounts huwezi kusoma udsm sasa chuo gani kinatoa course nyingi kinaacha kozi muhimu ya fedha. Siku hizi Nasikia B.com wameboresha walau unaweza kukuta course inayofanana na uhasibu.
 
Sio kila mwanafunz ana ndoto za kusoma udsm; kwan kuna coz kibao za maana hazpo kwenye hicho chuo. .na kusema wanaosoma udsm ni vipanga ni uongo pia. .
Kipimo cha vipanga kwa nchi ya Tz ni matokeo ya kidato cha NNE na Sita katika taaluma.

Njoo Udsm uone kama utaona divisheni za kuunga unga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…