Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,789
- 2,701
Habari Wakubwa.
Leo nikiwa katika biashara yangu walikuja vijana wawili. Vijana hao walionekana kukwaruzana kila mmoja akijaribu kumshinda mwenzake kukitukana chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Nikiwa kama Mhitimu kutoka chuo hicho. Nilivuta masikio yangu zaidi na umakini wote kutaka kujua nini sababu ya mvutano ule mkubwa.
Kwa nasibu vijana wale walikuja kwenye biashara yangu wakiwa bado wanararuana vikali kama wapo katika finali ya kombe la dunia.
Sauti yangu ya kuwakaribisha ndio iliweka nukta katika mabishano yao na kuwafanya wameze mafumba kadhaa ya mate jasho shingoni likiteremka kutokana na jua la Dar.
Niliwahudumia. Kisha nikawauliza kuhusu walichokuwa wakikitukana.
Ndio wakanipa filamu zima jinsi walivyo-apply Udsm na kutemwa kama kohozi. Walienda mbali zaidi nakusema kwa maksi walizopata walikuwa na haki za moja kwa moja za kuchaguliwa Udsm. Hapo ikabidi niulize ufaulu wao. Ndipo mmoja kwa kujitutumua akafungua mdomo wake na kusema ana divisheni two ya 11 mwenzake akadakia ana ya 10.
Nikawapa pole tuu na kuwaambia walifaulu tuu vizuri hivyo wa-appy vyuo vingine.
Mytake; jamani ninyi watoto mlioshuleni someni kama mnataka mambo makubwa. Sio unamaliza shule na kadivisheni two kako alafu unataka uchaguliwe chuo kikubwa cha vipanga.
Hakuna aliyekutuma ufeli. Kama unataka kusoma Udsm sharti upige msuli upate angalau kadivisheni one.
Kila mtu apambane na hali yake.
Udsm hoyeeeeee!