Chuki na husda dhidi ya wanaDiaspora

Chuki na husda dhidi ya wanaDiaspora

Sheria hiyo imo ndani ya Katiba ya zamani ambayo sote tunakubali kuwa imepitwa na wakati. Tatizo la Katiba hiyo iliundwa kukidhi wakati fulani na mambo yameshabadilika.
Ndio maana nikakuuliza wewe unaona tukiwapa uraia ndugu zetu hao tutaathirika na nini au wataleta matatizo gani?

Kwangu sioni tatizo
 
Kwa hivyo wana haki ya kulalamika iwapo hakuna tatizo na wananyanyapaliwa. Tubadilishe sheria imepitwa na wakati.

Kulalamika si suluhu wala kulaumu na kushutumu si jawabu..

Hoja na kuchukua hatua ndio jawabu..
Kama watu wanaanzisha mijadala kwa umoja..kupambana kwa nguvu na umoja pia kuacha tabia za kukwazana hapo itakuwa na mashiko..

Ila kubwa kuliko yote ni umoja...
 
Mimi nawashangaa sana watanzania mlioko nje... kutwa mnashindana kufungua mashina ya CCM utafikiri ndiyo inawapa kula huko,,, yakija mambo ya msingi kama haya ndiyo wa kwanza kulalamika!!...

Serikali ya MaCCM endeleen kuwabania hawa wanafiki wanje maana wamezidi kujipendekeza

I see the scourge of generalization manifests its exacerbation, whilst the plague of reductivist ignominy rear its ugly head vociferously.
 
Kulalamika si suluhu wala kulaumu na kushutumu si jawabu..

Hoja na kuchukua hatua ndio jawabu..
Kama watu wanaanzisha mijadala kwa umoja..kupambana kwa nguvu na umoja pia kuacha tabia za kukwazana hapo itakuwa na mashiko..

Ila kubwa kuliko yote ni umoja...

Mkuu uzoefu tulionao nchi hii bora ulalamike ili wenye nguvu wajione wanakufanyia ihsani kuondowa malalamiko kuliko kuleta mjadala! Huoni la Katiba mijadala na fedha zote bado wakubwa wanasema 'no' na jawabu itakuwa hivyo!
 
Mkuu kuna tofauti kati ya malalamiko na madai hilo utambue..

Hamuitaji kulalamika maana malalamiko wakati mwingine hupuuzwa na hukosa nguvu..

Madai ndo huwa na nguvu na huchukua hatamu..

Hebu chukua mfano huu..

Kumlalamikia aliyekudhulumu na kumdai aliyekudhulumu kupi bora?

Hamuhitaji kulalamika maana mtaitwa walalamishi..

Wananchi hawakulalamika kuwa wanataka katiba mpya bali walidai katiba mpya...

Ni wakati wa kuungana kudai haki ya uraia pacha..
 
sahihisho kidogo: Mlalamikaji sio mlalamishi bali anaemfanya mwenziwe alalamike ndio mlalamishi!

Hilo la kudai nimeshkwambia kuwa kwenye Taifa hili halikufikishi pahala lakini unatakiwa kulalamiko yaani upatikane kero ndio patafutwe ufumbuzi.
 
Watanzania ni porojo sana popote pale walipo, hawaishi kutafuta visingizio. Watu wenye nia ya kuwekeza nchini kwao hawaitaji uraia pacha kufanya hivyo. Tumewaona wapopo (wanaijeria) walioko kwenye nchi zinazokataa uraia pacha kama Norway, lakini wanaukana uraia wao na bado wanawekeza nyumbani. Acheni porojo, mjitume...ongezeni ujuzi mpate kazi za maana au muanzishe miradi yenu huko ughaibuni na mnaweza kuja huku nyumbani hata kama foreign investors (tena wengi hamjui tu, Tanzania inawajali foreign investors kuliko wazawa). Tatizo lenu wengi mmejikita kwenye "unskilled jobs" (kama vile kupiga "dish" subway, carpet cleaning, hotel room makers etc) halafu mnategemea uraia pacha utawaletea mabadiliko......no way, kama vipi mrudi tu nyumbani bado kuna ardhi kubwa tu yenye rutuba.

Deodat,
Jaribu kufikiria ulicho andika. Swala wanaigeria kuchukua uraia wa norway wakati nigeria inaruhusu uraia pacha ni tofauti na mtanzania kunyimwa uraia wa tanzania akiwa raia wa nchinyingine. Tunachongelea nikupoteza uraia wa nchi yako ya hasili ambayo kwa asilimiakubwa utarudi baada ya kuchoka kutafuta maisha. Hao wanaigeria huko norway Wanajua hawatapoteza uraia wa naigeria kwa sheria za nigeria na watarudi kwao kiraisi. Tofauti na bongo huna uhakika utaruusiwa kurudi bongo baada ya kuchukua uraia wa nchi nyingine. Pia watu wanaogopa kama unakanyumba bongo kanaweza kuchukuliwa na wapiga dili kama kagame alivyo chukukua nyuma za wapinzani wake.

Watu wameenda nje kutafuta elimu na maisha na ikabidi wachukue uraia wa nje kwanini waazibiwe kwa kukosa haki ya kisheria ya kurudi kwao hata kama hawajafanikiwa maisha kama unavyowakejeri. Kwanini waazibiwe kwa kujaribu kutafuta maisha nchi za nje wakati Tanzania imekuwa ikishidwa kuwapa watu elimubora kwa miaka mingi mpaka ikabidi watu waende nje kutafuta elimu. Na wengi wanaochukua uraia wa nje ni kwaajili ya kuweza ku-survive. Wa toto wa mafisadi wakienda nje huwa haitaji uraia wa hizo nchi kwasababu hanashida ya Ku-survive nje kwani wazazi wao huchota hela za kifisadi tanzania kiulaini na nje wanaenda kula bata tu.
 
Mkuu umeisoma post ya Chris Lukosi #37 na kuielewa?

Hivi mbunge akuonee wivu..husda...chuki vya nini?

Hivi watawala wanapobana mambo Fulani kulinda maslahi yao wewe kwako ni wivu?

Mataifa makubwa yanapoweka Sera kandamizi kwa nchi masikini ili kulinda maslahi yao wewe hii unaiita chuki? Husda? Wivu? Choyo?

Vita ya maslahi inaweza kupiganwa kwa nyimbo za wivu...choyo..chuki na husda?

Toka awali tunawaambia hii ni very serious issue tofauti na wengi mnavyodhani kwa kutoa sababu nyepesi..

Mtu anapopinga uraia pacha sababu ya maslahi yake huu si wivu wala husda hii ni nature ya capitalism...

Ni wakati wenu na nyinyi kujiratibu na kupigana kwa kutosha na wahafidhina..

Na hii itafanikiwa kwanza kwa diasporas kujipanga na kuwa na umoja madhubiti..( hapa panatiliwa mkazo sababu huko nje watanzania wengi wanachukiana na kuoneana wivu kuliko nyie mnavyoona huku nyumbani?

Pili mtambue hii ni vita ya maslahi si lelemama kama wivu au husda...

Naamini umenipata mpaka hapo..

CC: Kiranga Tuko JMUnish1 Mkandara .. OLESAIDIMU et al

Faida za Tanzania kuruhusu uraia wa nchi mbili ziko wazi. Kubwa ni kwamba Watanzania waliopo nje na waliochukua uraia wa nje (mostly kimaslahi), wataendelea kujisikia "Watanzania" na katika hili nchi itakuwa na chance kubwa zaidi ya kuwafaidi:
1. Kiutaalamu - Katika hili ikumbukwe kuwa ama kiushauri au kiutendaji, kuna sekta bado Tanzania inahitaji uzoefu na utaalamu wa nje ya nchi. Yupo profesa mmoja (wanaomkumbuka jina wanisaidie) ambaye alisema yeye alikuwa anafundisha chuo huko Marekani, hadi siku aliposhangaa anaitwa na mkuu wa chuo hicho akaambiwa "Raisi J. Nyerere anakuhitaji urudi Tanzania ukasaidie kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam". Hadi sasa bado tunawahitaji Watanzania wenzetu waliopo nje kiutaalamu

2. Kifedha - Watanzania wengi waliopo nje na ambao wanaweza kujitunzia vijiakiba kidogo, wangependa wawekeze "nyumbani" kwani wanaamini kuna siku watarudi nyumbani. Lakini kama mtu sio raia tena wa Tanzania, mwamko wa kuwekeza Tanzania hautakuwepo. Kumbukeni kuwa raisi Kikwete anazunguka nje ya nchi mara kwa mara kutafuta wawekezaji. Sijui ni kwa nini tunakataa fursa hii ya wawekezaji watanzania.

3. Kitalii - Hivi tunapovutia watalii tunatarajia ni lazima wawe Wazungu? Maelfu ya Watanzania waliopo nje ya nchi wanarudi kutembea nyumbani kusalimia ndugu na jamaa. Naamini kwa wastani, mtu akija Tz akakaa mwezi mmoja, atatumia zaidi ya shilingi milioni 5. Hivi tukiongelea watu 2500, si tunaongelea bilions?

4. Uhuru - Watanzania wengi waliopo nje na "wakalazimika" kuchukua raia za huko ili wafaidi fursa adimu huko wanajisikia kupoteza uhuru wao pale wanapoona kuwa wao sio watanzania tena. Wazazi ndugu na jamaa wapo Tanzania, kwa kiasi fulani inauma, na inakatisha tamaa. Nyumbani ni nyumbani tu...

5. Hakuna hasara ya kuwa na uraia wa nchi mbili - Hapa ndipo panaponbitatiza kidogo. Ukiacha huo wasiwasi wa Wazanzibari unaotajwa, binafsi sioni nchi itapoteza nini ikiruhusu uraia wa nchi mbili. Hapa ndio maana baadhi ya watu wanawaza "chuki", "Husda", nk.

USHAURI KWA WANA DIASPORA
1. Waungane. Tatizo kubwa linalowatesa sasa ni kugawanyika kisiasa. Waache kuweka siasa za bongo mbele na waweke maslahi ya taifa mbele katika suala hili.

2. Natarajia ndani ya muda mfupi ujao kuwepo na juhudi za kuunganisha wana diaspora. Waongee kwa sauti moja juu ya hili. Juhudi tunazosikia kila siku kufunguliwa tawi la CCM marekani, au la CDM uingereza tuzisikie kuzinduliwa chama cha Wanadiaspora...

Nawasilisha...
 
Hivi kuna ugumu gani wa kuelewa kuwa Diaspora ni Watanzania wenzetu?......hili ni jambo FUNDAMENTAL KABISA la mtu yeyote mwenye akili kulielewa.......linapokuja suala la sheria za uhamiaji.....ndio wana-diaspora wanasema inabidi iangaliwe upya ili iweze kukidhi fundamental rights za Wazawa waishio nje ya nchi......inawezekana kabisa isiwe dual citizenship...inaweza kuwa kuna aina za kutambua haki za mzawa ambazo ni za msingi......hivi nyie watu mnaojifanya hamuelewi.......hivi unahitaji macho ya aina gani ili kuona ndugu yako anakuwa treated ndani ya Tanzania kama foreigner!!!!.......sasa hivi tupo katika mkakati wa kuandika upya katiba yetu.....it is an opportunity kuliweka hili suala vizuri ili ndugu zetu wapate haki yao ya msingi.......

......mfano kuna sheria zamani zilikuwa zinawakandamiza wanawake......nyingi zimebadilishwa ili kuweka haki ya misingi sawa.....it is as simple as that.......kama sheria ziliwekwa zamani haimaanishi hii dunia ni STATIC/IMESIMAMA......mambo yanabadilika na inabidi tu-adjust sheria zetu kuendana na wakati.........

Kuhusu Diaspora na uchumi ni secondary argument na wala halina ubishi....rekodi zipo...sasa ni kitu gani hasa nyie mnaojifanya hamuelewi mnapinga??.....yaani mnataka Diaspora waje kuwawekewa pesa mifukoni mwenu??....hivi kweli wewe unayedai una ndugu zako nje ya nchi (kama ni kweli) unathubutu kusema huelewi faida za kiuchumi kwa ndugu zako kuwapo ughaibuni?.....iwe direct or indirect?.....labda kama hao ndugu zako ni VIBAKA/WABANGAIZAJI then una kila sababu ya kujiuliza faida zake........hata hivyo...kuwa mbangaizaji na yuko nje ya nchi isiwe ndio sababu ya kuwanyima haki yao ya msingi ya uraia wa aliko zaliwa......

Utadhani kiama kitaiangukia Tanzania wakiifuta hiyo sheria inayomnyang'anya Mtanzania mzawa Utanzania wake kisa tu eti kachukua uraia wa nchi nyingine.
 
Faida za Tanzania kuruhusu uraia wa nchi mbili ziko wazi. Kubwa ni kwamba Watanzania waliopo nje na waliochukua uraia wa nje (mostly kimaslahi), wataendelea kujisikia "Watanzania" na katika hili nchi itakuwa na chance kubwa zaidi ya kuwafaidi:
1. Kiutaalamu - Katika hili ikumbukwe kuwa ama kiushauri au kiutendaji, kuna sekta bado Tanzania inahitaji uzoefu na utaalamu wa nje ya nchi. Yupo profesa mmoja (wanaomkumbuka jina wanisaidie) ambaye alisema yeye alikuwa anafundisha chuo huko Marekani, hadi siku aliposhangaa anaitwa na mkuu wa chuo hicho akaambiwa "Raisi J. Nyerere anakuhitaji urudi Tanzania ukasaidie kwenye chuo kikuu cha Dar es Salaam". Hadi sasa bado tunawahitaji Watanzania wenzetu waliopo nje kiutaalamu

2. Kifedha - Watanzania wengi waliopo nje na ambao wanaweza kujitunzia vijiakiba kidogo, wangependa wawekeze "nyumbani" kwani wanaamini kuna siku watarudi nyumbani. Lakini kama mtu sio raia tena wa Tanzania, mwamko wa kuwekeza Tanzania hautakuwepo. Kumbukeni kuwa raisi Kikwete anazunguka nje ya nchi mara kwa mara kutafuta wawekezaji. Sijui ni kwa nini tunakataa fursa hii ya wawekezaji watanzania.

3. Kitalii - Hivi tunapovutia watalii tunatarajia ni lazima wawe Wazungu? Maelfu ya Watanzania waliopo nje ya nchi wanarudi kutembea nyumbani kusalimia ndugu na jamaa. Naamini kwa wastani, mtu akija Tz akakaa mwezi mmoja, atatumia zaidi ya shilingi milioni 5. Hivi tukiongelea watu 2500, si tunaongelea bilions?

4. Uhuru - Watanzania wengi waliopo nje na "wakalazimika" kuchukua raia za huko ili wafaidi fursa adimu huko wanajisikia kupoteza uhuru wao pale wanapoona kuwa wao sio watanzania tena. Wazazi ndugu na jamaa wapo Tanzania, kwa kiasi fulani inauma, na inakatisha tamaa. Nyumbani ni nyumbani tu...

5. Hakuna hasara ya kuwa na uraia wa nchi mbili - Hapa ndipo panaponbitatiza kidogo. Ukiacha huo wasiwasi wa Wazanzibari unaotajwa, binafsi sioni nchi itapoteza nini ikiruhusu uraia wa nchi mbili. Hapa ndio maana baadhi ya watu wanawaza "chuki", "Husda", nk.

USHAURI KWA WANA DIASPORA
1. Waungane. Tatizo kubwa linalowatesa sasa ni kugawanyika kisiasa. Waache kuweka siasa za bongo mbele na waweke maslahi ya taifa mbele katika suala hili.

2. Natarajia ndani ya muda mfupi ujao kuwepo na juhudi za kuunganisha wana diaspora. Waongee kwa sauti moja juu ya hili. Juhudi tunazosikia kila siku kufunguliwa tawi la CCM marekani, au la CDM uingereza tuzisikie kuzinduliwa chama cha Wanadiaspora...

Nawasilisha...

Katika wana diaspora wote wewe umekuja na hoja mujarabu...

Kwanza nikupongeze kwa hilo..

Umeongea vitu vya msingi na ni kweli kabisa suala hili linapaswa libebwe kwa hoja hizi..

Mi nashangaa watanzania wenzetu waishio huko Kuwa na tabia hizi..

1. Kutokuwa wamoja.. Hapa nakupa kisa kimoja wakati nipo US enzi zile za mama Maajar..
Kuna watanzania Fulani walikua wanapeleka umbea kwa diplomat flan dhidi ya wenzao..
Yalikuwa ni maneno ya chuki..fitina na dharau..

Wenyeji waliniambia hiyo ndio hali halisi..na ktk hali hii umoja wa kusimama kwa hoja ya nguvu unatoweka..

2. Kudharau nyumbani;
Ndugu zetu wengi wamekua na matendo na kauli. Mbaya za kudharau nyumbani na utu wa mwafrika kwa ujumla sitarejelea kauli hizo kwakuwa zinajulikana...Kauli hizi zinatumiwa na wahafidhina kama silaha kuu ya kipropaganda kuwafanya wanyumbani waukatae utaratibu Huu..
Kwa hili tunahitaji kubadilika hivyo baadhi ya diaspora waache tabia za dharau..kujifanya ujuaji sana...kashfa n.k n.k

3. Kuwa na mambo ya msingi ya kusimamia pindi viongozi wa kitaifa wawapo huko..
Hapa ndo swala la ufunguzi wa matawi ya chama....kupiga picha....mambo binafsi n.k n.k
Kwakweli suala la matawi ya vyama vya siasa ni threat kubwa ya kubomoa umoja na mshikamano wenu hilo hata Mimi siliungi mkono..

Inatakiwa kuonesha kwa vitendo kabisa pindi wanasiasa wawapo huko ikibidi hata kwa kukunja sura bila kujali kunyimwa nafasi ya kupiga picha kwamba mnataka dual citizenship

Ila kauli za wivu..husda...choyo...chuki zinaamsha mapambano na majibizano yasiyo na msingi..

Tukiyafanyia kazi hayo mapungufu nafikiri ushindi utapatikana ktk vita hii ya maslahi...
 
Ati mtu anapinga sababu anajibu "Sijui faida zake"
Duh! Wabongo wengine kwa kufuata mkumbo, mtu hajui hata anachochangia ni nini ilimradi kaona aliyereply wa kwanza naye anaunga mkono.. Nch zote ambazo wamekubaliana na hii system si wajinga, cheki wa-nigeria walivotupiga gep kwenye uchumi, kila sehemu nmetembea hawa jamaa wapo na wanapiga hela kirahisi sana, wakirudi home ni watu wenye pesa safi kabisa.. Bongo restrictions za ovyo tu, ila am sure hili swala soon litakubalika tu, maswala ya mjipange kuleta sijui evidence gani ni ujinga, kama serikali hili swala haijakaa ilichunguze ijue lina faida au hasara gani, yani hadi wananchi waje waanza kuwaconvince, wakiwadanganya je? Bongi bongo kweli, ingekua nje jamaa wangekua washaweka institution inafanya research ya faida na hasara na kukusanya data zote then kutoa conclusion, bongo ati unasikia mtuconvince, imekua proposal ya ndoa hii?
 
I see the scourge of generalization manifests its exacerbation, whilst the plague of reductivist ignominy rear its ugly head vociferously.

Mkuu naamini hayo maneno hatayaelewa kwakumsaidia mwandikie tu kwa kibongo maana naona mentally kijana ame shake!!!
 
Utadhani kiama kitaiangukia Tanzania wakiifuta hiyo sheria inayomnyang'anya Mtanzania mzawa Utanzania wake kisa tu eti kachukua uraia wa nchi nyingine.

Tatizo elimu..

Wananchi wa kawaida wakielewa umuhimu wa hili itakua anguko kuu kwa wahafidhina wa msimamo huu...
 
Katika wana diaspora wote wewe umekuja na hoja mujarabu...

Kwanza nikupongeze kwa hilo..

Umeongea vitu vya msingi na ni kweli kabisa suala hili linapaswa libebwe kwa hoja hizi..

Mi nashangaa watanzania wenzetu waishio huko Kuwa na tabia hizi..

1. Kutokuwa wamoja.. Hapa nakupa kisa kimoja wakati nipo US enzi zile za mama Maajar..
Kuna watanzania Fulani walikua wanapeleka umbea kwa diplomat flan dhidi ya wenzao..
Yalikuwa ni maneno ya chuki..fitina na dharau..

Wenyeji waliniambia hiyo ndio hali halisi..na ktk hali hii umoja wa kusimama kwa hoja ya nguvu unatoweka..

2. Kudharau nyumbani;
Ndugu zetu wengi wamekua na matendo na kauli. Mbaya za kudharau nyumbani na utu wa mwafrika kwa ujumla sitarejelea kauli hizo kwakuwa zinajulikana...Kauli hizi zinatumiwa na wahafidhina kama silaha kuu ya kipropaganda kuwafanya wanyumbani waukatae utaratibu Huu..
Kwa hili tunahitaji kubadilika hivyo baadhi ya diaspora waache tabia za dharau..kujifanya ujuaji sana...kashfa n.k n.k

3. Kuwa na mambo ya msingi ya kusimamia pindi viongozi wa kitaifa wawapo huko..
Hapa ndo swala la ufunguzi wa matawi ya chama....kupiga picha....mambo binafsi n.k n.k
Kwakweli suala la matawi ya vyama vya siasa ni threat kubwa ya kubomoa umoja na mshikamano wenu hilo hata Mimi siliungi mkono..

Inatakiwa kuonesha kwa vitendo kabisa pindi wanasiasa wawapo huko ikibidi hata kwa kukunja sura bila kujali kunyimwa nafasi ya kupiga picha kwamba mnataka dual citizenship

Ila kauli za wivu..husda...choyo...chuki zinaamsha mapambano na majibizano yasiyo na msingi..

Tukiyafanyia kazi hayo mapungufu nafikiri ushindi utapatikana ktk vita hii ya maslahi...

Mkuu, wakisubiri fursa hii wataumia.
1. Viongozi wawapo nje, wanakuwa eneo moja kwa wakati mmoja, na Watanzania huko nje wameenea dunia nzima

2. Kukutana na kiongozi nje ya nchi kunafanya mnaonekana kama "wageni"...

Mi napendekeza zianzishwe harakati za kutetea suala la "uraia wa nchi mbili". Makao makuu ya harakati hizi yawe DAR ES SALAAM... Mikutano, semina, makongamano nk zinazohusiana na harakati hizi zifanyike exclusively Dar es Salaam na naamini wapo wengi watakaosafiri kutoka nje kuhudhuria. Association za Watanzania kwenye miji tofauti huko nje zinaweza kuwasapoti wawakilishi wao wakahudhuria pia. Ingawa harakati hizi wadau wake wakubwa watakuwa Wanadiaspora, lakini zihusishe wadau wa ndani pia (naamini wapo wengi hapo hapo Tanzania, kwa namna moja au nyingine wanatetea hili suala). Wafanye mikutano na makongamano, wawaite wabunge (wa nyama vyote) na viongozi wa serikali, watetee hoja yao mbele yao. Bila shaka watashinda, kwa faida ya wanadiaspora wa sasa, wa baadae, na taifa kwa ujumla...
 
Nafikiri hilo ni sahihi but utakubaliana nami kuwa umoja kwanza baina ya diasporas ndio nguzo ya pekee katika hayo...
 
Yap... Umoja ndio nguzo pekee... Ndio maana niaksema wajiunganishe. But wasijiunganishe kutokea London au Washington... Wajiunganishe kutokea Dar es Salaa, ili kuonyesha bado wanauthamini "Utanzania" wao...
 
Well said
 
Nani atakaeanza sasa maana kwa hao waDiasp wengi wanalalamika hawana umoja huko huko wanakoishi

Sent from Mchina
 
Hapo ndio pagumu... lakini sio pagumu sana. Mkuu naamini wewe unaweza kuanzisha umoja huo...
 
Back
Top Bottom