Naona hujanielewa au labda ni mi sijakuelewa. Me sitaki kuongelea swala la nationality, my concern hapa ni citizenship. Na niseme tu naona unajikanganya, Unaposema mtu akitaka uraia wa Tanzania, na kama yeye ni mkenya itabidi aukane uraia wa Kenya. Ndio hasa ambacho si tunakitaka. We know these guys, bado hatujafikia hatua ya kuwa comfortable nao.
Na unaposema sheria ya inayopinga dual citizenship haimzuii mkenya kuwa na uraia wa Tanzania, me sielewi. Una maana kwamba mtu anaweza akaja Tanzania na kupata uraia bila kuukana uraia wa nchi yake. Kama ndio maana yako, basi nadhani unapaswa ku-revisit the facts.
Kama hujanielewa kwa mfano huo, basi sijui nikueleze nini ndugu yangu ili uelewe. Mdau hapo chini kishakujibu, na nchi karibu zote duniani kote citizenship ya kuzaliwa haipokonywi.
Nitasisitiza tena, Mkenya na mtu yeyote kutoka nchi zingine akija Tanzania akajifanya ana ukana uraia wake kwa kutumia sheria ya kinyanyembe iliopo, hapo ana wa mock tu na sheria yenu ya kinyanyembe. Kimsingi, anakuwa hajapoteza uraia wake wa kuzaliwa hii si kwa mkenya tu ni karibu nchi zote duniani ikiwemo korea kaskazini na Russia. Hivyo atajifanya anaukana uraia wake mnampa passport anarudi kwao anapewa passport nyingine.
Hivyo sheria hiyo ya kinyanyembe haimzuii mkenya kumiliki passport ya Tanzania na Kenya kwa wakati mmoja. Bali inamzuia Mtanzania wa kuzaliwa kumliki passport zaidi ya moja. Ni sheria kadamizi kwa watanzania wazawa tu, wakati inatoa loop hole ya dual kwa watu wasio wazawa. Sasa sheria ya Kinyanyembe na kilugaluga namna hii inalinda vipi masilahi ya Tanzania? ni sheria ya kijuha iliyopita viwango vyote vya kijuha.