Chuki na husda dhidi ya wanaDiaspora

Chuki na husda dhidi ya wanaDiaspora

_42481604_africa_migration416x363.gif


Hivi chuki dhuidi ya wana diaspora na hasa toka kwa wanasiasa na watu wenye hali nzuri za kimaisha hapa nyumbani inatokana na nini?

Cha ajabu ni kuwa mawaziri na viongozi kadhaa wa serikali ya nchi hii watoto wao wana uraia wa nchi mbili mbili japo sheria hiyo haipo. Mfano Waziri wa mambo ya nchi za nje ambaye diaspora iko chini yake, Bw Bernard Membe, watoto wake ni raia wa Canada, Sisemi kuwa kuwa na uraia wa nje ni dhambi lakini ungetegemea kuwa alikuwa na uwezo wa kuwaandikisha wanae kuwa ni raia wa Tanzania lakini alikubali waandikishwe kuwa ni raiua wa Canada. Cha ajabu ni kuwa Mheshimiwa Membe amekjuwa kimya sana huku watanzania ambao wako Diaspora wakiendelea kusulubiwa na wanasiasa na vyombo vya habari hii inanipelekea kulizia kuwa hivi chuki na husda dhidi ya wana Disapora (ambao wengi wao ni watoto wa maskini) inatokana na nini hasa?

Hivi vyama vya siasa vina maoni gani kuhusu hili suala?

Watanzania tuna choyo cha chuki badala ya kuwa na mapenzi na mafanikio ya wenzetu. Unawezaje kumnyima mtu haki yake? Maadam amezaliwa Tanzania atabaki kuwa Mtanzania tu.
Tunakataa ndugu zetu lakini mazao wanayochuma tunayapapatikia. Angalia mtu atokae nje jamaa na marafiki wanavyomzonga ili wapate chochote!
 
Ndugu yangu malcolmX

Unapaswa kutambua kilicho nyuma ya vikwazo vya suala hili si chuki na husda kama unavyodhani...

Tena umesema wanasiasa na matajiri ndio wenye chuki na husda dhidi ya diasporas je chuki na husda yao nini dhidi ya diasporas?

Kuanzisha mada kwa mrengo huo sidhani kama utapata uchangiaji mzuri toka kwa wadau..

jaribuni kujenga hoja zenye mashiko ambazo zitawashawishi ndugu zenu kulikubali hili suala..

Nimefuatilia mijadala mingi juu ya suala hili hapa jf na nje ya jf lakini sijawahi ona diaspora yoyote akitoa hoja ya mashiko ktk uchangizi wake zaidi ya kusema tunaonewa wivu...chuki..husda n.k n.k

mbaya zaidi hamuelezi hizo chuki..wivu..husda zinaletwa na nini hasa maana hao wanasiasa mnaowashutumu wengi wana ndugu na watoto nje ya nchi....

Kwanini msibadili aina hii ya mawazo na mje na hoja mujarabu?

Membe amepigania sana hii issue kwenye katiba mpya alikwama kwanini?

Kwenda kwa maneno mepesi namna hii katika issue nzito kama hii inayowaumiza itawagharimu wenyewe...

Jaribuni kubadilika maana mi sioni chuki..husda..wivu dhidi yenu unatoka wapi na kwanini ikiwa kwenda nje kila mtu akitaka anaweza kwenda kama wafanyavyo wengine sasa hapo sijui unaweza semaje..

Binafsi issue hii inanigusa pia kwakuwa nina ndugu na jamaa Nje ila tatizo kubwa lililopo kwetu ni uelewa juu ya jambo hili kwa wadau...

Kila la kheri..

Ndugu yangu unataka kuwekwe hoja gani ili mtu adai haki yake iliyo dhahiri. Kwani hao wanaozuia wanatowa hoja gani za maana?
Iwapo Mtanzania wa kuzaliwa anaonekana ni tatizo lakini kwanini mafao yake yasiwe tatizo.
Tatizo zima ni ufinyu wa kupambanua. Kwanini ulazimishe raia wako aukane uraia wake ili kupata uraia wa nchi nyengine? Kwanini isiwe mtu kuukana uraia kwa hiyari? Iwapo mazingira yanamlazimisha raia wako kutafuta njiaya kupata kipato nje ya nchi kwanini iwe nongwa?
 
Wewe si umeona hapo kwenye ramani, hapa Tanzania hao watu hawasaidii kitu. Mwaka 2011 Diaspora wa Ethiopia waliweza kutengeneza reliable electricity dam chini ya kiongozi marehemu Meles Zenawi. Kumbuka misaada mingi ya nje siyo ya nia nzuri ama ya kutuwezesha kujikomboa. Sasahivi Ethiopia wataweza kujitosheleza umeme na mwingine mwingi watauza nchi za jirani. Hawa wa kwetu wengi experience siyo nzuri, wakirudi wanakimbilia siasa na wanafanya madudu (ref. Masha, Nyalandu etc).

Halafu wengi wao huko ng'ambo ni wabangaizaji kama kina Chris Lukos, na wengine wakirudi huku hawaji kuwekeza waliyotokanayo huko, badala yake wanakuja kujificha kwenye siasa na kutafuta mianya ya ufisadi (Le Mutuz).
Kwani wakiwa na uraia wa nchi mbili tunaathirika vipi?
 
Watanzania ni porojo sana popote pale walipo, hawaishi kutafuta visingizio. Watu wenye nia ya kuwekeza nchini kwao hawaitaji uraia pacha kufanya hivyo. Tumewaona wapopo (wanaijeria) walioko kwenye nchi zinazokataa uraia pacha kama Norway, lakini wanaukana uraia wao na bado wanawekeza nyumbani. Acheni porojo, mjitume...ongezeni ujuzi mpate kazi za maana au muanzishe miradi yenu huko ughaibuni na mnaweza kuja huku nyumbani hata kama foreign investors (tena wengi hamjui tu, Tanzania inawajali foreign investors kuliko wazawa). Tatizo lenu wengi mmejikita kwenye "unskilled jobs" (kama vile kupiga "dish" subway, carpet cleaning, hotel room makers etc) halafu mnategemea uraia pacha utawaletea mabadiliko......no way, kama vipi mrudi tu nyumbani bado kuna ardhi kubwa tu yenye rutuba.

Deodat, yaani hapo ndo umemwaga nondo mpaka umefikia kikomo? Kwa hoja kama hizo, haishangazi mwanzilishi wa huu mjadala anatoa hoja kwamba Wabongo kinachotusumbua ni chuki na husda. Aina ya kazi anayofanya mtu ughaibuni ni uamuzi wake mwenyewe. Kuna watu wanavaa suti wanalipwa hela kidogo kuliko wazibua vyoo. Mbona Bongo kuna watu wanasukuma mkokoteni lakini wanasomesha watoto na wameridhika? Kazi ni kazi ilimradi mkono uende kinywani.

Kama sisi Wabongo tulioko nyumbani hatutaki uraia pacha - maana sisi ndo tunagoma, tuje na sababu zenye mshiko kuonesha kwamba kweli uraia pacha haukubaliki. Lakini vijembe na maneno ya kejeli yanadhibitisha tu kwamba kweli tuna wivu na husda tu badala ya sababu za msingi.
 
Mkuu ukiangalia asilimia kubwa ni wale wanaoogopa kupoteza nafasi zao kisiasa iwapo walio nje wataruhusiwa.

Solution kwa mtu anaetaka kuwa mwanasiasa TZ ni kuukana uraia alionao sasa na kurudi nyumbani kugombea

Mimi ni mhehe wa Kalenga, baba katokea Kalenga na mama Katokea Tosa maganga, wanangu pia ni full wahehe, sasa kesho nirudi nyumbani nione kenge yeyote ananisumbua, kwanza wengine ni wanyarwanda na warundi tu..
Uje na rambirambi zote za marehemu Dav Mwangosi,

Pia uje na doz za kutosha za ule ugonjwa wako.
 
Mkuu ukiangalia asilimia kubwa ni wale wanaoogopa kupoteza nafasi zao kisiasa iwapo walio nje wataruhusiwa.

Solution kwa mtu anaetaka kuwa mwanasiasa TZ ni kuukana uraia alionao sasa na kurudi nyumbani kugombea

Mimi ni mhehe wa Kalenga, baba katokea Kalenga na mama Katokea Tosa maganga, wanangu pia ni full wahehe, sasa kesho nirudi nyumbani nione kenge yeyote ananisumbua, kwanza wengine ni wanyarwanda na warundi tu..

Ha ha ha

Mkuu wangu Chris Lukosi

Umeongea point
Kidogo wewe unaonyesha uko deep ktk kuelewa kinachoendelea juu ya hili swala la uraia pacha..

Kidogo kupitia hii point yako nimepata picha kwanini baadhi ya wanasiasa wanapinga hilo...
Hapo ni kulinda maslahi yao sasa nashangaa wenzio wanaokuja na point nyepesi nyepesi na za kitoto eti ooh wivu.. Mara chuki sijui husda mpaka mtu unaduwaa..

Hiyo hoja yako kidogo serious kwamba shida ni hofu ya kupokwa mnofu na hii si kwenu tu hata huku ni vivyo hivyo..

BTW utaniambia unarudi mwezi wangapi ili nifanye mchakato wa kuagiza gari kabla hujaja huku...
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu unataka kuwekwe hoja gani ili mtu adai haki yake iliyo dhahiri. Kwani hao wanaozuia wanatowa hoja gani za maana?
Iwapo Mtanzania wa kuzaliwa anaonekana ni tatizo lakini kwanini mafao yake yasiwe tatizo.
Tatizo zima ni ufinyu wa kupambanua. Kwanini ulazimishe raia wako aukane uraia wake ili kupata uraia wa nchi nyengine? Kwanini isiwe mtu kuukana uraia kwa hiyari? Iwapo mazingira yanamlazimisha raia wako kutafuta njiaya kupata kipato nje ya nchi kwanini iwe nongwa?

Shida sio nongwa...

Shida uelewa..
Toa hoja zako ili nikukubalie au nikukatalie kulalamika hakuleti suluhu...
 
Majoka ya mdimu nyinyi, "tunaemdesha mambo yetu" gani hayo zaidi ya ufisadi na wizi wa mali za ummah.

Kama huku kumejaa ufisadi si mbaki huko huko. Mnataka uraia wa nchi iliyojaa ufisadi. Hii nchi tutajenga wenyewe, mbona hapo kwenye ramani sijaiona Botswana, Namibia, Angola etc nchi ambazo zimepiga maendeleo makubwa kiuchumi bila hayo "mabilioni" yenu.
 
Shida sio nongwa...

Shida uelewa..
Toa hoja zako ili nikukubalie au nikukatalie kulalamika hakuleti suluhu...

Hoja inakuwa hoja pale mnajadili kitu lakini pale mmoja anapofanya kuwa yeye ni juu ya mwenziwe basi yule wa chini huwa hatowi hoja bali hutowa malalamiko.
Kama unataka hoja basi wewe mwenyewe usiwaone wanaolalamika kuwa wana kosa.
Wachukulie Watanzania hao kama wewe halafu kuzungumzie hoja.
Mkuu anza kwa kueleza nini kosa la Watanzania hao ili tuone kwanini wanastahiki kuwekwa nafasi waliyowekwa.
 
Uje na rambirambi zote za marehemu Dav Mwangosi,

Pia uje na doz za kutosha za ule ugonjwa wako.

This is too silly..

Watu wanaongea mambo ya maana unaleta habari ya khanga..

Imbecilic!!!
 
Hoja inakuwa hoja pale mnajadili kitu lakini pale mmoja anapofanya kuwa yeye ni juu ya mwenziwe basi yule wa chini huwa hatowi hoja bali hutowa malalamiko.
Kama unataka hoja basi wewe mwenyewe usiwaone wanaolalamika kuwa wana kosa.
Wachukulie Watanzania hao kama wewe halafu kuzungumzie hoja.
Mkuu anza kwa kueleza nini kosa la Watanzania hao ili tuone kwanini wanastahiki kuwekwa nafasi waliyowekwa.

Mimi sioni kosa..

Nataka hoja ili nikubali au nikatae kwakuwa ki sheria hilo swala halipo..
Ili turejee kurekebisha sheria ndo panapohitajika michango kuntu ya wadau kushawishi mabadiliko ya sheria..
Hiyo dhana ya kosa iondoe coz watu nje wanaenda tafuta fursa za maisha ambazo hapa home ni chache...
 
Kama huku kumejaa ufisadi si mbaki huko huko. Mnataka uraia wa nchi iliyojaa ufisadi. Hii nchi tutajenga wenyewe, mbona hapo kwenye ramani sijaiona Botswana, Namibia, Angola etc nchi ambazo zimepiga maendeleo makubwa kiuchumi bila hayo "mabilioni" yenu.

Mabilioni wapi ndugu yangu, wengi wana survive tu ila kama ilivyo kawaida ya mtanzania huja na sababu zisizo na mwisho.

1. Kama una mabilioni njoo wekeza, uraia wa kigeni sio kikwazo, ni faida kwako kwasababu utapata incentives zote kama foreign investor na bado una advantage ya kuwa na uelewa wa local business environment.

2. Kama umedhamiria kupata nafasi ya kisiasa, njoo ugombee, akina Nyalandu si hao wamekaa huko ughaibuni na sasa ni wanasiasa wakubwa tu.......

3. Tatizo lenu wengi ni wababaishaji, mnataka uraia pacha ili mje m-test temperature of the water, hasa kwenye ulingo wa kisiasa, mambo yakiwa magumu mgeuze mlikotoka........

4. ooh, sijui wanasiasa wanaogopa tutachukua nafasi zao, nosense! - yaani kukaa kote huko ulaya tunategemea mje na business models za ukweli kumbe wenzetu bado mmetawaliwa na mawazo ya vijiwe vya kahawa. Tena niwaonye, mkija kugombea nafasi za kisiasa bila kuwa na agenda za msingi mtaangukia pua vibaya. Nimemuona mwenzenu mmoja aliyerudi 2010 akagombea, kampeni nzima yeye anatueleza ooh mimi nilikuwa sijui Netherlands, mara UK, nikaenda na US nimeona mengi......porojo nyingi bila kuonyesha mikakati ya kuleta mabadiliko, alipigwa chini vibaya mno.

Narudia tena, watu wenye malengo ya kufanya maendeleo ya kiuchumi nyumbani swala la uraia pacha sio kikwazo, na kama ni kikwazo basi nyie mlioko huko nje mtoe concrete cases ku-substantiate hoja zenu. Sisi wa huku nyumbani (aka wala vumbi) tunasema uraia pacha hauna hoja zenye mashiko, sasa nyie wenzetu mlioona mwanga mje na arguments na concrete cases to argue otherwise.
 
[h=1]How to improve diaspora engagement[/h]Asian governments serious about engaging diaspora groups more effectively must commit to building the capacity of the institutions they create


  • Share0

  • in[COLOR=#333333 !important]Share
[/COLOR]

TRADITIONAL-SRI-LANKAN-FI-007.jpg
A Sri Lankan fisherman. Sri Lanka has been among the Asian countries that have set up a ministry to engage its diasporas. Photograph: Reuters

Policymakers in the Asia-Pacific region increasingly recognise the value that diaspora populations bring to development efforts at home. Some governments in the region have taken an extra step in institutionalising their engagement with the diaspora by creating special offices or directorates within government agencies. Within Asia, 14 government institutions were created specifically to engage diasporas on a formal basis, occupying different levels of government and exhibiting diverse priorities and degrees of organisation.
Countries like India have established ministries to address the needs of diaspora populations.Ministry for Overseas Indian Affairs was formed in 2004 to address the lack of government policy coordination on migration and to implement programmes that reach out to the Indian diaspora. Bangladesh andSri Lanka also have established ministries to engage their diasporas.
A few diaspora institutions in Asia fall short of full ministry standing but still report directly to the highest executive body and enjoy a fairly influential position within the government. For instance, China's Overseas Chinese Affairs Office, which among other duties operates two universities catering mainly to the Chinese diaspora, is uniquely positioned under the state council, the country's highest executive body.
Similarly, the Philippines' Commission on Filipinos Overseas (CFO) is directly under the Office of the President. Established in 1980, the commission has a dual role of promoting both economic and cultural ties between the Philippines and its diaspora. The government also institutionalised diaspora engagement at the sub-ministry level by creating three special offices under the departments of labour and employment and foreign affairs.
Diaspora engagement does not stop at the national level. Diasporas are often inclined to engage at the local level, usually in their place of origin, where they are familiar with the context and, in many cases, still have family ties. Some states in India, for instance, have diaspora offices, the most active of which can be found in Kerala and Gujarat.
Some diaspora-engagement organisations are not clearly within the realm of government. In 1997, the South Korea government established the Overseas Koreans Foundation, a nonprofit organisation affiliated with the ministry of foreign affairs and trade. The foundation had a clear development mandate from the outset: to "utilise the capabilities of overseas Koreans for national development in line with its globalisation policy."
While many governments acknowledge the importance of diaspora engagement in development, many still lack the capacity to design effective policies and implement them on a meaningful scale. This explains the gap between schemes that look good on paper and truly effective policies and programmes that actually make a difference. Indeed, effective engagement almost always requires a concerted effort towards capacity building.
For many countries in Asia and elsewhere, the main challenges to effective engagement appear to centre on two issues: how best to obtain adequate funding and how to improve technical know-how. Governments serious about engaging diasporas have to commit to funding their efforts as fully as possible (and seeking funds from elsewhere to fill in remaining gaps) and to obtaining the operational knowledge and skills needed to pursue goals effectively. Indeed, for many governments, one of the most pressing challenges to diaspora engagement is how to support institutions that do not drain already limited public coffers while bringing in critical financial resources.
Ongoing monitoring, evaluation, and frequent adjustments should also be the foundation of any diaspora institution. Most appear to have placed significant resources at the front end while neglecting the feedback loop. Even if a government effectively facilitates emigrants' return or has built up an active network of diaspora members, it is crucial to monitor programme implementation, measure impact, and use findings to further improve engagement within and outside government.
Due to limited monitoring and evaluation, it is difficult to fully assess the effectiveness of diaspora institutions, not to mention their impact on development efforts at home. Nonetheless, their experiences still offer three important lessons, especially for governments in the west, which are contemplating engaging their own diasporas.
First, successfully creating formal government institutions requires serious preparatory work aimed at understanding diasporas' needs, wants, and potential; appraising the current government approach to diaspora engagement; and learning from the experiences of other countries. The Indian government, for instance, tasked a high-level committee with recommending a broad but flexible policy framework and country-specific plans to engage the estimated 20 million Indians abroad. For two years, a five-person committee undertook a mapping exercise focused not only on identifying the size and locations of the diaspora but also its members' skills, capacity, and willingness to engage.
Second, how institutions are created and how their activities are chosen are also critical indicators of success. During the planning phase it is important to delineate clearly the division of responsibilities inside and across government agencies and to establish sufficient buy-in from key actors. If an institution does not have legitimacy, it will become susceptible to political manipulation. Careful planning and communication are particularly important because some diasporas have little trust in their origin-country governments. Among diasporas that emigrated for mainly economic reasons, a perception of pervasive corruption and ineffective governance at home can also impede a government's ability to build trust. The Indian and Filipino diaspora are examples of a long-standing and economically driven diaspora whose trust had to be regained before the institutionalisation process could succeed.
Diaspora-engaging institutions should also invite diaspora involvement in setting their agendas to generate trust and ownership. Governments should take care, however, to avoid creating a privileged "insider" group of diaspora partners.
Based in Manila, Dovelyn Rannveig Agunias is a senior policy analyst with the Migration Policy Institute, an independent think tank that analyses international migration policy


 
Hivi kuna ugumu gani wa kuelewa kuwa Diaspora ni Watanzania wenzetu?......hili ni jambo FUNDAMENTAL KABISA la mtu yeyote mwenye akili kulielewa.......linapokuja suala la sheria za uhamiaji.....ndio wana-diaspora wanasema inabidi iangaliwe upya ili iweze kukidhi fundamental rights za Wazawa waishio nje ya nchi......inawezekana kabisa isiwe dual citizenship...inaweza kuwa kuna aina za kutambua haki za mzawa ambazo ni za msingi......hivi nyie watu mnaojifanya hamuelewi.......hivi unahitaji macho ya aina gani ili kuona ndugu yako anakuwa treated ndani ya Tanzania kama foreigner!!!!.......sasa hivi tupo katika mkakati wa kuandika upya katiba yetu.....it is an opportunity kuliweka hili suala vizuri ili ndugu zetu wapate haki yao ya msingi.......

......mfano kuna sheria zamani zilikuwa zinawakandamiza wanawake......nyingi zimebadilishwa ili kuweka haki ya misingi sawa.....it is as simple as that.......kama sheria ziliwekwa zamani haimaanishi hii dunia ni STATIC/IMESIMAMA......mambo yanabadilika na inabidi tu-adjust sheria zetu kuendana na wakati.........

Kuhusu Diaspora na uchumi ni secondary argument na wala halina ubishi....rekodi zipo...sasa ni kitu gani hasa nyie mnaojifanya hamuelewi mnapinga??.....yaani mnataka Diaspora waje kuwawekewa pesa mifukoni mwenu??....hivi kweli wewe unayedai una ndugu zako nje ya nchi (kama ni kweli) unathubutu kusema huelewi faida za kiuchumi kwa ndugu zako kuwapo ughaibuni?.....iwe direct or indirect?.....labda kama hao ndugu zako ni VIBAKA/WABANGAIZAJI then una kila sababu ya kujiuliza faida zake........hata hivyo...kuwa mbangaizaji na yuko nje ya nchi isiwe ndio sababu ya kuwanyima haki yao ya msingi ya uraia wa aliko zaliwa......
 
Ndugu yangu malcolmX

Unapaswa kutambua kilicho nyuma ya vikwazo vya suala hili si chuki na husda kama unavyodhani...

Tena umesema wanasiasa na matajiri ndio wenye chuki na husda dhidi ya diasporas je chuki na husda yao nini dhidi ya diasporas?

Kuanzisha mada kwa mrengo huo sidhani kama utapata uchangiaji mzuri toka kwa wadau..

jaribuni kujenga hoja zenye mashiko ambazo zitawashawishi ndugu zenu kulikubali hili suala..

Nimefuatilia mijadala mingi juu ya suala hili hapa jf na nje ya jf lakini sijawahi ona diaspora yoyote akitoa hoja ya mashiko ktk uchangizi wake zaidi ya kusema tunaonewa wivu...chuki..husda n.k n.k

mbaya zaidi hamuelezi hizo chuki..wivu..husda zinaletwa na nini hasa maana hao wanasiasa mnaowashutumu wengi wana ndugu na watoto nje ya nchi....

Kwanini msibadili aina hii ya mawazo na mje na hoja mujarabu?

Membe amepigania sana hii issue kwenye katiba mpya alikwama kwanini?

Kwenda kwa maneno mepesi namna hii katika issue nzito kama hii inayowaumiza itawagharimu wenyewe...

Jaribuni kubadilika maana mi sioni chuki..husda..wivu dhidi yenu unatoka wapi na kwanini ikiwa kwenda nje kila mtu akitaka anaweza kwenda kama wafanyavyo wengine sasa hapo sijui unaweza semaje..

Binafsi issue hii inanigusa pia kwakuwa nina ndugu na jamaa Nje ila tatizo kubwa lililopo kwetu ni uelewa juu ya jambo hili kwa wadau...

Kila la kheri..

Hoja ya mashiko si ndio hiyo kwamba tatizo ni CHUKI?
 
Mimi nawashangaa sana watanzania mlioko nje... kutwa mnashindana kufungua mashina ya CCM utafikiri ndiyo inawapa kula huko,,, yakija mambo ya msingi kama haya ndiyo wa kwanza kulalamika!!...

Serikali ya MaCCM endeleen kuwabania hawa wanafiki wanje maana wamezidi kujipendekeza
 
Mimi sioni kosa..

Nataka hoja ili nikubali au nikatae kwakuwa ki sheria hilo swala halipo..
Ili turejee kurekebisha sheria ndo panapohitajika michango kuntu ya wadau kushawishi mabadiliko ya sheria..
Hiyo dhana ya kosa iondoe coz watu nje wanaenda tafuta fursa za maisha ambazo hapa home ni chache...

Sheria hiyo imo ndani ya Katiba ya zamani ambayo sote tunakubali kuwa imepitwa na wakati. Tatizo la Katiba hiyo iliundwa kukidhi wakati fulani na mambo yameshabadilika.
Ndio maana nikakuuliza wewe unaona tukiwapa uraia ndugu zetu hao tutaathirika na nini au wataleta matatizo gani?
 
Hoja ya mashiko si ndio hiyo kwamba tatizo ni CHUKI?

Mkuu umeisoma post ya Chris Lukosi #37 na kuielewa?

Hivi mbunge akuonee wivu..husda...chuki vya nini?

Hivi watawala wanapobana mambo Fulani kulinda maslahi yao wewe kwako ni wivu?

Mataifa makubwa yanapoweka Sera kandamizi kwa nchi masikini ili kulinda maslahi yao wewe hii unaiita chuki? Husda? Wivu? Choyo?

Vita ya maslahi inaweza kupiganwa kwa nyimbo za wivu...choyo..chuki na husda?

Toka awali tunawaambia hii ni very serious issue tofauti na wengi mnavyodhani kwa kutoa sababu nyepesi..

Mtu anapopinga uraia pacha sababu ya maslahi yake huu si wivu wala husda hii ni nature ya capitalism...

Ni wakati wenu na nyinyi kujiratibu na kupigana kwa kutosha na wahafidhina..

Na hii itafanikiwa kwanza kwa diasporas kujipanga na kuwa na umoja madhubiti..( hapa panatiliwa mkazo sababu huko nje watanzania wengi wanachukiana na kuoneana wivu kuliko nyie mnavyoona huku nyumbani?

Pili mtambue hii ni vita ya maslahi si lelemama kama wivu au husda...

Naamini umenipata mpaka hapo..

CC: Kiranga Tuko JMUnish1 Mkandara .. OLESAIDIMU et al
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ukiangalia asilimia kubwa ni wale wanaoogopa kupoteza nafasi zao kisiasa iwapo walio nje wataruhusiwa..... kwanza wengine ni wanyarwanda na warundi tu..

Bw mkubwa naona kinamna una'echo' ile article ya lile gazeti .... la Rwanda
 
Back
Top Bottom