Chuki dhidi ya Rais Samia ni kwasababu ni mwanamke

Chuki dhidi ya Rais Samia ni kwasababu ni mwanamke

2999586_2537165_P6F2RAW0ULeENPMJA9tbbCN4.jpg


Marehemu Pungu alikuwa bingwa wa Hadaa akiwa na Chawa wake Madhubuti aliyegeuka Mwalimu wa You tube.
 
Mwendazake aliongeza shilingi ngapi?Au yeye alikuwa anaishi dunia ipi?Acheni chuki za kijinga.Mama ni bora mara 100 zaidi ya mungu wenu mwendazake

Mwendazake anaingiaje hapa ?
 
Kumkosoa mtu au kutokukubaliana naye katika baadhi ya matendo au maamuzi yake haimaanishi kumchukia.
Huenda kuna tatizo kwenye namna ya kutafsiri neno CHUKI.
Watanzania wengi hatupendi kuambiana ukweli mchungu. Tunapenda kusifian hata panapohitaji kukosoa.

Bila critics za waliotutangulia, dunia isingekuwa hivi ilivyo. Kama tungekubaliana katika kila jambo maendeleo yasingekuwepo.

Wewe tunakujua ni timu kaburi, nenda kazunguke kaburini mara Tano Magufuli ataamka.
 
Kila mtu ana mama yake na hamchukii.

Watu wanachokwazwa nacho ni tabia ya kutokuchukua hatua kwa maswala muhimu ya kitaifa. INACTION.

Na kuufanyia kazi ushauri mbaya wa watu waliomzunguza.

Circle yake ni ya watu ambao historia inatueleza matendo yao yako namna gani.

Hatutaki turudi tulikotoka.

Akitaka abadilike. Asipotaka basi hali itabakia kuwa hiyo hiyo na inaweza kuwa mbaya zaidi.

Maana binadamu huwa wanakuwa na levels za toleraance.
Anachukiwa kwa kukubali ccm ambacho ni chama cha wakulima na wafanyakazi kibinafsishwe na kuwa mali za koo za Kikwete, Makamba, Nauye na Kinana!
Na wanajisifu kuwa wao ndio wenye chama!
 
HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
RAIS wa JMT ni RAIS Hana jinsia,Hana dini. Hana chama, ni RAIS wa wote, Kila kukicha PROPAGANDA!!!!!! tatueni changamoto za wananchi.
 
Rais ameitisha kikao cha dharura usiku huu kwa saa za Bongo ikulu magogoni, tumpe muda baada ya kikao cha dharura anakuja na road map gani.
Kikao Cha nn tena na mlisema raisi hauhisiki na kupanda bei kwa mafuta?
 
Binafsi simlaumu sana mama Samia.
Mama Samia alipendekezwa kuwa mgombea mwenza 2015 nakumbuka hata yeye alishtuka kwa mshangao,lakini ila kama hayakuwa maigizo(kwamba pengine alitonywa mapema).

Hivyo ni wazi hakuwa amejiandaa kwa nafasi hiyo.
Ameshuhudia makamu wa Rais, watatu wamemaliza muda wao na wakapumzika,bila shaka hata yeye atakuwa alifikiria hivyo.

Niseme mama Samia hakuwahi kuwaza atakuwa Rais, pamoja na kuwa kwenye nafasi inayotoa uwezekano huo hata kama ni mdogo Sana.

Rais Kikwete alimpendekeza Dr. Bilali kuwa mgombea mwenza 2010,ili kumsaidia Dr.Shein kwenye uchaguzi wa Zanzibar ambako pia Dr. Bilali alikuwa akigombea nafasi ya urais,na inasemwa alikuwa akiungwa mkono sana na wanec wengi kutoka Zanzibar hivyo kuwa tishio kwa Shein ambaye waafidhina wa ccm walitaka ndiye awe Rais wa Zanzibar, ninaamini hata Kikwete alipompendekeza kuwa makamu wake,alijua ni nafasi isiyokuwa na madhara kabisa. Atakaa tu wakimaliza muda wao wanaondoka.

Sijui kama Rais Kikwete amewahi kujiuliza kuhusu risk aliyoicheza baada ya kutokea kifo cha Magufuli.
Kwamba unamuogopa Bilali kuwa Rais wa Zanzibar kuliko kuwa Rais wa JMT, Ambako atakuwa Amiri Jeshi Mkuu.

Na ndivyo ilivyotokea Sasa, Rais Samia hakuwa mmoja wa waliochukua fomu za kupendekezwa kugombea urais JMT 2015 na inawezekana hakutamani kuwa Rais.

Sasa leo kwa kudra ya Mwenyezi Mungu ni Rais wa JMT,bila kutarajia. Ni kweli kwenye uchaguzi wa 2020 walipigiwa kura wote na Magufuli, lakini pamoja na ukweli kuwa uchaguzi ulivurugwa, bado naamini watu wengi waliopiga kura watakuwa walimpigia Magufuli na Kama wapo waliopiga kwa kuvutiwa Samia watakuwa ni wachache sana.

Samia hakuwa mtu aliyefahamika sana huku bara na waliomfahamu labda kupitia bunge la katiba ambako alikuwa makamu wa mwenyekiti.

Hivyo hakuna aliyefikiri umakamu wake ni nafasi nyeti sana kuwa anaweza kuwa Rais wa JMT na hii bila hata yeye hakuamini kuwa Sasa amekuwa Rais wa JMT.

Hivyo basi mapungufu yanayolalamikiwa kwenye urais siyo sababu yeye eti kuwa ni mwanamke NO. Sababu kubwa naweza kuamini ni anajipanga na kukubali kuwa Rais.

Wapo wanawake waliochukua fomu kugombea urais na wanafahamika kuliko Samia na inawezekana hata kushindwa kwao ni kwa sababu ya kukosa kura nyingi hasa kutoka kwa wanawake wenzao.

Mtoa uzi ameegemea Sana kuwa Samia anakosolewa kutokana na jinsia yake ya kike, siyo kweli. Uingereza imewahi kuwa na waziri mkuu mwanamke,na kwa huku ni sawa na nafasi ya urais, Magreth Thatcher(1979-1990), mwaka 1982 nchi yake iliingia vitani, baada ya Argentina kuvamia visiwa vya Falklands, ambavyo ni sehemu ya uingereza, huyu mama ndiye alianzishiwa jina la iron Lady kwa namna alivyoiongoza uingereza mpaka kushinda vita hivyo. Angalia umbali kutoka Argentina mpaka uingereza, na vile visiwa viko karibu sana na Argentina lakini bado alishinda na kuvikomboa visiwa vile.

Hivyo yeye kuwa mwanamke siyo hoja ya msingi, muhimu sana yeye anaamini kwenye nini.
Magreth Thatcher angeanza kunung'unika kuwa hawa Argentina wanavamia visiwa hivi vya Falklands kwa sababu wameona waziri Mkuu ni mwanamke, bila angeshindwa mapema sana.

Na hii tabia ya kujikinga kwa kutegemea jinsia nimeiona sana kipindi cha Samia, lakini tunasahau Samia hakuwahi kuonyesha nia ya kuutaka urais. Angekuwa Rais ni Dr. Rose Migiro au Amina Salum Ally,tungeshangaa sana,kwani hawa walitamani kuwa marais.

Sasa Samia ni Rais na mtoa uzi umemalizia kwa kusema,mpende msipende. Sidhani kama kuna mtu anabisha kuwa Samia siyo Rais. Samia ni Rais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tu.

Kama ilivyokuwa kwa Magreth Thatcher na
ni makosa makubwa kulazimisha matatizo yaliyoko Rwanda, Kenya lazima na Tanzania yawepo.
Nilienda Rwanda 2011, haya maji ya madogo ya kunywa 500ml. Huku kwetu mikoani tunanunua shs 500/ rejareja kule Ni faranga 400/ sawa ni shs 1,000/ya Tanzania. Kikombe cha kahawa tshs 1,200/ huku haifiki hata mia tano.

Mzazi anayechunguliwa kwa jirani yake ili aone anavyowalea watoto wake ili na yeye amuige namna ya kulea/ kutunza watoto wake hafai hata kidogo.

Unalinganisha bei ya mafuta na Rwanda na kwa nini siyo Zanzibar ambayo wake Rais Mkuu ni wetu pia?

Hakuna anayehangaika na jinsia ya Rais tunachotaka na kutamani tuwe na Rais anayewahurumia na kuwapenda wananchi wake. Na siyo kuiga maisha ya nchi jirani Kama Kenya au Rwanda,raslimali zilizoko Tanzania,ni tofauti kabisa na Kenya au Rwanda.

Ni kweli tuna uhuru wa kuongea tofauti na miaka sita iliyopita,lakini kwa nini tujivunie ujinga? Kwamba mtu kwa makusudi kapiga marufuku tusitumie net za kuzuia mbu wa malaria, ambazo tayari tunazo,halafu huyo kwa sababu anazojua Mungu anamuondoa anaweka mwingine ambaye anatushangaa na kumshangaa aliyetuzuia tusitumie net za mbu,halafu siye tumshangilie na kumsifu huyu aliyeruhusu matumizi ya net kweli!!

Tunamuomba sana Mama Samia akubali na aamini yeye ndiye Rais wa JMT kwa kipindi hiki, yote yanayoikumba Tanzania ni ya kwake na kamwe asidanganywe na wanawake wanaomdanganya kuwa anasemwa au kulalamikiwa kwa sababu ni Rais mwanamke, asimame Kama alivyosimama Magreth Thatcher aonyeshe anaweza katikati ya mashaka mengi kutoka kwa wanaume na wanawake wengi tu. Hata uingereza hawakuamini kuwa Magreth Thatcher angeweza kusimamia na kushinda vita vile.

Wanawake msimdanganye Rais Samia,ili akose kujiamini au apaniki na mwishowe amuige Magufuli ataanguka mapema sana na mtashangaa.
 
Ni chuki tu na masilahi binafsi ya wanazi wa mwendazake.

Magufuli alisemwa sana kwa maovu yake aliyokuwa anawafanyia watanzania. Raisi Samia anarekebisha hali huyo. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia...wanazi wa Magufuli walikuwa wamezoea serikali ya kibabe hawataki Samia aongoze kwa maono yake,wanataka aongoze kqma Magufuli!
Basi mwendazake ana wafuasi wengi sana!
 
Technically Mwendazake anachukiwa na tabaka Tawala yaani elite class ila Samia anapendwa na hilo tabaka..

Mwendazake anapendwa na watu maskini huko waliomuona mtetezi wao licha ya ukweli kwamba hakuna cha maana alichowatetea wala hawakuondokana na umaskini wao,Hawa hawapendi Samia ila ndio wengi.
Kwa hoja yako hii Samia anapendwa na watu wasiozidi 5% hapa nchini
 
HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
Kapimwe haraka
 
Mama hana ujasiri wa kudhibiti wezi, yaani tutapigwa mbele na nyuma. Kama wapigaji ndio wamedhamini tours watajilipa vipi.
Bonde la mchicha tazara ilitakiwa liwe wazi Ili mji upumue limeshachukuliwa na wapigaji, maghorofa ya tazara yashavunjwa ni mayadi tupu. Mjini yadi za nn kwann zisiende Chalinze Ili malori yasije mjini.
 
Anachukiwa kwa kukubali ccm ambacho ni chama c⁷ha wakulima na wafanyakazi kibinafsishwe na kuwa mali za koo za Kikwete, Makamba, Nauye na Kinana!
Na wanajisifu kuwa wao ndio wenye chama!

CCM msingi wake ni kupigania na kuwatetea maslahi ya maskini.

Sasa hivi inatetea maslahi ya mafisadi. Watoto wa viongozi wala rushwa.
 
Sio chuki ni Maoni ya watanzania km ilivyo sku zote na mwisho wa sku 2025 wata vote kwa kishindo
 
mada nzuri ila huku kwetu petrol ni tsh 3,298 kwa lita sio tsh 3,100 kama ulivyosema mkuu. bei ya mwanzo ilikuwa tsh 3,012. ukweli bei mpya imetukera mpaka tumetamani kuhamia Ukraine!
 
Back
Top Bottom