Chuki dhidi ya Rais Samia ni kwasababu ni mwanamke

Wewe muhanga wa tetemeko la ardhi Kagera. Kama unataka kumpamba rais wa sasa, huna haja ya kuanza kumponda aliyepita. Watu wenye tabia hiyo ambayo haikubaliki wana kasumba ya kuendelea kuwa akina kipya kinyemi. Yaani Samia akiondoka, wataanza kumponda. Ni shidaa.
Hakuna cha muhanga,sue wengine huwa tunaenda field kazini,kwa mfano tunazunguka Vijijini kupeleka miradi ya maji Kwa pesa za uviko,sasa huwa tunawauliza wanavijiji kwamba yule mlikuwa mnamuita jembe mbona hatuoni aliwafanyia nini ikiwa sasa ndio mnaona hata Maji?

Watakwambia huyu mama hamna,unashindwa kuelewa gage yao hasa ya uongozi ni nini hupati jibu..

Kumbe unatakiwa usimsaidie maskini, Mwendazake aliwajulia kwa ujinga wao ndio maana alikuwa anawaigizia sijui kula mahindi mara kununua jogoo wanashangilia 😂😂
 
Kumkosoa mtu au kutokukubaliana naye katika baadhi ya matendo au maamuzi yake haimaanishi kumchukia.
Huenda kuna tatizo kwenye namna ya kutafsiri neno CHUKI.
Watanzania wengi hatupendi kuambiana ukweli mchungu. Tunapenda kusifian hata panapohitaji kukosoa.

Bila critics za waliotutangulia, dunia isingekuwa hivi ilivyo. Kama tungekubaliana katika kila jambo maendeleo yasingekuwepo.
 
Hata hivo , Mwanamke hapaswi kua Rais ,,Mwanamke hapaswi kua Waziri wa ULINZI , Tena Kwa nchi kama hiii ilojaa wapigaji ??

Basi, angalau awe ni mwanamke mwenye Akili, Uthubutu,Kujiamin, Mzalendo.

Sasa unakua mwanamke wa mipasho pasho, unafiki mwingi,, mbaya zaidi unakua mwanamke ambaye Hauna akili, Unadanganywa kirahisi, sio mfatiliaji, unacheka chekaaa tuu 'Mimi na macho malegevu lkn yanaona'.

KWA HUYU, TUMEPIGWA...HATA IVO BADO HAITOSHI NA HAMPI SABABU YA KUHALALISHA KUSHINDWA KWAKE NA KUJIFICHA KWENYE KIVULI CHA UANAMKE
Hawatakuelewa
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kila mtu ana mama yake na hamchukii.

Watu wanachokwazwa nacho ni tabia ya kutokuchukua hatua kwa maswala muhimu ya kitaifa. INACTION.

Na kuufanyia kazi ushauri mbaya wa watu waliomzunguza.

Circle yake ni ya watu ambao historia inatueleza matendo yao yako namna gani.

Hatutaki turudi tulikotoka.

Akitaka abadilike. Asipotaka basi hali itabakia kuwa hiyo hiyo na inaweza kuwa mbaya zaidi.

Maana binadamu huwa wanakuwa na levels za toleraance.
Acha kumtisha Rais anafanya vyema
Sio jiwe dictator mpenda Kiki mhuni yule
Mama yuko poa
Kama mwendazake angependa haki mbona hakukemea uhuni wa Sabaya na Makonda
 
HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
Umeongea vizuri, Mama anafanya vizuri na cha muhimu zaidi, anania njema sana kwa wananchi wake
Kama ningepewa nafasi ya kushauri kidogo;
Ningetamani alitazame suala la kodi kuwa nyingi/kubwa kwa wafanya biashara
Nachelea kusema kuwa, kodi zikiwa nyingi/kubwa wafanya biashara hawakui; wanabakia hapo walipo kama sio kushuka na hivyo kukosekana kwa Ajira na mwishowe makusanyo hayatakuwa mazuri. Kodi zikiwa rafiki (bila kulinganisha na nchi zilizoendelea) uchumi utasimama kwa muda ila baadae utakick off na kusonga mbele na hii itafanya tuweze kusimama wenyewe kwa kiasi kikubwa
Natamani tutengeneze kina Bakhreza na kina hayati mzee Mengi wengine ili waajiri watu na kuzalisha ili uchumi ukue
Huo ni mtazamo wangu
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Umeongelea kenya, Uganda, Burundi mbona huongelei bei ya petroli hapo jirani Zanzibar? Ama wao wana visima vya mafut?
Zanzibar sio Tanzania.Zanzibar inahudumia watu 1.5mln na eneo dogo,,Bara watu 60 mln na eneo kubwa..

Kwani bei ya mafuta imeanza leo kuwa chini kuliko Bara ? Kwani hujui miaka yote bidhaa Zanzibar huwa ni chini kuliko Bara?

Tunarudi kule kule,chuki binafsi
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Acha kumtisha Rais anafanya vyema
Sio jiwe dictator mpenda Kiki mhuni yule
Mama yuko poa
Kama mwendazake angependa haki mbona hakukemea uhuni wa Sabaya na Makonda
Yaani mkitaka niichukie hii Nchi ,aje mtu mwehu kama yule Mwendazake.
 
Zanzibar sio Tanzania.Zanzibar inahudumia watu 1.5mln na eneo dogo,,Bara watu 60 mln na eneo kubwa..

Kwani bei ya mafuta imeanza leo kuwa chini kuliko Bara ? Kwani hujui miaka yote bidhaa Zanzibar huwa ni chini kuliko Bara?

Tunarudi kule kule,chuki binafsi
Ukubwa wa nchi, eneo na watu vinahusiana vipi na bei ya bidhaa?

Nimekuliza, Zanzibar wana visima vya mafuta?

Unasema miaksa yote Zanzibar bidhaa ziko chini, wao wanazitoa wapi hizo za bei ya chini ikiwemo mafuta, wanaiba?
 
Unaposema incompetence unatakiwa kuja na vigezo linganishi vinginevyo ni muendelezo wa haters

Dunia nzima nchi zimepandisha Mishahara kujaribu kusaidia wananchi wao kupambana na inflation iliyopo, yeye mguu na njia USA for 2 weeks na watu zaidi ya 100, yuko busy kufungua cinema kwenye nchi ambayo watu wanataabika na wanataka solutions za matatizo yao lkn anazidi kuongeza Gharama serikali kwa safari zisizo na tija, yes ni incompetent!
 
HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
Pumba
 
Dunia nzima nchi zimepandisha Mishahara kujaribu kusaidia wananchi wao kupambana na inflation iliyopo, yeye mguu na njia USA for 2 weeks na watu zaidi ya 100, yuko busy kufungua cinema kwenye nchi ambayo watu wanataabika na wanataka solutions za matatizo yao lkn anazidi kuongeza Gharama serikali kwa safari zisizo na tija, yes ni incompetent!
Nilisema wewe ni mpumbavu na hater utabisha?

Kwa hiyo akipandisha salary ya watumishi 500k ndio itasaidia Watzn 60 mln kupambana na inflation?

Huwa siwezi ku argue na watu wenye akili ndogo kama za funza👇

Screenshot_20220508-180535.png

Screenshot_20220508-180742.png
 
Mleta mada unamaanisha kuwa watanzania hawajui kuwa mafuta yamepanda bei mara mbili yake,vyakula na mahitaji muhimu gharama za maisha zipo juu kuliko kwa mtangulizi wake,mwambieni mama atimize majukumu yaje uone kama kuna kiumbe chochote kitakacho piga domo,ata mbwa hawatabweka.
 
Ukubwa wa nchi, eneo na watu vinahusiana vipi na bei ya bidhaa?

Nimekuliza, Zanzibar wana visima vya mafuta?

Unasema miaksa yote Zanzibar bidhaa ziko chini, wao wanazitoa wapi hizo za bei ya chini ikiwemo mafuta, wanaiba?
Ndio maana nikaanza na kukupa maelezo..

Unajua maana ya Kodi? Unajua hasara ya kuwa na eneo kubwa na watu wengi ilhali una uwezo mdogo kuwahudumia?

Umewahi sikia panya Road Zanzibar? Endeleeni kufyatuana mtalia kila siku na mwishowe mtakuwa kama Ethiopia na Nigeria 👇

Screenshot_20220508-180310.png

Screenshot_20220508-175450.png
 
Mleta mada unamaanisha kuwa watanzania hawajui kuwa mafuta yamepanda bei mara mbili yake,vyakula na mahitaji muhimu gharama za maisha zipo juu kuliko kwa mtangulizi wake,mwambieni mama atimize majukumu yaje uone kama kuna kiumbe chochote kitakacho piga domo,ata mbwa hawatabweka.
Kwani saizi anatimiza majukumu ya nani? Unajua Nchi ina pesa za kugawa au mnaropoka tuu?

Mbona kula Bungeni wabunge wwalishindwa kuja na Suluhu wakaishia kusema serikali serikali ije ije ila hawasemi suluhisho..

Mkicheza vibaya mtakuwa kama Sri Lanka na Zambia afu ndio mtaona moto..

Kamfumuko kaduchu tuu ka bei makelele,Je mngefika hapa ilipo Turkey ingekuaje si mungeenda kuuza Tigo zenu na Figo?👇

Screenshot_20220508-210958.png
 
Tatizo sio Jinsia yake,tatizo la huyu mama kashindwa kutofautisha kwamba yeye alitakiwa kutimiza majukumu ya kijiti alichoaachiwa na JPM,yeye badala yake anapoteza muda kwenye royal tour na kumsimanga marehemu.Lazima tumseme tu
 
Back
Top Bottom