Chuki dhidi ya Rais Samia ni kwasababu ni mwanamke

HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
Kwa hiyo nae anamsema vibaya marehemu kwa sababu ni mwanamme? Mama anaupiga mwingi lakini goli hafungu jombaa
 
Kumsema sio shida ila hamchukii bali anamlaumu kwa kutufikisha hapa 👇

Screenshot_20220503-182121.png
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Tatizo sio Jinsia yake,tatizo la huyu mama kashindwa kutofautisha kwamba yeye alitakiwa kutimiza majukumu ya kijiti alichoaachiwa na JPM,yeye badala yake anapoteza muda kwenye royal tour na kumsimanga marehemu.Lazima tumseme tu
🚮🚮🚮

Screenshot_20220508-180535.png

Screenshot_20220508-180742.png
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hata hivo , Mwanamke hapaswi kua Rais ,,Mwanamke hapaswi kua Waziri wa ULINZI , Tena Kwa nchi kama hiii ilojaa wapigaji ??

Basi, angalau awe ni mwanamke mwenye Akili, Uthubutu,Kujiamin, Mzalendo.

Sasa unakua mwanamke wa mipasho pasho, unafiki mwingi,, mbaya zaidi unakua mwanamke ambaye Hauna akili, Unadanganywa kirahisi, sio mfatiliaji, unacheka chekaaa tuu 'Mimi na macho malegevu lkn yanaona'.

KWA HUYU, TUMEPIGWA...HATA IVO BADO HAITOSHI NA HAMPI SABABU YA KUHALALISHA KUSHINDWA KWAKE NA KUJIFICHA KWENYE KIVULI CHA UANAMKE
Kiongozi shupavu, makini, na mthubutu hajifichi nyuma ya udhaifu wake wowote wa jinsi, umbile, kabila, elimu, nk kwa sababu anaongozwa na kulindwa na Sheria, Kanuni, Taratibu, Mila na Tamaduni.
 
Nilisema wewe ni mpumbavu na hater utabisha?

Kwa hiyo akipandisha salary ya watumishi 500k ndio itasaidia Watzn 60 mln kupambana na inflation?

Huwa siwezi ku argue na watu wenye akili ndogo kama za funza👇

View attachment 2217207

View attachment 2217208

Bado ingeleta tofauti kubwa sana tu wafanyakazi laki 5 wana trickle down effect, isitoshe huko nchi zote Duniani walikopandisha ni wajinga ?

Huyo mtu wako ni incompetent, period!
 
Msitumie karata ya jinsia kuzima hoja za wakosoaji wenu.
 
Kila mtu ana mama yake na hamchukii.

Watu wanachokwazwa nacho ni tabia ya kutokuchukua hatua kwa maswala muhimu ya kitaifa. INACTION.

Na kuufanyia kazi ushauri mbaya wa watu waliomzunguza.

Circle yake ni ya watu ambao historia inatueleza matendo yao yako namna gani.

Hatutaki turudi tulikotoka.

Akitaka abadilike. Asipotaka basi hali itabakia kuwa hiyo hiyo na inaweza kuwa mbaya zaidi.

Maana binadamu huwa wanakuwa na levels za toleraance.
Sukuma gang naona unapata tabu ile mbaya, naona unataka kumaanisha Magufuli alikuwa mtu sahihi na alioongoza vizuri, hivyo huyu mama aongoze kama dhalimu. Futa kichwani kwako, huyu mama tunamkosoa kwa mapungufu yake na hatujali uanamke wake. Ila kama ni kipimo uongozi yeye na Magufuli, yeye ana afadhali kuliko Magufuli japo sio kwa ubora fullstop
 
Hata hivo , Mwanamke hapaswi kua Rais ,,Mwanamke hapaswi kua Waziri wa ULINZI , Tena Kwa nchi kama hiii ilojaa wapigaji ??

Basi, angalau awe ni mwanamke mwenye Akili, Uthubutu,Kujiamin, Mzalendo.

Sasa unakua mwanamke wa mipasho pasho, unafiki mwingi,, mbaya zaidi unakua mwanamke ambaye Hauna akili, Unadanganywa kirahisi, sio mfatiliaji, unacheka chekaaa tuu 'Mimi na macho malegevu lkn yanaona'.

KWA HUYU, TUMEPIGWA...HATA IVO BADO HAITOSHI NA HAMPI SABABU YA KUHALALISHA KUSHINDWA KWAKE NA KUJIFICHA KWENYE KIVULI CHA UANAMKE
Hizi sasa ndio chuki zenye viwango vya juu toka kwa pu.ng.uani linaloishi kwa shemej
 
Bado ingeleta tofauti kubwa sana tu wafanyakazi laki 5 wana trickle down effect, isitoshe huko nchi zote Duniani walikopandisha ni wajinga ?

Huyo mtu wako ni incompetent, period!
Kwani Rais alisema haongezi salary? Mwehu wenu yule kwa miaka 6 aliongeza bei gani?
 
Acha kumtisha Rais anafanya vyema
Sio jiwe dictator mpenda Kiki mhuni yule
Mama yuko poa
Kama mwendazake angependa haki mbona hakukemea uhuni wa Sabaya na Makonda

Usilazimishe watu kuwa kuna mambo mazuri yanafanyika maana zinatumika nguvu kubwa sana tuamini hivyo , acha watu wayaone wenyewe.

Wakati Inactions and errors are everywhere.
 
Nani anatumia nguvu kuaminisha watu? Ingekuwa hivyo si ungeona Samia kateka vyombo vya habari kulazimisha kuongea mambo ya serikali tuu kama Mwendazake wenu..

Si ungeona anadharirisha viongozi wenzake Ili kulazimisha kumsifu kama Mwendazake?

Samia sio mshamba wa uongozi hana ujinga huo amekuwa vp na Sasa Waziri,amekuwa serikalini kabla hata ya Mwendazake kuzimu kwa hiyo hana cha kulimbuka wala kufanya maigizo .
 
  • Thanks
Reactions: Tui
HAPO zamani kidogo, Tanzania palikuwa kimya. Ukithubutu kusema unatishiwa kutekwa. Unapotezwa.

Haikuwa vitisho vya uongo. Watu walitekwa na kupotezwa. Machi 19, 2021, taifa likajipatia rais mpya. Samia Suluhu Hassan. Mwanamke mstaarabu. Muungwana.

Mama Samia. Hivyo ndivyo Watanzania wanapenda kumwita. Ameruhusu watu waongee. Nchi huru kabisa. Haki inazingatiwa. Watu wanaongea jamani. Mashallah!

Katika taifa huru, wapo huufanyia dhuluma uhuru wao. Hufanya uhalifu wa uporaji na hata kuingilia uhuru wa wenzao.

Naam, wapo huamua kutekenya mahala ili matokeo yaumize wengi. Si ni sawa na aliyepiga jiwe mzinga wa nyuki, akasababisha wanakijiji waote nundu za kichwa?

Mahali fulani Tanzania leo, yupo anaona wivu kwa nini Watanzania wana furaha na amani leo. Anamsema Samia kwa lugha ya kuudhi, kusudi akasirike awe kama mtangulizi wake. Turudi kule kwa kutekana na kukosa uhuru wa kuongea.

Rais Samia ameikuta nchi inavuja damu. Fedha hakuna. Wizi mkubwa ulikuwa umeshamiri. Unyang'anyi wa mali za watu binafsi kwa kutumia dola.

Nani hajui kama wenye maduka ya kubadilishia fedha walidhulumiwa mitaji na uwekezaji wao wote? Biashara ziliingia wadudu. Uchumi ukawa taabani.

Misingi mizuri ambayo Rais Samia anaiweka, inairudisha nchi kwenye njia nzuri ya ustawi wa kiuchumi. Kama unajua jua zaidi; Rais Samia ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu. Anajua anachokifanya.

Hakuna mtu ambaye hajui hali ya uchumi ni mbaya ulimwenguni. Kila kona ya dunia ni vilio. Anzia Ulaya, Marekani mpaka Urusi palipo na kiini cha matatizo.

Tanzania kweli vilio vipo. Shida inayokuja ni kelele nyingi kuliko kujadili hali halisi.

Nani anajua kuwa Afrika Mashariki yote, ni Tanzania na Uganda hivi sasa ndizo zenye unafuu wa mfumuko wa bei?

Tanzania mfumuko wa bei ni asilimia 3.8, Uganda 3.2. Ukigusa Kenya ni asilimi 6.29, Rwanda 4.2, Burundi 13%, Sudan Kusini 25%, wageni wetu DRC wao ni 5%. Hizi taarifa Watanzania hawaambiwi.

Lisilofichika ni kwamba Watanzania wengi wanaingizwa kwenye mkumbo wa kulalamika. Hawaambiwi ukweli.

Kwamba katika nchi za Mashariki, Tanzania ndio inaongoza kwa bei ndogo ya mafuta.

Rwanda leo, petroli wananunua lita moja kwa Rwandan Franc 1,893. Fedha hiyo ni Shilingi ya Tanzania 4,320.

Mtanzania ananunua petroli leo kwa Shilingi 3,100. Jirani yake Kenya anauziwa lita moja kwa Shilingi ya Kenya 215. Hiyo ni 4,300 kwa Shilingi ya Tanzania.

Mganda akitaka petroli leo ananunua lita moja kwa Shilingi ya Uganda 5,263, kwa chenji ya noti za BOT ni 3,438.

Isinukuliwe kuwa ni sherehe na nderemo petroli kuuzwa Shilingi 3,100 kisa bei ni nafuu kuliko nchi zote jirani. Usahihi wa hoja ni kuwa manung'uniko yatoke kwa haki. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Mshangao sasa, kuna wanung'unikaji hata hawajui mzunguko wa nchi unavyokwenda. Au wanajua, ila ndio wale wagonjwa kunaosaka umaarufu mitandaoni. Wao bora waongee chochote waonekane. Basi tu waonekane.

Vuta picha, Serikali inasimamiwa na Bunge. Na tayari Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi kimeshaitaka Serikali iwasilishe majibu Jumanne (Mei 10), kuhusu hali ya kupanda kwa bei.

Nani anajua Serikali itaibuka na mpango gani wa kushusha bei hiyo Jumanne? Kwa nini watu wasisubiri hii mechi ya Bunge na Serikali halafu mjadala uje kwenye matokeo?

Basi bwana, Rais Samia kawa hana jema kwa kila analofanya. Hata kujitolea kwake kuwa mhusika mkuu wa filamu maalum ya “Tanzania; The Royal Tour”, nako kunabagazwa!

Royal Tour ni tangazo kubwa zaidi la vivutio vya utalii ambalo Tanzania imewahi kufanya.

Mbeba wazo na mtayarishaji mkuu ni Peter Greenberg. Rais Samia kwa kuona ni kitu chenye manufaa kwa nchi, amekipokea. Akakubali kushiriki makala ya kihistoria kutangaza vivutio vya utalii.

Kuna watu wenye ubongo wa ‘mtumba', wanasema eti watalii si huwa wanakuja bila filamu ya Royal Tour? Kwa hiyo, Rais Samia katenda jinai kufanya jambo la kuongeza watalii.

Yapo mataifa yanastawi kiuchumi na yanakua kwa kasi kimaendeleo kwa sababu ya utalii. Unathubutu vipi kumbeza Rais Samia kuhamasisha utalii ili kuzingenezea njia fedha za kigeni zije nchini na kukuza uchumi?

Tunajua na umma wa Watanzania kwa sehemu kubwa unafahamu kuwa Rais Samia anapigwa vita kubwa kwa sababu ni mwanamke. Hata atende jema lipi, chuki za watu kwa rais mwanamke zitaendelea kutokeza.

Ni kama Rais Samia anaendesha basi, halafu kila abiria anajiona ni dereva, kwa hiyo anakosoa bila hata adabu.

Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uwe hutaki mwanamke awe Rais au huupendi Uzanzibari wake. Ni Rais wa Tanzania.

JORDAN MASANJA
Mwathirika wa Tetemeko Kagera.
Uwe unaacha upumbavu, Kenya mafuta ni 2880. Mpumbavu mkubwa
 
Ni chuki tu na masilahi binafsi ya wanazi wa mwendazake.

Magufuli alisemwa sana kwa maovu yake aliyokuwa anawafanyia watanzania. Raisi Samia anarekebisha hali huyo. Na hapo ndipo tatizo linapoanzia...wanazi wa Magufuli walikuwa wamezoea serikali ya kibabe hawataki Samia aongoze kwa maono yake,wanataka aongoze kqma Magufuli!
Hebu sema ambapo Samia anarekebisha
 
Umeongelea kenya, Uganda, Burundi mbona huongelei bei ya petroli hapo jirani Zanzibar? Ama wao wana visima vya mafut?
Na Ni muongo huyo, Kenya na Burundi mafuta ni rahisi kuliko hapa. Tumewazidi Uganda tu
 
Umeongea vizuri, Mama anafanya vizuri na cha muhimu zaidi, anania njema sana kwa wananchi wake
Kama ningepewa nafasi ya kushauri kidogo;
Ningetamani alitazame suala la kodi kuwa nyingi/kubwa kwa wafanya biashara
Nachelea kusema kuwa, kodi zikiwa nyingi/kubwa wafanya biashara hawakui; wanabakia hapo walipo kama sio kushuka na hivyo kukosekana kwa Ajira na mwishowe makusanyo hayatakuwa mazuri. Kodi zikiwa rafiki (bila kulinganisha na nchi zilizoendelea) uchumi utasimama kwa muda ila baadae utakick off. Natamani tutengeneze kina Bakhreza na kina hayati mzee Mengi wengine ili waajiri watu na kuzalisha ili uchumi ukue
Huo ni mtazamo wangu
Hiyo nia njema haipo
 
Back
Top Bottom