Chris Lukosi katoa ushauri mzuri jinsi TRA wanavyokosa mapato

Mkuu tuseme umeagiza gari jipya la thamani ya milion 60 tzs ushuru wake utakuwa shilling ngapi?
inategemea na aina ya gari, kama ni private au commercial, private mara nyingi inakuwa juu kwenye kodi kuliko commercial, japo kwenye commercial pia kuna configuration inakuwa nafuu
volvo used trucks ya mwaka 2001 kwa mfano, ikiwa tractor unit 4x2 kodi ni ml 13, ikiwa 6x2 ni mil kama mil 17 , ila Volvo hiyo hiyo ya mwaka huo huo ikiwa rigid , kodi ni kama mil 38.
 

Chris Lukosi ni mpuuzi ,enzi za JIWE alikuwa anasifia tu muda wote ,aache unafiki angeshauri kipindi kile cha JIWE apunguze kodi sio awamu hii ndio anajifanya kuleta unafiki wake ,Aendelee kula chips na Chilisosi aliyoletewa na wanawe.
 
Wakishusha kodi watu wa nchi jirani watafuata magari hapa Bongo. Yard zitaibuka kotekote mipakani na kujuza uchumi. TRA bado wanafikiri kijamaa kuwa gari ni anasa.
 
Nasikia klm anafanya modification hapo hapo Dar ili kupunguza kibano cha import duty.
 
Shida ya hii nchi Magari yanaonekana kama kitu cha anasa na sio kitu muhimu..ila baskeli na pikipiki sio anasa ila nikitu cha lazama..
Nenda Zanzibar watu wanaendesha magari mpya bado sababu ya ushuru kuwa mdogo.. gari unanunua laki 7 Zanzibar na bado linatembea..
Umaskini mwingine huwa ni wakujitakia wenyewe.Wenye madaraka wanaona fahari kuendelea kunyenyekewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…