Chonde chonde kwa wanaotarajia kufunga ndoa

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,400
Naomba kutoa ushauri wa bure kwa wale wanaotarajia kufunga ndoa hivi karibuni,
Kama ni mwanaume mwenzangu jaribu kupunguza matumizi kwa ajiri ya maandalizi ya harusi..vijana wengi wanaingia kwenye mtego wa kukopa kwenye sehemu zao za kazi,mabank,vyama n.k kwa ajiri ya kufanikisha sherehe ya masaa yasiyozidi 6 yaani kwa usiku mmoja.

NDoa si sherehe,ndoa ni pale mnapobaki wawili wewe na mkeo hapo ndipo tunapoita ndoa..Wanaume wengi wameingia katika mtego wa kushawishika kutaka kufanya sherehe kubwa ili kuonyesha ufahari juu ya mwenzake au wafanyakazi wenzake au jamaa zake au marafiki zake n.k kisha baada ya hapo hubaki akiumia na deni kubwa alilokopa kwa ajili ya kufanikisha harusi ambalo atataabika nalo kati ya kipindi cha miezi 6 hadi miaka 3 na hii itaonyesha ugumu wa maisha kwa mda mfupi kwa yule ampendaye mkewe..kuanza kuishi maisha ya kujibana badala ya kuanza na maisha ya kufurahiana

Inakuwaje kijana unaingia harusi ya gharama hata kimsingi cha vyumba vitatu hauna..haiingii akilini unakopa kwa ajili ya usiku mmoja watu wale na kusaza badala ya kukopa uweke kibanda ambapo utalala na yule umpendaye hadi maisha yenu ya uzeeni?mwingine hata kiwanja hana,mwingine ndiyo hivyo nikupanga tu..

Ushauri:

Jitahidi kujibana kifedha na fanya sherehe ndogo sana kuliangana na uwezo wako wa kiuchumi

Achana na vitu au gharama zisizokuwa na umuhimu kwako kwa ajili ya siku hiyo..kama kukodi gari la gharama kubwa,ukumbi wa kifahari n.k

Washirikishe jamaa zako,marafiki zako au ndugu zako wakupe support ya kimwazo au kifedha

Kaa na zungumza na rafiki yako wa jamaa yako wa karibu aliyefunga ndoa siku si nyingi uone namna gani atakavyokushauri kupunguza gharama au kuepuka matatizo yaliyojitokeza kipindi cha sherehe yake

Kubari ushauri kutoka kwa best man wako

ANGALIZO

Mara zote harusi haikosekani mapungufu hata siku moja..kubali kile kilikwisha tokea.

NDOA ni nyinyi wawili baada ya kutoka kwenye sherehe usiku ule wa kwanza..mnapobaki nyinyi wawili ndipo tutapohita ndoa..

KW ushauri mwingine AFYA,MAHUSIANO NA NDOA unaweza kuinbox lakini ni kwa WANAUME TU
 
Ushauri mzuri, ila ngoja nimzuie bwana harusi to be asiingie humu, asijekuuona bure!!! Acha anispoil na GRAND WEDDING sababu ndoa zilivo za kichina saaivi kitu cha furaha unachobaki nacho ni PICHA ZA HARUSI TU!!! jinsi ulivotokelezea na shela la kufunga mtaa, kiatu cha bei na jigauni la kuwaziba mademu wote wa zamani wa bwana harusi midomo, kimoyomoyo ukisema shamba liliwashinda, nalilima mwenyewe sasa!
 
ushauri mzuri sana mkuu.....tatizo ni kwamba sometimes wao hawataki but watu wanaowazunguka ndo washawishi wakubwa....wakina dada pia...utasikia me nataka harusi kama ya fulani...
 
usiseme kwa nguvu kuna harusi ya mil 12 natarajia kwenda soon, bwana harusi asije kupita humu akaghairi bure......

Ila mnaotarajia kuoa msikie maneno haya....

Na wanawake pia mzingatie haya sio kufanya vyombo pati, kichen pati, sendoff pati aiiiiiii hizo hela heri ukafungue saluni upate hela
 
if there was one thing I'd love to stop are these glamorous wedings wakati mioyoni mwetu tunanungúnika kwa michango. Hivi wewe unajua uwezo wako wa sherehe ni wa kawaida, what sense does it make to plan for a 20 M wedding ? kwa nini usifanye evening dinner hapo home kwenu mambo yakaisha? I see all these weddings kama ni show off, trying to carry a 12M wedding at the expense of other people's pockets. Tena siku hizi kwenye vikao nasikia wanapanga ahh fulani ana kazi nzuri andika laki nne- kisha wanapiga simu Mzee unapledge ngapi? ukisema elfu kumu eeeehhh everbody gets sad (as if they deserve access to your pocket). Omba mchango wa shule au matibabu uone ndio utajua priority zetu
 
Utasababisha watu wakose ajira
-wapiga tarumbeta
-wakodisha vifaa vya harusi
-wapambaji na kadhalika
 
Naomba kutoa ushauri wa bure kwa wale wanaotarajia kufunga ndoa hivi karibuni,
Kama ni mwanaume mwenzangu jaribu kupunguza matumizi kwa ajiri ya maandalizi ya harusi..vijana wengi wanaingia kwenye mtego wa kukopa kwenye sehemu zao za kazi,mabank,vyama n.k kwa ajiri ya kufanikisha sherehe ya masaa yasiyozidi 6 yaani kwa usiku mmoja.

NDoa si sherehe,ndoa ni pale mnapobaki wawili wewe na mkeo hapo ndipo tunapoita ndoa..Wanaume wengi wameingia katika mtego wa kushawishika kutaka kufanya sherehe kubwa ili kuonyesha ufahari juu ya mwenzake au wafanyakazi wenzake au jamaa zake au marafiki zake n.k kisha baada ya hapo hubaki akiumia na deni kubwa alilokopa kwa ajili ya kufanikisha harusi ambalo atataabika nalo kati ya kipindi cha miezi 6 hadi miaka 3 na hii itaonyesha ugumu wa maisha kwa mda mfupi kwa yule ampendaye mkewe..kuanza kuishi maisha ya kujibana badala ya kuanza na maisha ya kufurahiana

Inakuwaje kijana unaingia harusi ya gharama hata kimsingi cha vyumba vitatu hauna..haiingii akilini unakopa kwa ajili ya usiku mmoja watu wale na kusaza badala ya kukopa uweke kibanda ambapo utalala na yule umpendaye hadi maisha yenu ya uzeeni?mwingine hata kiwanja hana,mwingine ndiyo hivyo nikupanga tu..

Ushauri:

Jitahidi kujibana kifedha na fanya sherehe ndogo sana kuliangana na uwezo wako wa kiuchumi

Achana na vitu au gharama zisizokuwa na umuhimu kwako kwa ajili ya siku hiyo..kama kukodi gari la gharama kubwa,ukumbi wa kifahari n.k

Washirikishe jamaa zako,marafiki zako au ndugu zako wakupe support ya kimwazo au kifedha

Kaa na zungumza na rafiki yako wa jamaa yako wa karibu aliyefunga ndoa siku si nyingi uone namna gani atakavyokushauri kupunguza gharama au kuepuka matatizo yaliyojitokeza kipindi cha sherehe yake

Kubari ushauri kutoka kwa best man wako

ANGALIZO

Mara zote harusi haikosekani mapungufu hata siku moja..kubali kile kilikwisha tokea.

NDOA ni nyinyi wawili baada ya kutoka kwenye sherehe usiku ule wa kwanza..mnapobaki nyinyi wawili ndipo tutapohita ndoa..

KW ushauri mwingine AFYA,MAHUSIANO NA NDOA unaweza kuinbox lakini ni kwa WANAUME TU

Mkuu ungetusimulia ili kutupa mwanga zaidi wewe ulitumia gharama gani katika harusi yako na harusi isizidi kiasi gani na kiasi gani kinatosha
 
Mkuu umenigusa, naumiza kichwa haswaaa!

Huko kwenye makanisa kwa Kakobe na Kule kwa Mwingira wanafungisha ndoa 100 kwa wakati mmoja hakuna kikao wala matatizo yoyote ili mradi makubaliano na umpendaye tu sherehe mbele kwa mbele
 
Am tryng kum-convince my wife tto be to do away with kitchen party maana naiona usanii mtupu n a waste of money.
Thank God we both agree on a middle size wedding ceremony.
 
Hizo ni changamoto za kazi itapelekea kuzaa wazo lingine zuri la kuanzisha shughuli nyingine kwani sifa ya mjasiamari kubadilika kama kinyonga kwa kuwa mbunifu wa kufanya biashara tofauti tofauti
 
Ushairi mzuri sana! Lakini harusi za siku hizi niza kufata mkumbo!

Wengine baada ya harusi wana kosa chakula ndani!
 
ushauri mzuri sana
mkuu.....tatizo ni kwamba sometimes wao hawataki but watu wanaowazunguka
ndo washawishi wakubwa....wakina dada pia...utasikia me nataka harusi
kama ya fulani...

uzoefu wangu ni kuwa gharama za sherehe za harusi huchangwa na wanajamii. bw. harusi anaweza asitoe hata senti!
 
nani yupo tayari twende kwa mchungaji mimi,yeye, wasimamizi na wazazî? hata harusi sihitaji. . . SERIOUS!!!!!!
 
Mkuu umenigusa, naumiza kichwa haswaaa!

Kichwa kisikuume,harusi haifanywi na bwana harusi bali wadau watakaoudhulia hiyo shughuli.Tafuta michango kadri uwezavyo,watakaokuchangia hadi dakika ya mwisho fanya nao sherehe hao,hata kama mtakua watu 10.
 
Back
Top Bottom