"Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkaanani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi" (Kutoka 3:7,8).
Hata Wana wa Israeli wakati wanakombolewa toka Misri, wapo waliopinga kukombolewa na kusema wameridhika na maisha wanayoishi wakiwa Misri, ila Musa hakukata tamaa aliendelea kuwahimiza kwamba wanapaswa kuondoka Misri.
Na walipoanza safari ya kuondoka Misri, walipofika bahari ya shamu waliogopa sana,
ndipo wana wa Israeli wakamgeukia Musa ?Je kwa sababu hapakuwa na makaburi katika nchi
ya Misri umetutoa huko ili tufe jangwani?? (mstari.11).
Lakini Mungu alikuwa anajua nini kitatokea, alikuwa anawapima ili kuwafundisha waweze kumtumainia yeye,
Musa akawaambia watu ?Msiogope, simameni tu mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo?BWANA
atawapigania,nanyi mtanyamaza kimya? (Kutoka14:13,14)
Hivyo nasi ktk vita hii ya kutafuta ukombozi halisi wa taifa hili tunapaswa kuondoa Woga, ingawa tunajua ktk process hii wapo watakao kufa ila ni bora tufe wachache kama sadaka ili watakao baki waishi maisha ya raha siku zote.