Choma meli zako zote

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Mwaka 1519 Kamanda mmoja wa kikosi cha Kihispania aliyeitwa Hernan Cortes alienda kukivamia kisiwa cha Veracruz cha nchini Mexico.

Alipowasili ufukweni aliamuru askari wote 600 na mabaharia wote washuke kisha akaagiza meli zote 11 zichomwe moto.

Kisha akawauliza askari wake, "mnaona nini baharini?"
Wakajibu"tunaona meli zetu zikiungua moto".

Akawaambia safi sana hii inamaanisha hatuna uchaguzi hapa. Ni ama tushinde vita au tuuawe lakini hakuna njia ya kukimbia.

Kilichotokea ni kwamba walishinda vita japo walikuwa wachache.

Somo la kujifunza.

1: Mara nyingi ni rahisi kuacha kufanya jambo kama kuna mbadala. Hakikisha unaweka umakini wako kwenye jambo moja tu hadi ufike nalo mwisho.

2: Jiulize ni meli gani katika maisha yako unazotakiwa kuzichoma kuanzia Leo ili ufikie mafanikio yako.

Je ni ajira uliyo nayo kwa sasa?

Je ni mahusiano uliyonayo?

Je ni marafiki wako wa sasa?

Pengine ni biashara uliyonayo?

Au ni kuchati sana kwenye mitandao ya kijamii?

Hizo ni baadhi ya meli unazoweza kuzichoma.

3: Fanya maamuzi kuwa hutarudi nyuma hadi umetimiza lengo lako. Wakati mwingine utalazimika kuacha vitu unavyovipenda, kubadili mtindo wa maisha na kutafuta maarifa yanayoendana na kule unakotaka kufika.

Kumbuka Choma meli zako zote"

The best way to learn is to lean from the best"

Credit: Mwalimu Samwiterson
 
Burn Your Boats - the Secret to Success - Ignore Limits
soma hapo Uone uongo wako na kuurekebisha
 
Back
Top Bottom