Jussa: Rais katoka Zanzibar imekuwa nongwa, Rais alipokuwa wa kwao hawakuona Tanganyika imeuliwa

Jussa: Rais katoka Zanzibar imekuwa nongwa, Rais alipokuwa wa kwao hawakuona Tanganyika imeuliwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,351
Reaction score
18,605
Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Ismail Jussa, amewashukia baadhi ya wanasiasa wanaokosoa mfumo wa Muungano na uwepo wa Rais kutoka Zanzibar, akisema wameanza kukumbuka "Utanganyika" wao kutokana na chuki binafsi dhidi ya viongozi waliopo badala ya kusimama kwenye misingi ya kisheria na kikatiba.

Soma Pia: Jussa: Kuna watu wamejimilikisha ajenda ya mabadiliko wanataka tuwafuate

Akizungumza leo Agosti 29, 2026, katika Ukumbi wa Majid Hall, Mjini Magharibi Unguja wakati wa ziara ya chama hicho, Jussa amebainisha kuwa viongozi hao hawakuwahi kuona tatizo wakati marais waliopita walipokuwa wanatoka upande wa Bara, lakini sasa imekuwa fujo baada ya fursa hiyo kushikwa na kiongozi kutoka Zanzibar.

"Alivyokuwa Rais wa kwao hawakuona Tanganyika imeuliwa, leo Rais katoka Zanzibar imekuwa nongwa"

 
Ismail Jussa, Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo Jussa alikuwa akizungumza leo Agosti 29, 2026, katika ziara ya chama hicho, katika ukumbi wa Majid Hall, Mjini Magharibi, Unguja.

"Alivyokuwa Rais wa kwao hawakuona Tanganyika imeuliwa, leo Rais katoka Zanzibar imekuwa nongwa"

Hizo taarabu zimekaa mahali pake
 
Sisi wabara ni wajinga sana na ndio maama wanatoa kauli za aina hii
Mimi naomba tu tutawaliwe na wazanzibar hadi kiyama. waTanganyika hawajui wanachokitaka na wala hawana habari na Tanganyika. Wao wape vijihela kidogo basi wako tayari kuuza na infact wameshauza uhuru wao.
waZanzibar tangu mwanzo wanaipigania nchi yao, na ikija maslahi ya taifa lao wanasimama imara kama wamoja. They are not ready to compromise. Sisi huku Tanganyika mpinzani akisema utanganyika hadi watanganyika wenzake wanamuwinda kumuua kisa aliyesema hivyo ni CHADEMA.
 
Back
Top Bottom