Chinga ONE-Asili Inayopotea

Chinga ONE-Asili Inayopotea

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
IMGS1001.JPG
 
Ilikuwa na sababu, sababu hiyo haipo tena hivyo lazima ipotee. Historia inaonyesha wamakonde walikuwa wanajichanja na kuweka ndonya ili wawe wabaya (ugly) maana wazungu walipenda watumwa wanaovutia hivyo hiyo ilikuwa mbinu yao kujiokoa.
 
asante sana kwa ujumbe huu
 
Ilikuwa na sababu, sababu hiyo haipo tena hivyo lazima ipotee. Historia inaonyesha wamakonde walikuwa wanajichanja na kuweka ndonya ili wawe wabaya (ugly) maana wazungu walipenda watumwa wanaovutia hivyo hiyo ilikuwa mbinu yao kujiokoa.
picha hii imepigwa jana wakati wa ziara ya waziri mkuu jimboni kwake
 
Sawa kabisa-ilikuwa kujiokoa na mwarabu asiwachukue utumwa kwa vile mtumwa akiuzwa sokoni akipakwa mafuta ili ngozi yake ipendeze. Hawa wakaamua kujichanja. Kipo Kitabu cha zamani kiitwacho-"Chale za Kimakonde". Ikabakia hawa kuwa walinzi majumbani kwani wakali ikawa ndio kazi yao kuu hadi baada ya ukoloni lakini ulinzi sasa zaidi ni wamasai. Hata meno yao wanaume wakiyachonga kuwa kama msumeno wanawake ndio ndonya. Pamoja na kuonekana wachafu kwa rangi na ndonya-hawa wamakonde ni wasafi sana kimazingira, vyombo vyao mama anasugua na kinakuwa cheupe sana hata masufuria. Pia, wanaheshimu sana wanawake ni matrilineal wanaridhi kwa mama. Mwanamke anamiliki mali na anaheshimiwa hapigwi hovyo na kuaibishwa hadharani. Nimesoma Mtwara, nimefanya kazi za seeikali za miradi na JTK Nachingwea siongei la kuambiwa. Kuna watu wa Amazon hufanya hivi kupichora, nyonya domo kubwa linavutwa na mkuu wa koo au mganga huweka dawa zake domoni, hawavai nguo bali kumfunga mjamaa kinamna kiunoni. Vitabu na picha zaoi vipo nami nilipata kuwaona huko Brazil. Duniani kuna mambo. Unakuja kuona culture bara fulani inafanana na hiyo Bara la mbali kabisa. Mungu atusaidie.
Ilikuwa na sababu, sababu hiyo haipo tena hivyo lazima ipotee. Historia inaonyesha wamakonde walikuwa wanajichanja na kuweka ndonya ili wawe wabaya (ugly) maana wazungu walipenda watumwa wanaovutia hivyo hiyo ilikuwa mbinu yao kujiokoa.
 
kuna tamaduni tutzilumbuka sana sidhani hata watoto wa sasa wa kichinga wanaijua hii
 
Nadhani itakuwa ngumu kwa sasa kujaribu kutunza huu utamaduni maana utandawazi umetuvamia kwa kasi Na vijana waliopo hawataki kuwa kama wazazi wao.
lol kazi ipo
 
Bora walivyoacha,
Si vzr kwa binaadamu kujiharibu kwa makusudi ili utishe au uonekane mbaya,
Ndio mana zamani walikua wanasema wamakonde wanakula nyama za watu,

Kutokana na muonekano wao wa kutisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom