Jitu la kienyeji
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,426
- 7,942
Karne ya 13, Ulaya ilishuhudia moja ya maamuzi ya kijinga na ya kikatili zaidi kuwahi kufanywa na kiongozi mkuu wa dini uamuzi uliokuja kuligharimu bara hilo zima mamilioni ya maisha ya watu na karibu kulifuta kwenye ramani ya dunia!
Mnamo mwaka 1233 AD, Papa Gregory IX alitoa waraka rasmi wa Kipapa ulioitwa "Vox in Rama". Ndani ya waraka huo, alitangaza rasmi kuwa paka weusi ni vyombo vya Shetani na mawakala wa wachawi, akidai kuwa walikuwa wakitumika kwenye ibada za siri za giza.
Hofu na ushirikina ulipotanda kwa kasi, wananchi kote barani Ulaya walianza msako mkali wa kuwaua paka bila huruma, haijalishi mweusi wala mwekundu wala wa kijani. Paka walisakwa na kuangamizwa kote barani ulaya, na waliobaki basi ilikua Rehema ya MUNGU tu. Ndani ya miaka michache tu, mitaa ya Ulaya ikabaki haina hata paka mmoja. Watu waliamini wamesafisha jamii yao na kumshinda shetani.
Lakini hawakujua walikuwa wanachimba kaburi lao wenyewe.
Asili haidanganywi wala haisamehe upumbavu. Miongo michache baadaye, katikati ya karne ya 14, ugonjwa wa kutisha wa Tauni (The Black Death) uliipiga Ulaya kama dhoruba ya moto. Ugonjwa huo ulikuwa ukienezwa na viroboto waliokaa kwenye miili ya panya.
Kwa sababu wanadamu walikuwa wamewaua walinzi wao wa asili—paka—idadi ya panya ililipuka na kuongezeka kwa kasi ya ajabu mitaani bila kizuizi chochote. Walitawala nyumba, chakula, na mitaa.
Matokeo yake? Zaidi ya theluthi moja ya watu wote barani Uropa watu kati ya milioni 25 hadi 50—walifariki dunia kwa mateso ya kutisha mno!
Hiyo ndiyo ilikuwa gharama ya vita ya kijinga dhidi ya asili. Wakati mwanadamu anapoingilia mizani ya ulimwengu kwa ajili ya hofu na ushirikina, asili hairudishi nyuma kwa maneno—hulipa kisasi kwa moto.