China yanyonga hadharani wanasiasa 26

China yanyonga hadharani wanasiasa 26

Mataifa yote yasiyo na Democratisia raia wake huwa ni wakatili sana na hawana utu,sababu hawajafundishwa misingi ya utu na Upendo wa kuwathamini wengine. Angalia waarabu na wachina hawaachani tabia za ukatili.Kwa Asia angalau wajapani na Wakorea kusini ndo angalau wako civilized wanao utu

Marekani, uingereza n.k unawazungumziaje??? Maana hao ndio makatili sana na wauwaji namba moja duniani na kama utawatetea basi hizo ni chuki zako binafsi.
 
30714130_2108021735881122_8507926270831998773_n.jpg

China yanyonga hadharani wanasiasa 26 ambao ni wabadhilifu wa Mali za umma (Mafisadi).

Mafisadi hao walihukumiwa kifo cha kupigwa risasi uwanjani hadharani watu wakishuhudia baada ya kubainika kupora Mali ya umma. Inadaiwa kuwa yumo bilionare namba saba wa China.

Hii inawafaa wa hapa kwetu...hasa hasa wenye MAGWANDA YA KIJANI
 
Huo ndio uongozi kwa hakika yaani mtubukipendekezwa kiwa kiongozi unalia na kusaga meno daadeki sio huku wanagombania space za ubunge mpaka yanalogana

Tena yanalogana sana tu mkuu 😀😀😀😀😀 yanakimbilia dunia while maisha yenyewe mafupi.
 
Nchi za wengine wanajitaid sana kupigana na ufisadi,

Swali la kujiuliza ni je kwanini tanzania ufisadi tunaunga mkono?
 
Kwa kifupi, nchi inayotekeleza adhabu ya kifo hadharani bado haijaingia kwenye jamii ya wastaarabu. Utajiri si kitu mbele ya kukosa ustaarabu. Inaniwia taabu sana kuamini kuwa China ya leo hii inaweza kuendekeza mfumo wa kishenzi kiasi hicho. Walioendelea zaidi, hiyo adhabu yenyewe walishaiondoa kwenye msamiati wao. Na haijawahi kuwa suluhisho ukiachilia mbali unafiki unaoambatana na utekelezaji wake.
Kwani sheria ya kusema fisadi asiuwawe katunga nani kwenye hizo nchi ambazo ww unaziiita civilized na kinyume chake kwenye hizo nchi unazoziita non civilized? Kwani si watu hao hao kwa my oppinion naona china ndiyo maaana imepanda uchumi kwa kasi sana kwa kuwa wao wana uongozi thabiti marekani ya leo imechukua miaka takribani 300 kuwa hivi ilivyo na hapo bado mpaka sasa ni capitalist(inanyonya nchi ambazo ni 3rd world). from 1776 independent day to now on angalia china ni miaka mingapi kama sio 50---> na kutokea kuwa sawa kiuchumi na tanzania mpaka kuwa on par na marekani kwenye uchumi.kingine ni kuwa fisadi ni muuuuaji mkubwa kwa kuwa
1.akifisadi fedha za madawa hospitalini watu watakufa kwa kukosa huduma stahiki hapo hajaua bado au kwa kuwa hajashika silaha tu?
2.akitafuna fedha ya vitabu na madawati mashuleni wanafunzi watashindwa kusoma na hii itapeleke kuwa na wajinga(illiteracy) wengi mno kuliko waliosoma hii inapelekea uchumi kushuka na nchi kukwama kwa kukosa wasomi.
Yako mengi ila kiufupi KABLA HAUJATOA POST JARIBU KUANGALIA KWA JICHO LA TATU NA KUCHAMBUA MAWAZO YAKO MKUU sio unakurupuka kupost kwa kuwa hauzuiliwi na mtu.
 
Ikija huku akina kijo bisimba na ukawa watageuka.
 
Safi sana China

Hii kitu ikifanyiwa kazi hapa bongo kuna jamii zitapungua sana kwa idadi
 
Kwani sheria ya kusema fisadi asiuwawe katunga nani kwenye hizo nchi ambazo ww unaziiita civilized na kinyume chake kwenye hizo nchi unazoziita non civilized? Kwani si watu hao hao kwa my oppinion naona china ndiyo maaana imepanda uchumi kwa kasi sana kwa kuwa wao wana uongozi thabiti marekani ya leo imechukua miaka takribani 300 kuwa hivi ilivyo na hapo bado mpaka sasa ni capitalist(inanyonya nchi ambazo ni 3rd world). from 1776 independent day to now on angalia china ni miaka mingapi kama sio 50---> na kutokea kuwa sawa kiuchumi na tanzania mpaka kuwa on par na marekani kwenye uchumi.kingine ni kuwa fisadi ni muuuuaji mkubwa kwa kuwa
1.akifisadi fedha za madawa hospitalini watu watakufa kwa kukosa huduma stahiki hapo hajaua bado au kwa kuwa hajashika silaha tu?
2.akitafuna fedha ya vitabu na madawati mashuleni wanafunzi watashindwa kusoma na hii itapeleke kuwa na wajinga(illiteracy) wengi mno kuliko waliosoma hii inapelekea uchumi kushuka na nchi kukwama kwa kukosa wasomi.
Yako mengi ila kiufupi KABLA HAUJATOA POST JARIBU KUANGALIA KWA JICHO LA TATU NA KUCHAMBUA MAWAZO YAKO MKUU sio unakurupuka kupost kwa kuwa hauzuiliwi na mtu.
Kwanza kabisa, Huhitaji kumuua binadamu hadharani kama jawabu la tatizo hilo. Pili, huko China kwenyewe na kwingineko, imethibitika kuwa adhabu hiyo hutumika zaidi kisiasa; kuwanyonga wapinzani wa serikali kwa kisingizio cha ufisadi. Usikimbilie tu kutoa nadharia nyepesi za kiuchumi kuhalalisha kadhia hii nzito. Sijui kama kweli unauelewa mfumo wa uchumi wa China ulivyo. Naona unautolea maelezo ya kienyeji tena marahisi sana. It is not that simple. There is no short-cut to real human development.

Marekani wamepitia hatua zote za maendeleo na kufanikiwa kujenga mfumo imara na thabiti wa maendeleo usiomithilika dunia nzima. Ndio maana nchi zote zikiwemo China na Urusi zimeweka (deposit) utajiri wake Marekani. Ndio sehemu pekee yake inayoaminika duniani kwa mfumo wa fedha na utajiri duniani. Mabosi na matajiri wote wa China na Urusi wanasomesha watoto wao Marekani na kuhamishia mali zao huko.

Halafu ujue China, mtu akikosana na kiongozi mkuu mara nyingi atatangazwa fisadi na kulazimishwa kukiri wizi hadharani. Ni kama hapa Tanzania baada ya Lowassa kutangazwa kuwa fisadi papa halafu walioko madarakani CCM waamue kumnyonga hadharani. Jiulize watakuwa na uhalali/usafi gani wa kufanya hivyo? Na ni akina nani nchini watashangilia kwa dhati na kina nani watataharuki kuhusu kitendo hicho. Na ni kweli hiyo ndiyo itakuwa kiboko ya kumaliza au kupunguza ufisadi nchini? Sijui kama unaelewa maana hasa ya kitendo hicho. Si rahisi kurasimisha mauaji ya binadamu kwa serikali zetu hizi zinazoendeshwa kwa hila, ulaghai na uozo wa kila aina. You simply don't give them such a blank cheque!
 
Hapo
30714130_2108021735881122_8507926270831998773_n.jpg

China yanyonga hadharani wanasiasa 26 ambao ni wabadhilifu wa Mali za umma (Mafisadi).

Mafisadi hao walihukumiwa kifo cha kupigwa risasi uwanjani hadharani watu wakishuhudia baada ya kubainika kupora Mali ya umma. Inadaiwa kuwa yumo bilionare namba saba wa China.
Hapo ndipo utaona ubafiki wa wazungu, hutasikia kiongozi wa China anapekekwa ICC.
 
Back
Top Bottom