BBC.
China inadaiwa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti.
Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika.
"Badala ya kushirikiana na serikali za mataifa hayo, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked , mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka 'wakimbizi'," Watetezi hao wa usalama walisema walisema.
Waliongeza kuwa mamlaka ya China, kati ya Aprili 2021 na Julai 2022, "imewashawishi" raia 230,000 kurejea China kujibu mashtaka ya jinai kuhusu mawasiliano ya simu na ulaghai wa jumla.
Pia ilisema serikali ya China ilipiga marufuku raia wake kuhamia nchi tisa ambazo hazikutajwa kwa makosa ya "udanganyifu mkubwa, ulaghai wa simu na uhalifu wa mtandao".
BBC inafuatilia juu ya taarifa hii kwa kina katika mamlaka za serikali ya Tanzania na kutoa taarifa zaidi.
=======
Kufuatia taarifa iliyotolewa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa China itafungua vituo vya Polisi Afrika ikiwemo Tanzania ubalozi wa China kupitia akaunti rasmi ya Twitter wamekanusha taarifa hiyo na kusema kuwa ni uzushi.
Kwa upande wao Ubalozi wa China nchini Tanzania umekanusha taarifa hizo na kusema sio za kweli bali zimetungwa na baadhi ya Vyombo vya Habari vya Magharibi ili kuvuruga ushirikiano uliopo kati ya China na Afrika.
Ubalozi huo umesema China na Tanzania ni Marafiki wa muda mrefu kwenye maeneo yote na hawawezi kuyumbishwa na uzushi na kuvitaka Vyombo vya Habari vilivyosema vinautafuta Ubalozi kuthibitisha taarifa hiyo vifike Ubalozi “Mmesema mnataka kauli yetu, tupo hapa tunawasubiri”
Balozi wa Tanzania nchini China asisitiza kuwa China haifungui Kituo cha polisi Tanzania
Balozi wa Tanzania nchini China Mberwa Kairuki amekanusha taarifa zilizochapishwa na baadhi vya Vyombo vya Habari kwamba China inadaiwa kutaka kufungua Vituo vya Polisi nchini Tanzania “Taarifa hizi hazina ukweli wowote zipuuzwe”
Taarifa hiyo iliyochapishwa na Vyombo mbalimbali vya Habari ilisema China inadaiwa kufungua Vituo vya Polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na Raia wake wanaoishi katika nchi hizi tatu za Afrika.