China isingemchelewesha Lowassa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,532
TANZANIA imeingiliwa. Mtuhumiwa wa ufisadi ni miongoni mwa wagombea urais Tanzania. Uzembe huu unawezekana Tanzania tu. Huwezi kugombea nafasi yoyote Marekani ukiwa na kashfa kama zinazomkabili Edward Lowassa, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.

China ndio kabisa haivumilii uzembe wa aina hii unaoendekezwa Tanzania. Enzi zile Chadema kikiwa chama cha upinzani kinachojitanabahisha kwa vita dhidi ya ufisadi kilipata kuwa na mbunge machachari wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.

Ndesemburo ni miongoni mwa wabunge makini walioijadili Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Richmond LLC ya Houston, Marekani 2006, iliyosababisha, Waziri Mkuu, Lowassa, kujiuzulu.

Ndesamburo aliliambia Bunge, "…nchi za wenzetu kama za China, wahujumu wa namna hii siyo kwamba wanajadiliwa, wananyongwa hadharani." Kwamba wenye kuthibitika kuwa ni mafisadi wananyongwa China.

China, kwa mfano, ilimhukumu kunyongwa Liu Han, Februari 2015. Hii ni pamoja na kwamba Han alikuwa na shilingi trilioni 10. Fedha hizo za kifisadi hazikuweza kuinusuru nafsi yake na kuzimu. Gazeti la Telegraph la Uingereza la Februari 9, mwaka huu wa 2015 liliripoti kuwa Han alikamatwa 2013 na kunyongwa mara moja baada ya kupatikana na hatia ya ufisadi.

Operesheni Fox Hunt; maana yake ni Operesheni Kamata Mbweha. Kamata Mbweha imefanikisha kukamatwa watuhumiwa wa ufisadi 680 waliokimbilia Marekani, Canada, Australia na kwingineko. Walirudishwa China kujibu mashitaka ya ufisadi. Waliopatikana na hatia tayari wamekwishanyongwa. China haitaki porojo kuhusu ufisadi.

Dk. Harrison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge (kwa wakati huo), aliwasilisha taarifa ya Richmond bungeni Februari 6, 2008. Kamati ilimtuhumu Lowassa, pamoja na mambo mengine, kuvunja sheria kwa kushinikiza Tanesco kupokonywa jukumu la kutafuta kampuni ya kufua umeme.

Waziri wa Nishati na Madini, alimwandikia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julai 13, mwaka 2006, kuwa, "Nimezungumza tena na Waziri Mkuu (Lowassa) leo, juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo (wa Lowassa) ni ule ule niliokueleza awali na ameagiza…achukuliwe Richmond."

Kamati ya Dk. Mwakyembe ilimpa Lowassa masharti mawili. Kwanza, ajipime kutokana na ushahidi uliopatikana dhidi yake. Pili, au Bunge lithibitishe ushiriki wake kama angegoma.

Februari 7, 2008, Spika, Samuel Sitta, alimpa Lowassa nafasi ya kujitetea. Lowassa alikuwa na saa zaidi ya 18 kujipanga kujibu. Badala ya kujitetea alijiuzulu. Lowassa alifahamu kuwa asingeweza kuwababaisha wabunge makini kama akina Dk. Wilbrod Slaa.

Lowassa anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond. Siyo kweli. Magazeti yalianika bayana kashfa hiyo. Lowassa anadai kuwa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond akiwaeleza wenzake "kuhusu habari za magazeti." Alihisi kuelemewa?

Lowassa, na wapambe wake, anajitahidi kujionyesha kuwa yeye ni mtu wa uamuzi mgumu. Anatamani umma uamini kuwa Kikwete ndiye aliyekuwa na mamlaka ya kuvunja mkataba wa Richmond. Alipoona kuwa Kikwete havunji mkataba kwa nini hakujiuzulu? Mtu wa "uamuzi mgumu" asingesubiri Kamati Teule ianike uozo wa kashfa ili kujiuzulu.

Jitihada za Lowassa kujinasua katika kashfa ya Richmond iliyotia taifa hasara ya zaidi ya shilingi milioni 152 kwa siku, kwa miaka miwili, zikagonga mwamba. Anadai alionewa. Wakuonewa Lowassa? Wajumbe wa kamati hiyo wako hai.

Wabunge waliokuwa wakali kama akina Christopher Sendeka, Lucas Selelii, James Lembeli, Anna Malecela mpo? Dk. Slaa na wapinzani wenzake waliokuwa bungeni Februari 6 na 7, 2008 wakinyamaza mawe yataongea.

Na kwa jinsi Chadema hasa mwanasheria wake, Tundu Lissu, inavyohaha kumsafisha Lowassa kwa kashfa hii ya Richmond, siku za mawe kuitetea Tanzania haziko mbali.

Akiwa Mtera, Dodoma, Lowassa aliamua kutohutubia mkutano wa kampeni na badala yake aliwaruhusu wananchi wamuulize maswali. Michael Makanyi alimuuliza Lowassa kuhusu Richmond. Lowassa aligoma kujibu. Ukigoma kujibu swali mahakamani unafungwa.

Na siyo Richmond tu. Uadilifu wa Lowassa unatiliwa shaka na watu wengi, wakubwa kwa wadogo. Septemba 15, 2007 pale Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam na kwa ujasiri mkubwa Dk. Slaa alimtaja Lowassa katika orodha aliyodai ni ya mafisadi. Na kwa jinsi Lowassa anavyotamani kuwa Rais, japo kwa saa chache tu, angekimbilia mahakamani kama angekuwa msafi. Hakudiriki!

Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani, alituhumiwa kuwa ni fisadi. Sumaye alielewa kuwa dawa ya tuhuma ni kusafishwa na Mahakama. Aliwashtaki wote waliomtuhumu ikiwa ni pamoja na magazeti kadhaa. Sumaye aliuthibitishia umma, kupitia Mahakama, kuwa siyo fisadi.

Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari waliokutana na Lowassa Dodoma mwezi Mei nao waliutilia shaka na kuhoji utajiri wake. Lowassa aliwajibu akisema kuwa "ana ng'ombe kati ya 800 na 1,000. Kwetu Umasaini unapokuwa kiongozi unapewa ng'ombe ili usipate taabu kwa ajili ya kuwakarimu wageni wanapokuja." Siyo kweli. Hupewi ng'ombe Maasai ukiwa kiongozi.

Lowassa alikuwa Waziri wa Ardhi hadi mwaka 1995. Kuna tuhuma lukuki za yeye kujimilikisha ardhi kifisadi. Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo. Lowassa anadaiwa kujimilikisha na kuwamilikisha rafiki zake ranchi za taifa zikiwamo Mzeri iliyoko Korogwe, Mkata iliyoko Kilosa pamoja na Manyara iliyoko Monduli.

Lowassa anadiriki kuwakashifu wazalendo wanaopinga wizi wa mali za umma. Alisema, "..kudanganya watu kwamba nikiwa maskini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga."

Hakuna anayewachukia matajiri waliopata fedha zao kwa juhudi na njia halali, wanaolipa kodi na hawajawahi kupora ofisi za umma. Bilionea Philemon Ndesamburo, kwa mfano, ni kipenzi cha watu. Hakuna anayeutilia shaka utajiri wake. Anamiliki hadi chopa. Bilionea mwingine anayeheshimika ni Dk. Reginald Mengi. Mengi anamiliki hadi vyombo vya habari.

Haiwezekani kuwaorodhesha hapa matajiri wasafi Tanzania. Ni wengi. Hatuna shida nao. Ieleweke pia kuwa, kwa baadhi ya watu, nikiwamo mimi, Lowassa ni adui mkubwa wa sheria na utawala bora. Mwanzoni mwa kampeni zake alijaribu kuonyesha kucha zake akiahidi kuwaachia wabakaji waliopatikana na hatia

mahakamani. Wabakaji hao walikata rufaa lakini majaji wa Mahakama ya Rufaa wakawakuta na hatia. Lowassa angepata bahati ya kuwa rais angeunajisi muhimili wa Mahakama.

Gazeti la Mwananchi la tarehe 26 Mei 2015 lilimnukuu Lowassa akiuelezea uviziaji wake, "Chini ya uongozi wa Rais (Benjamin) Mkapa tukagundua hawa jamaa (City Water) ni matapeli...tulifanya kikao saa tisa alasiri, tukachukua kibali cha kumkamata yule Mzungu wa City Water na tukamfukuza akaondoka siku hiyo hiyo kwa ndege kurudi kwao, tulifanya saa tisa alasiri ili asiende mahakamani kupata zuio, kwa hiyo tulivizia muda huo ili asije kwenda kupata zuio." Huo ni uviziaji wa kimafia. Au mzungu aligoma kumpa Lowassa asilimia za mgawo?

Lowassa anadaiwa kuomba kura kanisani, Tabora, kwa kuwataka Walutheri wasali ili Tanzania impate Rais Mlutheri. Hii ni aibu. Ni uroho wa madaraka. Hata hivyo, bila shaka wengine iwe Walutheri ama la, wamemsikia na wamemwelewa. Watakuwa wameona rangi yake halisi na wanaweza wakaifanyia kazi kauli hiyo ya Lowassa, Oktoba 25.

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa kazi kubwa ya makabila iliyobaki ni kutambika. Hata hivyo, muhusika akipotosha kabila lake inaleta mushkeli na hasa kama anagombea wadhifa mkubwa zaidi nchini.

Waandishi makini wa wasifu wangeshachapisha vitabu vinavyoweka bayana historia ya viongozi wanaosaka madaraka kwa njia yenye shaka kama huyu Lowassa.

Naamini, wale wanaojitahidi kumsafisha Lowassa dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili watakuwa wakifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi na si taifa. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anawatahadharisha Watanzania dhidi ya genge hilo la wasafishaji akisema; "Hao wanaomtaka Lowassa ni wale wanaojua watanufaika binafsi (Lowassa akiwa Rais)." Mbowe anaonya kuwa Lowassa hafai kuongoza Tanzania.

Chanzo: Raia Mwema
 
Tunaanza na mkulu, kwa nini alimlea fisadi kiasi hicho jamani? Yaani ameshindwa kumnyonga hadi leo?!!!!!
Hivi tanzania wakisema wananyonga mafisadi si tutanyongwa wote? Kazi ipo kwa mnyongaji sasa yeye sijui atanyongwa na nani? Maana ye ndo atakuwa bonge la lifisadi.
 
kama china walikuwa hawacheleweshi mbona lowasa hajanyongwa wakati sheria hizo zito tanzania ya kunyonga mpaka kufa
 
China kuanzia rais anachukia rushwa na ufisadi na anamaanisha na mfumo ndivyo ulivyo. Sasa unataka kufananisha China na mfumo wetu? Badala ya kumshitaki kama kweli ni fisadi mnaishia kusema pembeni tu kwamba fidai ...fisadi, fisadi anaruhusiwa kuchukua fomu za kugombea urais, ...fisadi anawapelekesha kwenye kampeni. Kwa nini wasitumie mwanya huo kumshtaki ili kumaliza mzizi wa fitna?

Leo hii ningesikia kesi ya fisadi inaunguruma na anatakiwa mahakamani ningewapigia kura CCM, ila kwa usanii kama waliotufanyia washtakiwa wa EPA sina hamu nao hata kidogo, unawakatamata watu na kuwafunga kisha unawaachia kwa kukosa ushahidi? Mbona hizo hela hazijarudi kama hakuna aliyezichukua?
 
Nyie ccm ni maboya ndiyo maana tunataka tuwatoe madarakani.kama mna polisi,mahakama na mnashindwa kumkamata nyie ni maboya nchi imeawashinda pisheni ukawa wawaonyeshe wanaume wanavyotawala
 
Kwani tume haikuliona hilo,Magufuri aliuza nyumba za serikali kwa bei ya nyanya,nyingine akachukua yeye,nyingine akampa kimada wake,sio kashfa?na ole wake Lowasa akiingia Ikulu tunawanyanganya hizo nyumba!
 
Back
Top Bottom