China isingemchelewesha Lowassa

Naona umekuwa kama dr mihogo kumsema sana lowasa, hata tutajue madhambi na mapungufu ya huyo mnayemuita hana doa la kifisadi magufuli, manake tuwe fair ndo ujue ccm hakuna msafi, wananchi kuamka ndugu ni huu udhalimu wa ccm, kipindi hiki cha miaka 10 watu wa kipato cha chini wameteswa sana, hebu ona huu mtiririko na mengine ambayo siyajui sasa yote kasababisha lowasa, tuwe fair kaka,

1. Wanawake kujifungulia Sakafuni

2. Watoto kusomea chini ya Miti

3. Watumishi kulipwa mishahara ya Hadaa

4. Twiga kupandishwa kwenye Ndege

5. wizi wa ESCROW

6. Ufisadi wa EPA

7. Ufisadi wa RICHMOND

8. Ujangili Uliokithiri

9. Mikataba Mobovu ya Dhahabu

10. Mikataba mibovu kwenye Tanzanite

11. Mikataba mibovu kwenye Almasi

12. Ubinafsishaji wa Bandari, ATC, Mashamba yaNAFCO, VIWANDA, NBC nk

13. Huduma duni za Afya

14. Huduma Mbovu za Elimu

15. Ukosefu wa Maji

16. Ukosefu wa Umeme wa Uhakika

17. Gharama kubwa za Umeme

18. Kupanda kwa Bei ya Mafuta ilhali inashuka kwenye soka la Dunia

19. Gharama kubwa za vifurushi vya simu za mkononi

20. Wawekezaji kutokulipa kodi

21. Rais kusaini cheque kwa dhehebu moja

22. Pengo la kukataa Rasimu ya Katiba mpya

23. Ubovu wa barabara

24. Kugawana Nyumba za Serikali

25. Mauaji ya Daudi Mwangosi

31. Mkaahapa kujimilikisha mgodi wa Kiwira

32. Yusuf Marope kutumia Bilioni 5 uchaguzimdogo wa Tarime

33. Ufisadi wa Deep Green
34. Ufisadi wa Meremeta

35. Mabomu ya Arusha

36. Uvamizi wa vituo vya Police

37. Ununuzi wa Mv Dar es Salaam kifisadi

38. Mabehewa Feki ya Treni –

39. Ununuzi wa Ndege ya Rais

40. Mikataba 17 ya kichina

41. Kushamiri kwa biashara ya Sembe (madawa ya kulevya)

42. Usafirishaji wa Meno ya Tembo

We umemkomalia lowasa tu hayo hujayaona
 
Tungeungana tukatae wana siasa hasa Wa ccm ningeelewa post yako. Vile vile kitanzi kilitakiwa tuanze na raisi wenu maana ndo anaepiga ela nyingi kwa sasa kwa ujinga wenu..
 
liekashfa ya escrow ingelikua china la wanyongaji wa china wangefurahi msafi ni kingunge pekee na kaondokaa ccm
 
Kama kunyonga kuna familia za vigogo zitateketea kabisa kwa kunyongwa. Unamjua mhusika mkuu wa escrow? Hata aliyeuza nyumba za serikali angetandikwa risasi alafu familia ikalipe zile risasi. CCM kwa ujumla wangebaki kina Kingunge na Nyerere tu, Wengine wote wantedhanyongwa.
 
Na wewe una poor analysis. Wote uliowataja hawagombei urais. EL anagombea urais. Point ni kwamba sawa na uliowataja hapo juu hawafai kuwa marais wa nchi hii sababu ni fisadi. Ushkaji ndi umetufikisha hapa. Mode ya utawala wa sasa ndo mode ya EL. Unasema mabadiliko. Are u serious? Zaidi ni ushabiki na matumaini ya kiambulia vyeo vya kishkaji akiingia ikulu. Zaidi ya hapo EL hafai kuwa rais.

Wewe kwenu wapi? Umesoma wapi? Una uchungu kiasi gani na Nchi hii mpaka uitetee system ya wapigaji?
 
Na serikali hiyohiyo ya china ingeonekana ya kipuuzi kama ingemchelewesha MAGUFULI aliyeuza kwa bei ya kutupa na kugawana nyumba za umma na maswahiba wake, kuvunja mikataba kwa kukurupuka na kusababisha hasara kwa taifa ya zaidi ya sh. 900b,
 
Na serikali hiyohiyo ya china ingeonekana ya kipuuzi kama ingemchelewesha MAGUFULI aliyeuza nyumba kwa bei ya kutupa na kugawana nyumba za umma na maswahiba wake, kuvunja mikataba kwa kukurupuka na kusababisha hasara kwa taifa ya zaidi ya sh. 900b,
 
Ukweli ni kuwa tz msafi hayupo wote tunanuka rushwa ila tunataka kuitoa ccm madarakani imetawala imechoka .
 
Hyo list of shame ina majna 11, na lowassa yupo no 8,, mbn huanzii no 1 pia mkuu wa Kaya yupo pia 2010 aligombea ukaufyata,, tafakar kw kna list yte
 
Nilishasema kama miaka 10 iliyopita, huwezi kuwa na akili timamu ukashabikia matendo ya viongozi wa CCM. Ni miaka 9 sasa tangu tuambiwe mgao wa umeme utakuwa historia leo sijui kama wana la kutueleza
 
Pole pole and company at work. Mkuu huna jipya, huo wimbo juu ya ufisadi wa Lowasa wananchi tumeuchoka, tunachotaka ni CCM ikae pembeni. Angekuwa na hatia ya huo ufisadi, mzee JK alishindwa nini kumpeleka mahakamani? Mbona imefanyika hivyo kwa mzee Mramba na wenzake. Wimbo wa ufisadi wa Lowasa mnaachiwa muucheze hapo Lumumba, wananchi wimbo wao ni MBADILIKO-LOWASA, LOWASA-MABADILIKO. Mkuu tukutane kwenye masanduku ya kura tarehe 25, nakutakia kila la kheri.
 
Kenya ilikuwa na washukiwa wa mauaji ya kimbari, Rais na naibu wake, na kesi zinaendelea na wananchi walimwacha raila wakawaweka washukiwa, Peeples power mpaka leo uchumi ni mara mbili ya bongo, tanzanite zinauzwa kuliko bongo, wanaona faida yake
 
Inatupasa kufika mahali tuangalie wapi tulipotoka wapi tulipo na wapi tunaelekea, tukiweza kufanya hivyo tutaweza kuwajua waliotufikisha tulipo labda kwa mabaya au mazuri waliyoyafanya. Mtu mwenye akili akiangalia Edo lipopita na mambo aliyoyafanya ni ukweli usiopingika kua hawezi kuleta mabadiliko anayoahidi. Kama kwa miaka yote aliyokua serikalini amevurunda kwa afaida ake mwenyewe. hapa anatuhadaa ni ukweli kuwa hawezi
 
Siwezi kuisoma sana haabri yenyewe kwanza haina mvuto, lakini cha kuuliza kama Lowasa ni fisadi kwa nini hajachukuliwa hatua, au ndio kusema alikuwa anaishi kwenya nchi ya serikali legelege? Hivi sasa ukiambiwa utafute watu safi 50 Tanzania utawapata? acheni kuwa wavivu wakufikiri ! Lowasa ni safi kama ana elements za ufusadi ni kwakuwa alikuwa kwenye mfumo ambao unalea ufisadi
 
Back
Top Bottom