Chimbuko la Uislam na Karen Armstrong

Mwanzoni zilikuwa mbili. Baadae katika kuwaridhisha/kuwashawishi/kutafuta kukubalika kwa wayahudi waliompokea Madina, Muhamad aliamrisha ziwe tatu kuendana nao. Sasa zilifikaje tano. Tuendelee na usomaji hapa.
Kwa ufaham wangu hiki kipart kinashida kidogo au upotoshaji kwa kuwa kweli waislamu mwanzo walisali Mara mbili kwa siku ila mwaka wa kumi na mbili tangu mission ya Muhammad(Pbuh) iliamriwa kusaliwa Mara tano hapo kabla hawajaamia yathrib (medina) ambapo waliishi karibu na wayahudi hivyo sio sahihi kuwa waliiga kusali Mara tatu kama Armstrong alivyoeleza kutoka kwa wayahudi kwani waislamu walihamia Medina mwaka wa 13 tangu mission ya Muhammad (pbuh) kuanza
 
Siku nyingine uwe unatulia ukiona huna cha kuandika,suala la imani tu ulilo jifaragua kwalo nimekupa wasaa wa kulijengea hoja umeshindwa,sasa haya mengine ni muhalo kuyaweza.

Mjinga kama wewe nakupuuza sababi napoteza muda. Ukiwa na hoja leta tujadili,ila mpaka tulimalize hili la imani ulilo lianzisha.

Hivi ndivyo nilivyo mimi,mlipoambiwa msome na mkaenda kujidai mmesoma,mlizidhulumu nafsi zenu.

Kazi yangu nimemaliza.
Unasoma story za Wikipedia unatuleta hapa
 
Kiarabu kinaweza kuwa ngumu kwako kueleweka, labda nikueleweshe kupitia kifaransa, neno "Vous" linapotumika huwa na maana ya wewe (umoja) au ninyi, lkn kwenye umoja si kwamba linatumika kwa kila mtu, la hasha. Ikiwa mtu unamheshimu, utatumia " Vous " yaani wewe ninayekuheshimu yaani mtu mwenye cheo, lkn akiwa mtu wa kawaida unasema 'tu '

Kwenye English language, "You " pia humaanisha wewe au nyinyi, je ni wakati gani na mazingira wasomi wa English wapo wengi wataeleza.



Kwa hiyo kwenye kiarabu litumikapo neno نحن "sisi " kwenye nafsi ya umoja humaanisha utukufu au cheo,

Wasio jua huwa wanaingia mzima mzima eti wakiona ni hoja yenye kusupport imani ya Mungu zaid ya mmoja.La hasha sivyo.

Magwiji huwa wanawacheka wakiwaona kama ni wenye upungufu wa elimu.
Sasa mkuu kutaka kujua tu hivyo paka nikajifunze hiko kiarabu tena,duh
 
Kwa ufaham wangu hiki kipart kinashida kidogo au upotoshaji kwa kuwa kweli waislamu mwanzo walisali Mara mbili kwa siku ila mwaka wa kumi na mbili tangu mission ya Muhammad(Pbuh) iliamriwa kusaliwa Mara tano hapo kabla hawajaamia yathrib (medina) ambapo waliishi karibu na wayahudi hivyo sio sahihi kuwa waliiga kusali Mara tatu kama Armstrong alivyoeleza kutoka kwa wayahudi kwani waislamu walihamia Medina mwaka wa 13 tangu mission ya Muhammad (pbuh) kuanza
Mission ya Muhamad ilianza lini?
 
Unasoma story za Wikipedia unatuleta hapa
Onyesha kipi nimekitoa "Wikipedia". Ukiweza naacha kujadiliana katika hii mada.

Bado nakudai juu ya suala la imani. Usitake kuvaa viatu navyo vaa mimi,ona sasa vinavyo kupwaya.

Nipo ...
 
Hii ni Quran imesema tukampa injili ila haijaiita injili ya Issa.

je, na mimi nitakuwa sahihi kuiita Quran 'Quran ya mtume' na sio 'Quran takatifu'?
Unapo ambiwa Injili ya Issa si kwa maana yake bali alipewa na Mola wake kama muongozo,na ukisema Qur'aan ya Muhammad kwa maana ya kupewa kitabu haina shida.
 
Wew na mwamedi wezi tu!credible source ni Bible pekeyake nimeisoma yote mara 7
 
Salam wanaJF!

Mwanamama Karen Armstrong alifanya utafiti wa miaka mingi kuhusu chimbuko na mabadiliko ya dhana ya Mungu [Ieleweke ni dhana ya Mungu sio Mungu - Concept of God and Not God]. Baada ya utafiti huo akaja na kitabu alichokiitwa HISTORY OF GOD: THE 4,000 YEARS QUEST OF JUDAISM, CHRISTIANITY AND ISLAM. Kitabu hiki chenye umri wa takribani miaka takribani 30 sasa, kimeelezea ni kwa vipi dhana ya Mungu imekuwepo toka dunia ya kale, na imekuwa ikibadilika kila nyakati zinapobadilika. Na pili ameelezea chimbuko la dini kuu tatu duniani za Uyahu6, Ukristo na Uislam. Hapa ameelezea mazingira yalipoibukia dini hizi na mapokeo yake.

Katika mfululizo wa makala hizi ni simulizi kutoka kwenye kitabu hicho. Kila siku nitaweka sehemu moja ili tupate kuelewa taratibu na tuweze kujadili. Elimu za falsafa na dini huwa zinahitaji mwendo wa taratibu.

SEHEMU YA I - KUTEREMSHWA QURAN.

Katika mwaka 610 katika jiji la kibiashara lilokuwa na changamoto nyingi wakayi huo la Meka katika mji wa Hijjaz, mfanyabiashara wa kiarabu Ambaye pengine hajawahi kusoma Biblia, wala pengine alikuwa hajawahi kuwasikia kina Yeremia, isaya wala ezekiel alikuwa na mapitio kama yao. Kila mwaka, Muhamad Ibin Abdallah, kutoka kabila la Kureshi alikuwa akiipeleka familia yake kwenye milima ya Hijra iliyopo nje ya mji wa Maka kwa ajili ya kufanya maombi kipindi cha mwezi wa Ramadhani. Huu ulikuwa ni utamaduni wa jamii ya waarabu. Muhamad alikuwa akimuomba Mungu wa Juu wa Waarabu, na kutoa sadaka na chakula kwa masikini waliokuja kumtembelea kipindi hicho. Pengine alitumia muda wake kutafakari juu ya yanayojiri Katika mji wa Meka. Haya yanathibitishwa na maisha yake ya baadae wakati akiwaza jinsi gani ya kuiweka sawa jamii yake ya Maka, ambayo licha ya mafanikio yake ya sasa, imekuwa ikipitia matatizo mengi.

Vizazi viwili nyuma, watu wa Kuresh walipitia maisha ya kuhamahama kutafuta chakula katika nyika za uarabuni kama zilivyo jamii zingine za wabeduni. Katika karne ya sita mwishoni jamii hii ilibadilika na kuwa eneo muhimu kwa waarabu baada ya mafanikio yake makubwa kibiashara. Matajiri wengi walijitokeza na hali ya maisha iliboreka. Lakini mfumo wa maisha wa mila za asili za waarabu, uliondolewa na ubepari. Watu wengi walikuwa na wasiwasi na hatima yao chini ya mfumo katili wa ubepari, hivyo Muḥammad aliona ipo haja ya kuwa na itikadi mpya itakayorekebisha matatizo yanayojitokeza huko Maka.

Kwa mazingira yale, ufumbuzi wowote wa kisiasa ilikuwa ni lazima uwe na asili/sura ya kidini. Muhamad alitambua kuwa pesa ndio inakuwa mbadala wa Dini kwa Wakureshi. Hofu kubwa ya Muhamad ni kuwa, pesa iliyopokwa wakureshi ilipaswa tu iwaokoe kutoka kwenye madhira ya mfumo wa kubangaiza, Magonjwa na vurugu katika ya jamii ya wabeduni, Pesa sasa inageuzwa kuwa ndio 'msingi wa maisha yao'. Jamii imefanikiwa na kujitosheleza vya kutosha, kiasi cha baadhi ya watu kujiona kwakuwa ni matajiri basi wao wanamaisha ya milele (immortal). Kwa mtazamo wa Muhamad hali hii ya jamii ya wakureshi kujitosheleza (Istaqa), italeta utengano katika jamii yao. Miaka ya nyuma wakati wanaishi Nomadic life, mfumo wa maisha ulikuwa ni jamii kwanza, kisha mtu baadae. Jamii hiyo ilitambua kuwa ili kuishi, basi jamii inategemeana. Hivyo jamii ilipaswa kuwasaidia masikini na makundi yasiyojiweza. Kwa sasa umimi umetawala na kuuondoa umoja wa kijamii na ushindani umeondoa mashirikiano ya jamii. Watu walianza kujenga utajiri bila kujali waqureshi masikini. Kila koo ilipambana dhidi ya koo zingine ili kutengeneza utajiri. Koo za hali ya chini kama ya Hashmi yake Muhamad mwenyewe zilijiona ziko hatarini.

Muhamad aliona kama wakureshi wasipopata mfumo mwingine utaofanya wawe wamoja, basi tamaa ya utajiri utaitawanyisha kabila ya Wakureshi. Jamii zingine za kiarabu za kibeduni katika maeneo ya Hijaz na Najad nao zilikuwa kwenye taharuki. Watu waliishi kwa mapambano na kupigana kati yao ili tu kupata mahitaji ya msingi ya kila siku. Katika kujenga jamii moja, waarabu walikuwa na mfumo waliouita Muruwah, ambao ulitimiza majukumu mengi ya dini. Lakini kwa ujumla, waarabu hawakuwa na muda na dini. Walikuwa ni wapagan waliokuwa wakiamini katika miungu kila mmoja wa kwake nyumbani kwake. Haikuwepo Mfumo au imani moja iliyowaelezea waarabu umuhimu wa Mungu na maeneo matakatifu katika maisha. Hakuwa na ufahamu juu ya maisha baada ya kifo, Ila waliamini kuwa Giza (ambayo inaweza kutafsiriwa kama muda au hatma), ilikuwa ni UKUU(SUPREME). Katika jamii ambayo idadi ya vifo iko juu, Mtazamo huu ulikuwa muhimu.

Jamii za magharibi wanamtazamo mfupi kuhusu Muruwah, lakini kiuhalisia ilimaanisha hamasa ya mapambano, Uvumilivu na ustahimilivu kwenye shida na kujitoa kwa kabila. Mila za Muruwah ziliwataka jamii kuwa watiifu kwa kiongozi wa kabila (sayyid) hata kama maisha yake mwenyewe yako hatarini. Iliwataka jamii wailinde jamii na makundi yaliyo hatarini na pia wailipie kisasi jamii yao inapotendewa uovu. Kuhakikisha kuwa kabila linaendelea, Sayyid aliwagawia sehemu ya utajiri wake kwa watu, na katika mazingira ambayo mtu ameuawa, basi naye Sayyid alimuua mwanafamilia mmoja kutoka familia ya muuaji. Hii ilitokana kuwa ilikuwa ngumu wakati mwingine kumpata muuaji halisi, sababu ya mazingira aliweza kupotea na asijulikane, hivyo hakukua na wajibu wa kumuadhibu muuaji bali mwanafamilia wake.

Sababu ya kutokuwepo kwa utawala mmoja, mapigano yalikuwa ndiyo njia ya kuhakikisha usalama wa jamii. Hakukua na mfumo wa ulinzi ambao unaweza ufananisha na majeshi ya polisi wa leo. Kama chief akishindwa kupigana vita, basi hakuna mtu atayemuheshimu na anaweza jichukulia sheria mkononi na chochote kisimtokee. Hivyo kabila moja kupigana na jingine ilikuwa ndio mfumo wa kutafuta haki.

Licha ya mapungufu hayo ya ukatili, mfumo wa Muruwah ulikuwa na faida zake. Ulisisitiza usawa na matumizi sawa na bidhaa. Pengine katika jamik ambayo biadhaa ni adimu, basi usawa wa matumizi ya bidhaa ni muhimu. Mafunzo ya upeo na ukarimu zilikuwa ni mila muhimu na zikawafundisha Waarabu kutozingatia kesho yake. Mila hizi zilikuja kuwa za muhimu sana kwenye uislam, kama tutavyoona huko mbele. Mfumo huu uliwafaa waarabu kwa muda mrefu, ila kufikia karne ya 6, hakuweza kuendana na mazingira ya kisasa. Wakati wa kipindi cha mwisho cha zama kabla ya Uislam, waarabu wanakiita Jahiliyyah (zama za giza), watu wengi hawakuwa na amani pia walikuwa na mashaka juu ya imani zilitawala wakati huo. Kipindi hiki, Waarabu walikuwa wamezungukwa na dola kubwa mbili, Sassanid Persia na Byzantium.

Wafanyabiashara waliokuwa wakienda miji ya syria na iraq ya sasa, ndio waliokuwa chachu ya maendeleo kwani walikuwa wakija na hadithi na mawazo kuhusu ustaarabu waliokuta huko. Lakini vurugu za mara kwa mara, ziliwazuia waarabu kuwa jamii iliyo settle licha ya kuapata ideas mpya kutoka kwenye jamii zilizosettle za wasyria na wairaq. Hawakua na muda wa kuungana na kutengeza maisha yao kwa ujumla. Hivyo hata maeneo yenye rutuba hasa Uarabuni ya kusuni(Yemen ya leo), iliyokuwa na faida ya kijiografia ya mvua za Monson, ikachukiliwa na wapersia. Kuja kwa ideas mpya, kulihatarisha mila za kijama za jamii. Mfano, dhana ya kikristo ya Maisha baada ya kifo ambayo inasisitiza kuwa kila mmoja atawajibika kwa matendo yake, inaashirisha kila mtu kutengeneza maisha yake, na sio jamii kwa pamoja. Muhamad alikuwa ni mtu mwenye akili ya juu sana, (exceptional genius), hadi anafariki mwaka 632 alikuwa amefanikiwa kuziunganisha kabila za kiarabu Kuwa jamii moja iliyoungana (Ummah). Alifanikiwa kuweka imani ambayo kiupekee ilifit mila za waarabu na kuweza kuwapa hamasa kubwa ya maisha na kufanikiwa kutengeneza dola kubwa ya kiislam, Iliyoanzia Himalayas to the Pyrenees.

Na kujenga utamaduni/ustaarabu wa pekeee. Wakati Muhamad akiwa milimani akisali, ni dhahiri hakutegemea kufikia mafanikio makubwa kiasi hicho. Kama walivyokuwa waarabu wengine, Muhamad alimuamini al-Lah, jina la Mungu wa Juu wa waarabu toka kale. Neno hili lilitafsirika kuwa ni Mungu. Na Mungu huyu alikuwa na ufanano na Mungu aliyeabudiwa na wayahudi na Wakristo. Aliamini kuwa Mtume wa Mungu huyo ndiye atakaye wakomboa jamii yake, lakini kamwe hakuwaza kuwa yeye ndiye angekuwa mtume huyo. Jamii za waarabu kwa muda mrefu hakufurahishwa kuwa Mungu wao, al-Lah hajatuma mtume wake kwao wala kuwapa maandiko matakatifu, licha ya kuwa kwa miaka yote toka kale walikuwa na madhabahu wanayomuabudia. Hadi karne ya 7, waarabu wengi waliamini kuwa Kabah, dhabahu kuwa lenye umbo la Mche mraba, lililopo katikati ya mji wa Maka toka kale, lipo pale kwa ajili ya al-Lah, licha ya kuwa mungu wa watu wa Nabate aliyeitwa Hubal ndiye aliyekuwa dhabahu lake.

Kabah lilikuwa ni eneo la ufahari wa watu wengi wa Maka na ndiyo lilikuwa eneo takatifu Muhimu zaidi kwa watu wa Urabuni. Kila mwaka watu kutoka maeneo mbalimbali ya kuzunguka uarabuni walienda pale kwa ajili ya kuhiji. Na kufanya Ibada za kitamaduni kwa siku kadhaa. Eneo lote takatifu la kuzunguka kabah lilikuwa ni marufuku kufanyia mapigano, hivyo maeneo hayo na viunga vyake, biashara zilifanyika sana kwa kujua kuwa Chuki za kikabila maeneo yale zinasitishwa na kuzuia vurugu. Wakureshi walijua, bila maeneo hayo kuwa matakatifu, kamwe wasingefanikiwa kwenye ufanyaji biashara, hivyo ufahari wao ulitokana na eneo hilo hivyo walihitaji kulilinda eneo hilo takatifu la kale. Licha ya kuwa al-Lah amewapa upendeleo maalum wao wakureshi, lakini hakuwatumia mtume kama ilivyokuwa kwa Abraham, Moses au Yesu na Pia waarabu hawakuwa na maandiko matakatifu yaliyopo kwa lugha yao wenyewe. Hivyo walijihisi unyonge mara kwa mara wanapokutana na wafanyabiashara wa kiyahudi au kikristo waliokuwa wakiwadhihaki kuwa Watu washenzi ambao hawajapata ufunuo wa Mungu. Waarabu waliwaheshimu watu hawa kwa kuwa na elimu ambayo wao hawana.

Wakristo na wayahudi walikuwa wameendelea zaidi katika ukanda huo(kwenye masuala ya kidini), Lakini mtazamo wa waarabu ni kuwa ukristo na uyahudi ulikuwa ni bora tu dhidi ya miungu iliyopo maeneo yao huko. Kulikuwa na baadhi ya makabila ya wayahudi waliokuwa na mashaka na ukazi wao huko Yathrib(madina) na Fadak, na baadhi ya waliokuwepo kwenye eneo la kaskazini mwa Mpaka wa Persian na Byzantine Empire walibadili dini kwenye kwenye ukristo. Lakini wabeduni walikuwa na msimamo na waliojitegemea, Na hawakutaka kuwa chini ya utawala wa dola kubwa kama wenzao wa Yemen, na walijua fika dola zote za persian na Byzantine walitumia dini za uyahudi na ukristo kueneza tawala na mila zao kwenye ukanda huo. Pia walikwisha choka na migawanyiko ya kitamaduni, hivyo hawakutaka kabisa itikadi ya kigeni na inayofunzwa kwa lugha na tamaduni za kigeni.

Baadhi ya waarabu walijaribu kubuni imani ya Mungu mmoja ambayo haitakuwa na msukumo wa kibepari ndani yake. Kama ambavyo mwanahistoria wa Kipalestine wa Karne ya tano, Sozomenus anavyoeleza kuwa, Baadhi ya waarabu wa syria waligundua kitu kilichoitwa dini halisi ya Abraham, ambaye aliishi kabla Mungu hajaleta Torati wala Injili, Ambaye kwa hivyo hakuwa Myahudi wala Mkristo. Muda mchache Kabla Muhamad hajapokea wito wake wa kitume, mwandishi aliyemuelezea aitwa Muhamad ibin Ishaq, Waquresh wanne Wa maka, waliamua kutafuta dini halisi ya Abraham (Hinifiyyah). Baadhi ya waandishi wa kimagharibi, wanadai Kuwa suala la Hinifiyyah ni la kubuni na ilikuwa ni ishara ya kutapatapa kwa jamii hiyo ya zama za giza (jahiliyyah) Lakini ina msingi wake.
Mahaniffs watatu, hawa wanajulikana kama ni waislam wa mwanzo. Ubaydallah ibn Jahsh aliyekuwa binamu wa Muhammad, Waraqa ibn Nawfal ambaye baadae alibadili dini na kuwa mkristo, Zayd ibn Amri mjomba wake Umar ibn al-Khattab, washirika wa karibu wa Muhamad na aliyekuwa kiongozi wa pili wa dola ya kiislam(khalifa). Kuna hadithi kuwa siku moja kabla ya ufunuo kwa Muhamad, Zayd alipowakuta waquresh kwenye kaaba, alitamka maneno kuwa '....laiti angejua Mungu anaabudiwa vipi, basi angemuabudu, lakini kwa bahati mbaya hajui'.

Tamanio hili la kupata ufunuo, lilijibiwa usiku wa 17 wa Mwezi wa Ramadhani mwaka 610 katika mlima Hira. Alipokuwa amelala Muhamad alistuka usingizini na kuhisi kuwa amezingirwa na uwepo wa utakatifu katika eneo hilo. Baadae Alilielezea tukio hili lisiloelezeka kwa urahisi. Akitumia lugha ya kiarabu. Alieleza kuwa Malaika alijitokeza na kumpa maagizo kuwa, 'SOMA'[IQRA]. Kama ilivyokuwa kwa mitume ya kiyahudi waliokuwa wagumu kusoma maneno ha Mungu, naye Muhamad alikataa. Akijibu kwa 'Mimi siwezi kusoma'. Hakuwa Kahin, wasoma ushairi wa kikureshi. Anasema Muhamad kuwa malaika alimbana mwili kiasi cha kuhisu Pumzi inamtoka, Na kisha Malaika akamuachia na kumuambia tena IQRA. Alikataa na malaika akambana tena kiasi cha kufika mwisho wa uvumilivu. Mara hiyo ya tatu, Muḥammad alipata maneno aliyohisi tu yanatoka mdomoni kwake akiyatamka.

Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
Ambaye amefundisha kwa kalamu.


Maneno ya Mungu yakatamkwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya kiarabu na maandiko haya yakaitwa Quran: Usomaji.

Kesho tutaendelea na yaliyojiri baada ya Muḥammad kuteremshiwa Quran.
Uandishi wa namna hii,kama uko hivi katika hicho kitabu una makosq mengi sana. Kuna mengi ya kuzua.

Yaani huyu mama alitakiwa arejee vitabu vya asili vilivyo elezea habari ya Mtume,sababu kila kitu kipo wazi.
kutoka kabila la Kureshi alikuwa akiipeleka familia yake kwenye milima ya Hijra iliyopo nje ya mji wa Maka kwa ajili ya kufanya maombi kipindi cha mwezi wa Ramadhani.
Mfano hiki kipande,muandishi alitakiwa aweke ushahidi,sababu kina ukakasi. Maana familia ya Mtume ipi ? Na hayo maombi walikuwa wanayaelekezea wapi na kwa nani ?

Milima ya Hijra ndiyo milima gani ?
 
Hii nayo si hoja. Kuacha watu waseme si lazima waseme,na hapa kuna sababu nyingi.

Kadjalika kuna kujitapa na kuandika ukweli. Hapa naandika ukweli,ukweli ambao huwezi kuupinga wala kuukosoa kielimu.

Hakuna kichaa wa namna hii,haikai elimu kwa kichaa wala mjinga,ndiyo maana haya ninayo yaandika hakuna kichaa anayo yadiriki. Kama naandila uongo mpe kazi hii kichaa.

Nani amesema kwamba hujatoa mfano ? Msingi wa hoja yangu ni wewe kulinganisha vitu visivyo fanana. Soma vizuri nilichokiandika uone uzembe wako. Inaonekana ninacho kiandika hukisomi au hukieliwi.

Halafu kwa ujinga wako bado unakataa kama sikufundishi. Huwa nakwambia ya kuwa elimu ya mantiki ni dhaifu sana,mpaka unashindwa kuhoji. Ulitoa mfano wa dhana,dhana ambayo umeiegemeza kwa mtu asiye jua kusema ya kuwa square root ya 2 ni kumi. Nikaonyesha ujinga wako kwa kujenga hoja hi,kisha nikakwambia hivi asiyejua halimpitii hilo. Kwa maana unatengeneza ujinga kwa ujinga usio wezekana,yaani ni ujinga maradufu,kisha nikahitimisha ya kuwa unaandika kisicho halisi kwa kilicho halisi. Hujaelewa wapi ?

Vipi iwepo contradiction kwa mtu asiye jua uliyedhania atasema square root ya 2 ni 10 ? Wakati jibu linajulikana kuwa si kumi lazima liwe chini ya 2. Ni sawa udai kuna contradiction ya kuwa nusu ni mara ni moja juu ya mbili au moja gawa kwa mbili kisha mtu akasema ni tatu,kisha kwa kusema kwake ukasema hiyo ni contradiction. Hakuna contradiction hapo. Bali mmoja amekosea. Sasa usiwe unaandika andika tu kizembe.

Si kweli. Umesoma mantiki kwa nani mzee ? Au umejisomea mwenyewe ? Huwa hamchelewi kusema nimesoma mwenyewe sijafundishwa. Haya ndiyo matatizo ya kusoma mambo mwenyewe.

Unakosea sababu mantiki ni dhaifu katika uhalisia,yaani iko mbali na uhalisia ndiyo maana ukaweza kulinganisha vitu visivyo linganishwa katika uhalisia.

Unakosea kielimu,sababu umeshasema hujui square root ni nini,kinyume chake utakuwa unabahatisha na hakuna kubahatisha katika elimu.

Nyinyi ndiyo huwa mnasema "Mimo sijui lakini hunidanganyi chochote". Vipi usidanganywe wakati hujui ?

Kadhalika unakosea sababu utakuwa hujui bali unabahatisha,na hakuna kubahatisha katika elimu. Yaani unakuwa bado unakosea na hujui.

Nacho pinga ni wewe kulinganisha visivyo linganishwa wala kulinganishika na nina pinga wewe kujalia kuwepo kwa "contrdiction" sehemu ambayo haina "contradiction" huu ni uhuni na uzandiki.

Mpaka ikidhi vigezo na masharti.
Nikijua kwamba square root ya mbili ni kazima iwe ndogo kuliko 2, halafu mtu akaniambia square root ya 2 ni 10, na mimi najua 10 ni kubwa kuliko 2, nikasema 10 haiwezi kuwa square root ya 2, kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, hapo sijawemeza kujua kwamba 10 si square root ya 2, bila hata kujua squar3 root ya 2 ni nini?

Unabishia hesabu?

Unasema square root ya 2 ni 10?
 
Nikijua kwamba square root ya mbili ni kazima iwe ndogo kuliko 2, halafu mtu akaniambia square root ya 2 ni 10, na mimi najua 10 ni kubwa kuliko 2, nikasema 10 haiwezi kuwa square root ya 2, kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, hapo sijawemeza kujua kwamba 10 si square root ya 2, bila hata kujua squar3 root ya 2 ni nini?

Unabishia hesabu?

Unasema square root ya 2 ni 10?
Hivi huwa unaelewa ninacho kiandika ?

Ungekuwa umeelewa usingerudia huu utoto.
 
Uandishi wa namna hii,kama uko hivi katika hicho kitabu una makosq mengi sana. Kuna mengi ya kuzua.

Yaani huyu mama alitakiwa arejee vitabu vya asili vilivyo elezea habari ya Mtume,sababu kila kitu kipo wazi.

Mfano hiki kipande,muandishi alitakiwa aweke ushahidi,sababu kina ukakasi. Maana familia ya Mtume ipi ? Na hayo maombi walikuwa wanayaelekezea wapi na kwa nani ?

Milima ya Hijra ndiyo milima gani ?
Ni typo, Mount Hira and not Hijra.
 
Hivi huwa unaelewa ninacho kiandika ?

Ungekuwa umeelewa usingerudia huu utoto.
Nitaelewaje mtu unabishia hesabu?

Nimeona njia rahisi kabisa ya kuelezea mantiki ni hesabu, hesabu simple haina ubishi.

10 haiwezi kuwa square root ya 2.

Kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 10.

Hivyo naweza kujua 10 si square root ya 2, bila hata kujua square root ya 2 ni ipi.

Jibu la 10 kuwa square root ya 2 lina contradict basic principle ya kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na hivyo jibu hili si sahihi, naweza kujua jibu hili si sahihi hata kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi. Naliondoa jibu hili kwa "elimination method".

Hapo tumeona mtu anaweza kujua jibu fulani si sahihi, bila hata kujua jibu sahihi. Sihitaji kujua mji mkuu wa Tanzania ni mji gani ili kujua kwamba Washington DC, mji ulio Marekani, hauwezi kuwa mji mkuu wa Tanzania, ikiwa najua mji mkuu wa Tanzania ni lazima uwe Tanzania.

Unabisha nini sasa hapo?
 
Nitaelewaje mtu unabishia hesabu?

Nimeona njia rahisi kabisa ya kuelezea mantiki ni hesabu, hesabu haina ubishi.

10 haiwezi kuwa square root ya 2.

Kwa sababu square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 10.

Hivyo naweza kujua 10 si square root ya 2, bila hata kujua square root ya 2 ni ipi.

Jibu la 10 kuwa square root ya 2 lina contradict basic principle ya kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na hivyo jibu hili si sahihi, naweza kujua jibu hili si sahihi hata kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi. Naliondoa jibu hili kwa "elimination method".

Unabisha nini sasa hapo?
Soma nilicho kiandika,nimeeleza kwa Kiswahili chepesi sana.

Nashangaa unapo hamisha hoja kwa kusema nabshia hesabu wakati jambo hilo hulikuti katika nilicho kiandika,na nimeweka wazi msingi wa hoja yako na yangu ni katika dhana yako juu ya aisyejua na ukadhania kwa kukata kabisa atasema ya kuwa square root ya 2 ni 10, na hoja yako nyingine ni kujaalia "contradiction" sehemu ambayo hakuna "contradiction", lakini kwa kutokuwa makini unaleta hoja mpya ya kusema nabishia hesabu ?

Nani amekwambia kwamba 10 inaweza kuwa square root ya 2 ? Kuwa makini mzee.

Huwezi kujua square root ya 2 kuwa ni ndogo kuliko 2 kama hujui nini maana ya Square root,hili weka akilini.

Kaka unasinzia nini ? Au kama umeshughulishwa tulia kwanza ndiyo ujenge hoja. Usipoteze muda kwa jambo ambalo sijaliandika.
 
Soma nilicho kiandika,nimeeleza kwa Kiswahili chepesi sana.

Nashangaa unapo hamisha hoja kwa kusema nabshia hesabu wakati jambo hilo hulikuti katika nilicho kiandika,na nimeweka wazi msingi wa hoja yako na yangu ni katika dhana yako juu ya aisyejua na ukadhania kwa kukata kabisa atasema ya kuwa square root ya 2 ni 10, na hoja yako nyingine ni kujaalia "contradiction" sehemu ambayo hakuna "contradiction", lakini kwa kutokuwa makini unaleta hoja mpya ya kusema nabishia hesabu ?

Nani amekwambia kwamba 10 inaweza kuwa square root ya 2 ? Kuwa makini mzee.

Huwezi kujua square root ya 2 kuwa ni ndogo kuliko 2 kama hujui nini maana ya Square root,hili weka akilini.

Kaka unasinzia nini ? Au kama umeshughulishwa tulia kwanza ndiyo ujenge hoja. Usipoteze muda kwa jambo ambalo sijaliandika.
Tuanze polepole.

Hoja yangu ya msingi ni kwamba, mtu anaweza kujua jibu fulani si sahihi, kwa sababu lina contradict basic principle, bila hata ya kujua jibu sahihi ni lipi.

Unakubaliana na hoja hii au unaipinga?
 
Kunyenyekea kwake na kutii.
Ni vipi kwenye kunyenyekea na kutii pekee kumfanye mtu aitwe muislam? Ni wazi lazima kuwe na utofauti wa kimatendo ambayo itamtanabaisha mtu kuwa muislam. Wapo waliotii na kunyenyekea kwa Mungu wao tofauti na anayetambulika kwa jina la Allah je yafaa kuitwa waislam?

Uislam una misingi (nguzo) je unao ushahidi wa kimatendo aliyoyafanya Adam kutimiza nguzo zote tano za uislam?
 
Back
Top Bottom