Chimbuko halisi la migogoro shule ya sekondari Nyiendo

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
200
431
Kuanzia Mkuu wa shule aliyeifungua Issa Izengo mpaka Mkuu wa shule aliyepokea kijiti chake Erasto Arende, Shule ya Sekondari Nyiendo haikuwahi kuwa kwenye vuguvugu la migogoro mpaka alipoingia mkuu wa shule aliyepo sasa!

1. Philosophy ya kwanza ya mkuu wa shule ni kutopenda kukosolewa na ukimkosoa basi yanaanza maisha ya visasi na chuki kwa mwalimu husika.

Kipindi anaingia madarakani walimu wa kwanza kukumbana na hili rungu walikuwa 11 ambao mara kwa mara vikaoni walikuwa wakiulizia mambo ya shule kwa uwazi na ukweli. Hili jambo lilimkera sana na kwa usaidizi wa mawazo ya mwl mmoja toka idara ya taaluma walimu wale waliidhinishwa wakafundishe shule za msingi.

Shule ikaanza kuyumba.Wazazi wanalaumu serikali haiajiri walimu wakati kuna mtu kimakusudi kabisa bila kujali athari ambazo zingejitokeza baadae akaamua kuwapeleka shule za msingi. Ikitokea mwalimu kaugua ama dharura watoto hawasomi. Shule imepwaya Kwa uzembe wa mtu mmoja na bado yupo madarakani!Wanaotaka kuamini hili fikeni kituoni. Tujiulize swali ingekuwa yeye ndie mmiliki wa hii shule angeweza kuwa jasiri kupeleka walimu mashule mengine huku wanafunzi wake wakiteseka?Jibu ni hapana,asingeweza. Kafanya hayo maana hana cha kupoteza!

2. Ni mkuu wa shule asiyependa kupelekewa walimu wa field na hata wakipelekwa wanaweza maliza mafunzo bila mkuu wa shule kujua wanaishi vipi! Wanaohitaji ushahidi wa hili tafuteni walimu waliopita hapo ndani ya miaka mitatu au minne.Na hata wakirudi field bunda, huwa hawarudi Nyiendo na hawataki kuisikia kabisa!

3. Yeye kiukweli ni mkuu mzuri ila kaharibiwa na makundi

4. Ni Mwalimu anayehusudu siasa za makundi sana,kiasi kwamba ukiwa na mgogoro nae umekuwa na mgogoro na kundi zima ambalo kazi zake huwa ni kusikiliza nani kasema nini juu ya mkuu wa shule kisha taarifa zinapelekwa ofisini.Hili kundi ndilo lenye mandate ya kupitisha ama kukataa agenda za shule vikaoni.Wanaohitaji kujua pia hili fuatilieni. Na haya ndio yanaenda kuisambaratisha shule siku za baadae!

5.Kuna mwalimu mmoja wa somo la kiswahili huyu ni kama chaja ya Kobe au msumeno!Kwa kifupi huwa hana kundi maalum ila ni mfitinishi sana.(Huyu ana makala yake)

6.Taaluma haijapewa kipaumbele inashangaza katika pannel za usahihishaji walimu wanaweza kukaa hata siku mbili bila kupewa hata maji achana na suala la chai au chakula.Mnaohitaji kujua hili fuatilieni kituoni muone. Kutokana na taaluma kupewa less priority haishangazi kuona mwalimu kuchukua mitihani na kuwapa wanafunzi kusahihisha.Hili pia fuatilieni.

7. Hana utu hata kama mwalimu wake kalazwa hospital ni nadra kwenda kumjulia hali labda ataanza sasa baada ya kuona hii post. Na unaweza toa taarifa ya msiba ukajibiwa simply tu,ok mwalimu.

Mtakaofuatilia pia ulizeni wanafunzi uwajibikaji wa walimu wao.Mkiangalia Class journal tu zitawapoteza.Kikubwa mtakaopofika shuleni msiulizie walimu tu. Iteni walimu wasiofungamana na upande wowote wawape uhalisia maana tayari alishalipanga genge lake kumtetea!

Bado tunaendelea....stay tuned

Mshampata mbuzi wa kafara bado mnawasaka watatu ambao wote ni wanawake. Ila hasa hasa wamebaki wawili wote somo la kiswahili.
 
Back
Top Bottom