Cheti cha Kuzaliwa kiwe na option ya 'single parent'

Cheti cha Kuzaliwa kiwe na option ya 'single parent'

Pole Grena....

Sifungani na upande wowote, ila kuhusu mada tajwa napendekeza hivii.....
1. Jina la baba liwepo kwenye cheti cha kuzaliwa bila kujali baba anawajibika au hawajibiki, amekimbia matunzo au alikataa mimba.
Kuna memba mmoja amesema ukweli, kisaikolojia watoto wanaathirika sana panapokuwa na tofauti ya malezi kwa wazazi akilinganisha na watoto wenzie shuleni. Huyu memba ni mwalimu, na watoto wanafunguka mwa walimu zaidi kuliko baba au mama. Kisaidia watoto acha mtoto aje kumkataa mzazi wake mwenyewe ambaye hakuhusika na malezi yake akiwa mkubwa. Maana penye ukweli uongo hujificha japo mara ingine uongo hugeuzwa ukweli kwa kutumia pesa.

2. Linapokuja swala la mzazi mmoja anaposhuhulikia nyaraka za kisafiria - passport au kuomba visa, basi ofisi husika ichukue jukumu la kuhakiki kuwa huyu mzazi kweli ni single parent na hatoroshi mtoto au kumuingiza kwenye biashara haramu.
Amana yake hapa mamlaka za passport na visa wangeweka muda wa kuhakiki nyaraka za mzazi au mtoto aliyelelewa na single parent (Amana yake kwa wakati huo hawezi kuleta nyaraka za mzazi mwenzie kuridhia safari ya mtoto) basi mamlaka husika itatumia miezi 2 kuhakiki kweli jina la baba/mama Mwenye cheti cha kuzaliwa ni jina tuu na hajajihusisha na Maelezo kwa maana ya kwamba mamlaka itamtafuta mhusika (with google wiki hizi unaweza mpata mtu Wakazi kwa kuanzia au kuulizia- trace) kisha atahojiwa maswali chokozi ambayo mamlaka itajua tuu huyu ni mama/ baba galasha.

Basi single parent atapewa passport au visa ya mwanae waendelee na maisha.
Ikiwa mzazi galasha akataka kumharibia mwenzie makusudi tuu pia itafahamika maana maswali yatakiwa ni kuhakiki je yupo kiuhalisia kwenye maisha ya kilasiku ya mtoto bila kujali anahela ama laah. Mfano; mtoto anasoma shule gani, ana kovu gani la kudumu kwenye mwili wake, mwalimu wake wa darasa anaitwa nani, rafiki wa mtoto wako ni nani, mtoto wako anapendelea vitu gani (hobbies).

Hili swala liwekwe kwa namna ya kuangalia mtoto alitoroshwe Ila pia mzazi anayemlea mtoto pekeyake akiwa anataka kusafiri na mtoto asifungiwe milango kisa alete uhakiki wa baba mzazi ambaye wakati huo wana ugomvi na mzazi mwenzie.

Mei show a siku, sio tuu kuwa makini na njia za uzazi wa mpango, sio tuu kuwa wepesi kutoa mimba, sio tuu kuacha kudinyana bali kujitathmini kabla ya kitendo chochote unachotaka fanya, UKIP tayari kukabiliana na matokeo ya utachokifanya ikiwa ni pamoja na stress, kuonewa, kudhulumiwa, kudharauliwa n.k.....???!

Alamsiki.
 
Mtoto ana wazazi wawili unless umepandikizwa mbegu
Hili swala la kupandikiza mbegu naona watu wengi linawachanganya na suala responsibility ya mzazi.

Jamani kupandikiza mbegu ni maamuzi wanayoyafanya wanandoa au mtu binafsi pale anapotaka mtoto kutokana na kuwa na shida za uzazi.

Haihusiana na u single parent sababu Kama wanandoa wawili wamepandikiza mbegu mtoto ni wao wote just wametumia njia nyingine kumpata kutokana na kushindikana kwa mfumo wa kawaida. Majukumu ya kumlea ni ya wao wote
 
Unadhani kuwa mzazi ni kuweza kuzaa/kuzalisha tu?? Kuwa mzazi ni kuwa responsible for your kids haijalishi mko pamoja au mmeachana na mzazi mwenzako Watoto lazima uwape kipaumbele. sio unazalisha huko halafu unatekeleza Watoto then unajiita Baba. Hapo ni sperm donor tu
Dah!! Najiuliza sana! Wengine wanafunga na kuomba wapate watoto! Wengine wanazitoa mimba na kuwauwa watoto! Wengine wanagombana kisa wamepata mtoto!
Wengine wanaamini mtoto ni baraka!
Wengine wanathubutu kumnyang’anya mtoto haki zake za ki DNA!
Hizi mambo ya kutegesha mimba kwa expectations za maisha ya hali ya juu na tamaa nadhani ndio chanzo cha haya, huwezi kuusikia huu upumbavu huko masaini, umang’atini, vijijini huko na kwingineko ambako hakuna hawa wanaojiita wasomi! Muogopeni MUNGU sasa na muwapende watoto mnaopewa kama zawadi na baraka na MUNGU! Huwezi kusema unampenda mtoto wako kwa kumlea kwa ugomvi! Utakuta ni single maza lakini kazaa wa kwanza kaachika, kazalishwa na mwingine kaachika! Something wrong somewhere
 
Dah!! Najiuliza sana! Wengine wanafunga na kuomba wapate watoto! Wengine wanazitoa mimba na kuwauwa watoto! Wengine wanagombana kisa wamepata mtoto!
Wengine wanaamini mtoto ni baraka!
Wengine wanathubutu kumnyang’anya mtoto haki zake za ki DNA!
Hizi mambo ya kutegesha mimba kwa expectations za maisha ya hali ya juu na tamaa nadhani ndio chanzo cha haya, huwezi kuusikia huu upumbavu huko masaini, umang’atini, vijijini huko na kwingineko ambako hakuna hawa wanaojiita wasomi! Muogopeni MUNGU sasa na muwapende watoto mnaopewa kama zawadi na baraka na MUNGU! Huwezi kusema unampenda mtoto wako kwa kumlea kwa ugomvi! Utakuta ni single maza lakini kazaa wa kwanza kaachika, kazakishwa na mwingine kaachika! Something wrong somewhere
Elewa post, hakuna sehemu imesemwa unamlea mtoto kiugomvi. Kama hauna mawasiliano na baba na hana msaada na mtoto inshort kawatekeleza, why use his name kwa birth certificate???
 
Elewa post, hakuna sehemu imesemwa unamlea mtoto kiugomvi. Kama hauna mawasiliano na baba na hana msaada na mtoto why use his name kwa birth certificate???
Nikweli hakuna sehemu kumesemwa neno UGOMVI! Ila kwa busara za wenye hekima watajiuliza kulikoni hutaki jina la baba litumike!!?
Wababa wanafariki na watoto bado wanatumia ubin wao, wababa wanafungwa lakini watoto hawabadili ubin wao, wababa wanapotea katika mazingira ya kutatanisha lakini watoto hawabadili ubin! Wababa wanafilisika watoto hawabadili ubin, wababa wanakuwa vichaa watoto hawabadili ubin! Je! Weye usiyetaka mtoto asitumie ubin wa baba mzazi ulibakwa na stranger usiyewahi kumjua? Ulipata mimba ukiwa swimming pool!!? Lazima kuna roho ya ugomvi inayosukuma kumkomoa mtoto na sio baba mzazi! Mpiganie mtoto wako apate haki ya kumjua baba maana hata MUNGU anamtambua baba mzazi na sio baba copy!
 
Nikweli hakuna sehemu kumesemwa neno UGOMVI! Ila kwa busara za wenye hekima watajiuliza kulikoni hutaki jina la baba litumike!!?
Wababa wanafariki na watoto bado wanatumia ubin wao, wababa wanafungwa lakini watoto hawabadili ubin wao, wababa wanapotea katika mazingira ya kutatanisha lakini watoto hawabadili ubin! Wababa wanafilisika watoto hawabadili ubin, wababa wanakuwa vichaa watoto hawabadili ubin! Je! Weye usiyetaka mtoto asitumie ubin wa baba mzazi ulibakwa na stranger usiyewahi kumjua? Ulipata mimba ukiwa swimming pool!!? Lazima kuna roho ya ugomvi inayosukuma kumkomoa mtoto na sio baba mzazi! Mpiganie mtoto wako apate haki ya kumjua baba maana hata MUNGU anamtambua baba mzazi na sio baba copy!
Ubaba ni more than biological factors, si eti kwasababu wewe ndo biological fathee lakini haufanyi vile anavyotakiwa baba afanye utegemee heshima yako ibaki palepale.

Baba lazima utimize majukumu and be there for your kids, usitegemee unapotea huko hauna mawasiliano tangu umuache dada wa watu mjamzito, hujawahi mwona hata mtoto Halafu bado upewe heshima ya ubaba.

Halafu baba aliyefariki, aliyefilisika watoe kwenye huu mjadala. Tunaongelea baba asiyekuwepo kwenye maisha ya mtoto na hana shida hata ya kutaka kujua mtoto anaendelea yani Kama vile hayuko duniani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] na mtu akinitundika akimbie atanitambua aisee, aache chata nzuri hvo, huyo lazima arudi kwa machozi
Huishiwi vituko! [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
 
Ubaba ni more than biological factors, si eti kwasababu wewe ndo biological fathee lakini haufanyi vile anavyotakiwa baba afanye utegemee heshima yako ibaki palepale.

Baba lazima utimize majukumu and be there for your kids, usitegemee unapotea huko hauna mawasiliano tangu umuache dada wa watu mjamzito, hujawahi mwona hata mtoto Halafu bado upewe heshima ya ubaba.

Halafu baba aliyefariki, aliyefilisika watoe kwenye huu mjadala. Tunaongelea baba asiyekuwepo kwenye maisha ya mtoto na hana shida hata ya kutaka kujua mtoto anaendelea yani Kama vile hayuko duniani.
Dah! Mpeni tu mtoto jina la baba yake kuepuka dhambi ya kudanganya. Akikuwa mwambieni ukweli yeye aamue kusamehe au kutokusamehe! Hii itaepusha lawama na tukumbuke maisha hubadilika hivyo na binadamu mioyo hubadilika! Leo na kesho baba ndio huyoo anaonyeshwa kwenye TV ameshikilia matanzanite ya kilo ishirini kama laizer unadhani hutaruka juu nakumwambia mtoto baba yako huyooo!!!? Au baba mzazi ndio kawa waziri flani hivi si kesho yake tu uko mapokezi na mtoto!!? Haya mambo yasitatuliwe kwa hasira! Cheti hakitabadili utambulisho wa kihaki wa mtoto, cheti kitabaki kama hati shitaka danyanyifu kwa pande mbili, kwa baba na kwa MUNGU!
Ni mtazamo wangu tu!
 
Mtu hana msaada,lakini mbegu zake ndio zina msaada kwa kukupa hicho kiumbe.

Kazi kwelikweli.
 
Watu wanakosea Sana.

Kila mtoto anahaki ya kuzaliwa ndani ya familia yenye wazazi wote.

Kama hutaki kuzaa usifanye ngono na mtu ambaye huna mpango wa kuwa na future naye.
 
A
Sasa kama alitaka uzae kwa nini akatae mtoto.We ulijilengesha kisha ukataka mimba halafu ukaleta dharau akakubwaga.
Are you serious? Hujui Dunia ilivyo? Jadili Kama mtu mzima, mimba hazikataliwi?
 
Habari zenu wakuu,

Kwenye suala la cheti cha kuzaliwa hapa Tanzania ni lazima sehemu ya wazazi wa mtoto Baba na Mama majina yao yawekwe. Hili linaleta ugumu kwa single parent ambapo unalazimishwa kumuweka mtu ambaye hana msaada na wewe tangu ujauzito na wala hakusaidii chochote na ukute hajawahi kumuona huyo mtoto tangu azaliwe.

Rita inabidi mliangalie hili, isiwe ni lazima majina ya wazazi wote wawili wawepo kwenye cheti cha kuzalia. Kuwe na option ya mzazi mmoja Kama single parent, sio kulazimisha majina ya baba eti kama humuweki baba wa mtoto weka baba yako au kaka ilimradi ile nafasi ya baba mtoto isiwe wazi.

Nchi za wenzetu hata hapo Kenya tu wanafanya hili, baadae kama baba atarudi na mama ataridhia mtoto atumie jina la baba, wanarudisha cheti na kuongeza jina la baba.

Na hii pia inaleta matatizo in future utakuta documents za baba zinahitajika just because jina lake liko kwenye cheti Cha kuzaliwa na hapo utakuta hamna mawasiliano. Lakini ukiwa single parent wanajua baba hayuko kwenye maisha ya mtoto. Eg uende kuapply passport au visa uhamiaji na ubalozi kote watataka consent letter kutoka kwa baba kuthibitisha anakubaliana mtoto asafiri.

Kuwa mzazi sio kuzalisha/kuzaa tu, Lazima Kama mzazi ubebe majukumu yako. Iwe mko pamoja au mmeachana na mzazi mwenzako, Watoto lazima wapewe kipaumbele.

Rita msilazimishe watu kuwa mababa kwa kuweka majina yao kwenye cheti Cha kuzaliwa wakati hata hajui sura ya mtoto. Sheria ibadilishwe, Option ya single parent inahitajika.
Mtoto ataitwa
Jesse Mariam au Merina Mariam
 
Baba ndio kamkosesha haki maana ni mjinga na Mimi sioni umuhimu wakuandika jina lake kwa mwanangu asije na yeye kurithi tabia zake chafu
Hihiiii mlicheza wote kwenye matope leo unasema mwenzio ndo mchafu....😁😁😁
 
Back
Top Bottom