Cheti cha Kuzaliwa kiwe na option ya 'single parent'

Cheti cha Kuzaliwa kiwe na option ya 'single parent'

Grena

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
656
Reaction score
1,557
Habari zenu wakuu,

Kwenye suala la cheti cha kuzaliwa hapa Tanzania ni lazima sehemu ya wazazi wa mtoto Baba na Mama majina yao yawekwe. Hili linaleta ugumu kwa single parent ambapo unalazimishwa kumuweka mtu ambaye hana msaada na wewe tangu ujauzito na wala hakusaidii chochote na ukute hajawahi kumuona huyo mtoto tangu azaliwe.

Rita inabidi mliangalie hili, isiwe ni lazima majina ya wazazi wote wawili wawepo kwenye cheti cha kuzaliwa. Kuwe na option ya mzazi mmoja Kama single parent, sio kulazimisha majina ya baba eti kama humuweki baba wa mtoto weka baba yako au kaka ilimradi ile nafasi ya baba mtoto isiwe wazi.

Nchi za wenzetu hata hapo Kenya tu wanafanya hili, baadae kama baba atarudi na mama ataridhia mtoto atumie jina la baba, wanarudisha cheti na kuongeza jina la baba.

Na hii pia inaleta matatizo in future utakuta documents za baba zinahitajika just because jina lake liko kwenye cheti cha kuzaliwa na hapo utakuta hamna mawasiliano. Lakini ukiwa single parent wanajua baba hayuko kwenye maisha ya mtoto. Eg uende kuapply passport au visa uhamiaji na ubalozi kote watataka consent letter kutoka kwa baba kuthibitisha anakubaliana mtoto asafiri.

Kuwa mzazi ni kuwa responsible for your kids haijalishi mko pamoja au mmeachana na mzazi mwenzako Watoto lazima uwape kipaumbele. sio unazalisha huko halafu unatekeleza Watoto then unajiita Baba. Hapo ni sperm donor tu

Rita msilazimishe watu kuwa mababa kwa kuweka majina yao kwenye cheti Cha kuzaliwa wakati hata hajui sura ya mtoto. Sheria ibadilishwe, Option ya single parent inahitajika.
 
Mimba haitengenezwi na mtu mmoja, inabidi umweke tu kama sperm donor lakini siyo baba mlezi.
Mkuu shida inakuja kuwa in future unakuwa huna Uhuru na mtoto lazima baba documents zake zihitajike na ukute hamna mawasiliano lakini ukiwa single parent yeye anajulikana hayuko kwenye maisha ya mtoto. Mfano unaenda kuomba passport ama visa ya mtoto, uhamiaji na ubalozi kote watataka consent letter kutoka kwa baba kuthibitisha anakubaliana mtoto asafiri.
 
I have a question,hivi kwa scenario 'uyo mum' alikua single, na alikua raped na unknown assailant kupelekea mimba, kwenye birth certificate wanajaza nini?
 
I have a question,hivi kwa scenario 'uyo mum' alikua single, na alikua raped na unknown assailant kupelekea mimba,kwenye birth certificate wanajaza nini?
Kutakuwa na namna ya kuweka rekodi kwa tukio la namna hiyo.
 
Hata kama nimekimbia mimba lazima utaandika jina langu tu "Masumbuko Malinyingi"maana mimba hujaitunga peke ako binadamu hatutumii asexual reproduction.

Tofauti na hapo labda umwandike kaka ako.
 
Hivi katika maisha tuliyonayo kuna mtoto alipatikana kwa mzazi mmoja pekee? Nitaunga mkono hoja yako kama siku ikiweezekana mkianza kupata mimba bila ya mwenza mlieshirikiana, kuingiziana, kukatikiana, kuwekana kifo cha mende, dogg style, popo kanyea mbingu!

I'm out.
 
Unadhani kuwa mzazi ni kuweza kuzaa/kuzalisha tu?? Kuwa mzazi ni kuwa responsible for your kids haijalishi mko pamoja au mmeachana na mzazi mwenzako Watoto lazima uwape kipaumbele. sio unazalisha huko halafu unatekeleza Watoto then unajiita Baba. Hapo ni sperm donor tu
 
Hivi katika maisha tuliyonayo kuna mtoto alipatikana kwa mzazi mmoja pekee? Nitaunga mkono hoja yako kama siku ikiweezekana mkianza kupata mimba bila ya mwenza mlieshirikiana, kuingiziana, kukatikiana, kuwekana kifo cha mende, dogg style, popo kanyea mbingu!
I'm out.
Hivi yule jamaa alikuwa sijui mkuu wa nini kwa sasa anaishi Kigamboni, kwa mapito yake (alienda hadi China) hayawezi kulijibia hilo swali lako?
Ila kuingiziana kwa style ya kuchunguliana tamu sana
 
Mkuu shida inakuja kuwa in future unakuwa huna Uhuru na mtoto lazima baba documents zake zihitajike na ukute hamna mawasiliano lakini ukiwa single parent yeye anajulikana hayuko kwenye maisha ya mtoto. Mfano unaenda kuomba passport ama visa ya mtoto, uhamiaji na ubalozi kote watataka consent letter kutoka kwa baba kuthibitisha anakubaliana mtoto asafiri.
True Rita wabadilike kwa kweli mtu ka amemkataa mtoto Kuna haja ya kumwandika kweli?
 
Back
Top Bottom