Cheti cha kumaliza kidato cha nne. miaka 11 iliopita. nakifata wapi?

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,325
Habari wadau..

Kwa wenye ufaham hivi cheti cha kumaliza kidato cha nne kisipochukuliwa miaka mingi.. kinakuwepo bado shuleni au kinarudi NECTA...

Nauliza maana nataka kwenda shuleni niliposoma kukifuata.. sass nisije poteza nauli yangu kukikuta hakipo kimesharudi NECTA...

Nilikuwa natumia results slip mda mrefu ya form 4 kwenye mambo yote ya elimu na hata ajira..

Sasa nakihitaji kwa ajili ya application za goverment sector jobs..

Nimespend 5 yrs kwenye sekta binafsi nadhani kwa ujuzi nilioupata nahitaji kumuunga mkono Magufuli kwenye serikali yake kama mtumishi..ambapo wao wanataka vyeti tu sio results slip.
 
Mkuu unataka kuhamia government sector nina imani wewe ni muadilifu maana sasa hivi hakuna ujanja ujanja tena watu wanakimbia sasa. Anyway ninadhani cheti chako kitakuwa shule ingawa ingajaribu kuwasiliana nao kwanza
habari wadau..

kwa wenye ufaham hivi cheti cha kumaliza kidato cha nne kisipochukuliwa miaka mingi.. kinakuwepo bado shuleni au kinarud necta...

nauliza maana nataka kwenda shuleni niliposoma kukifuata.. sass nisije poteza nauli yangu kukikuta hakipo kimesharud necta.

nilikuwa natumia results slip mda mrefu ya form 4 kwenye mambo yote ya elimu na hata ajira..

sasa nakihitaji kwa ajili ya application za goverment sector jobs..

nimespend 5 yrs kwenye sekta binafsi nazan kwa ujuzi nilioupata nahitaj kumuunga mkono magufuli kwenye serikali yake kama mtumishi..

ambapo wao wanataka vyeti tu sio results slip
 
me kuna jamaa nlisoma nae alichelewa miaka miwili tu kwenda shule hajakikuta.....akakifuata necta
 
Kipo Shule,mi Nimehitimu Kidato Cha Nne Mwaka 2002 Mwaka Huu 2005 Mwezi Wa 9 Ndo Nimeenda Kukichukua Shuleni
 
Mkuu kinaweza kuepo shulen cha msing faya mawasiliano kwanza mm nilihitimu 2007 nikaenda chukua 2014
 
Nenda NECTA watakupa ac no ya kulipia CRDB then utawapelekea stakabadhi ya malipo watakupa cheti, shule utapewa leaving certificate kwani hazina mamlaka ya kukaa na vyeti zaidi miaka mitatu
 
Nenda shuleni wala usidanganyike na mambo yakwenda necta kama hakidaiwi na necta kitakua shuleni lakini kama mwalimu mkuu hatokua mwaminifu huenda alishapiga bei maana tatizo kama hiyo ilishawahi nikuta mara baada ya kumaliza chuo nikaenda fatilia cheti changu mkuu wa shule akaniambia kilishaibiwa na mwalimu mwenzake na alimfikisha kwenye vyombo vya dola lakini chaajabu mtuhumiwa baada ya kupewa mdhamana alitoroka na mpaka leo hajulikani alipo.
 
Back
Top Bottom