uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Habari wanaJf katika jukwaa hili tukufu la kuongezana maarifa,
Naomba msaada wa sehemu ipi sahihi nikafuate cheti changu cha kidato cha sita
Nilimaliza kidato cha sita, shule ya sekondari Pugu miaka kama 10 imepita. Sasa sikufuatilia cheti baada ya kumaliza kutokana na matokeo kuwa mazuri na kjiunga moja kwa moja chuo kikuu na bahati nzuri wakati nipo mwaka wa pili kimasomo nikapata ajira kutokana na matokeo kuwa mazuri ya kidato cha nne, sita na chuo kwa miaka miwili. Mwaka Wa tatu nilimaliza nikiwa tayari ndani ya ajira na nilipata ajira kwa kutumia cheti cha kidato cha nne, result slip kidato cha sita na nikawasilisha cheti cha chuo kikuu baada ya kumaliza
Lakini kutokana na sekeseke hili la vyeti feki, nimewaza sana nikaonelea nifuatilie cheti changu cha kidato cha sita japo hakihitajiki kikazi. Sasa kwa wanaofahamu masuala haya.
Je cheti hichi niende baraza la mitihani NECTA au shuleni Pugu Sekondari? Pili niende na nini kama ile result slip tu au kuna ziada yoyote? Na tatu suala la gharama naweza kulipishwa faini yoyote. Kwa ada sidaiwi kule shule
Asanteni