Cheo cha Balozi kama alichopewa Bashiru maana yake nini?

Acha Tuteseke Maana Alisema Mapema
Kosea Kuoa/Kuolewa Lakini Siyo Kuchagua
 
Kuna mahala niliwahi kuskia CS ni mkuu wa mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania..kwa hiyo ubalozi wa CS ni kwa sababu yeye ni mkuu wa Mabalozi pia.

Katibu Mkuu mstaafu Luhanjo hakua balozi... so alikua hawasimamii mabalozi? Kwa hoja yako?
 
Inawezekana kua katiba Kiongozi bila kua balozi...

Ila Rais ana mamlaka yote ya kufanya kile anachotaka kufanya...
 
Kama nilivyoambatanisha ili kutokuvunja katiba Kwa kuwa Bashiru hakuwa mtumishi wa umma afisa wa kuteuliwa kama katiba inavyotaka hivyo rais alimteua awe Kwanza balozi kukidhi kigezo hicho ndipo awe katibu mkuu kiongozi.
Sio lazima katibu mkuu kiongozi awe balozi Ila ni lazima awe mtumishi wa umma wa nafasi za afisa wa kuteuliwa na Kwa kumteua awe balozi Kwanza imemwezesha kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.View attachment 1713377

Unaweza kutusaidia ukurasa namba 42? Naona kifungu cha 7 kinaelezea anatakiwa awe kwenye nyadhifa gani
 
Bashiru ni mtumishi halali wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Kote huko alipo ni kwa kuazimwa maarufu chuo kikuu kama Secondment. Akitumbuliwa leo hii atarudi pale chuo kikuu UDSM kuendelea na majukumu yake ya Utumishi wa Umma. Mbona hamfuatilii mambo kabla ya kukosoa?

Uhadhiri sio nafasi ya kuteuliwa, kwahiyo kuwa mtumishi wa uma pekee haitoshi.
 
Back
Top Bottom