Cheo cha Balozi kama alichopewa Bashiru maana yake nini?

Kama nilivyoambatanisha ili kutokuvunja katiba Kwa kuwa Bashiru hakuwa mtumishi wa umma afisa wa kuteuliwa kama katiba inavyotaka hivyo rais alimteua awe Kwanza balozi kukidhi kigezo hicho ndipo awe katibu mkuu kiongozi.
Sio lazima katibu mkuu kiongozi awe balozi Ila ni lazima awe mtumishi wa umma wa nafasi za afisa wa kuteuliwa na Kwa kumteua awe balozi Kwanza imemwezesha kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.View attachment 1713377
asante ndugu, nimekuelewa
 
Ubalozi huo ni wa heshima tu,japo kua chief secretary naona ni bado sana panatakiwa mtu wa kumuambia rais ukweli na kuweza kumkatalia pia kwy baathi ya mambo! Huyu hataweza ametolewa jalalani huyo
Mnataka Rais akishauriwa jambo hata kwa kukataliwa na wasaidizi wake basi waite press conference kusema Rais tumemkatalia Rais jambo fulani? Au Rais amekataa ushauri wao? Dah! Hiyo itakuwa serikali ya wapi? Itamuongoza nani?
Watanzania tusipende sana Rais awe dhaifu, iwe kwa hulka yake au kupitia katiba. Kenya wamejaribu na imewashinda. Wameamua kubadilisha katiba ifanane na ya Tanzania kwa sehemu kubwa.
 
Kama nilivyoambatanisha ili kutokuvunja katiba Kwa kuwa Bashiru hakuwa mtumishi wa umma afisa wa kuteuliwa kama katiba inavyotaka hivyo rais alimteua awe Kwanza balozi kukidhi kigezo hicho ndipo awe katibu mkuu kiongozi.
Sio lazima katibu mkuu kiongozi awe balozi Ila ni lazima awe mtumishi wa umma wa nafasi za afisa wa kuteuliwa na Kwa kumteua awe balozi Kwanza imemwezesha kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.View attachment 1713377
Bashiru ni mtumishi halali wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Kote huko alipo ni kwa kuazimwa maarufu chuo kikuu kama Secondment. Akitumbuliwa leo hii atarudi pale chuo kikuu UDSM kuendelea na majukumu yake ya Utumishi wa Umma. Mbona hamfuatilii mambo kabla ya kukosoa?
 
CS kama mkuu wa utumishi wa umma, ni vema akawa balozi ili kufanya oversight kwa mabalozi na balozi zetu vyema.
Kuwa balozi kuna mlink vizuri na balozi za nchi za kigeni pia.
 
Wanaosema sio mtumishi waende UDSM college of social sciences wakaulize. Au kama sio mvivu atafute Prospectus ya UDSM 2020 nakala ya mtandaoni ukurasa wa 330 na 331.
 
Ubalozi ni hadhi, unaambatana na baadhi ya stahiki ikiwa ni pamoja na diplomatic passport and treatment, kama hautaki andamana.
 
Mkuu katiba haina kipengele chochote kinachozungumzia sifa za mtu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi.

Katibu Mkuu Kiongozi ni zao la Sheria ya Utumishi wa Umma yaani The Public Service Act ya Mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marejeo mbalimbali hasa hasa 2016, 2018, 2019.

Sheria hii nayo haiweki sifa za mtu kuteuliwa kuwa katibu Kiongozi.

Kwa marejeo naiambatanisha nakala ya sheria husika hapa.
View attachment 1713338
Walishadanganywa na Mnyika,
Kwa hiyo wanacheza dance wasilolisikia ila wanaangalia Mnyika anachezaje!
 
Sheria inataka huyo afisa awe ni mtumishi mwandamizi hivyo unaona alivyoteuliwa kuwa balozi jana ndio tayari ameshakidhi kigezo cha kuwa afisa mwandamizi? Afisa mwandamizi awe ametumikia angalau miaka kumi katika ngazi mbalimbali hadi kufikia kuwa katibu mkuu wa wizara au nafasi inayolingana na hiyo lakini huyo mtu wako juzi kati tu ndio ameokotwa jalalani(kwa mujibu wa kabudi)
Duh! Ebu tuwekee reference
 
Kuna mahala niliwahi kuskia CS ni mkuu wa mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania..kwa hiyo ubalozi wa CS ni kwa sababu yeye ni mkuu wa Mabalozi pia.
 
Utakuta hata mteuzi kwa kuwa alimkuta balozi ombeni sefue basi anafikiri ni lazima awe balozi lakini ukweli sio lazima kwani martin lumbanga hakuwa balozi na Philemon Luhanjo hakuwa balozi
Lakini watu humu mnavo mshusha Raisi wetu yani mnamuona kama mshamba fulani limbukeni Jinga fulani duh sio vizuri.
 
Utakuta hata mteuzi kwa kuwa alimkuta balozi ombeni sefue basi anafikiri ni lazima awe balozi lakini ukweli sio lazima kwani martin lumbanga hakuwa balozi na Philemon Luhanjo hakuwa balozi
Ni Kukariri Kama Kasuku 😄😃😁
 
Wanaosema sio mtumishi waende UDSM college of social sciences wakaulize. Au kama sio mvivu atafute Prospectus ya UDSM 2020 nakala ya mtandaoni ukurasa wa 330 na 331.
... sio tu anatakiwa kuwa mtumishi wa umma, bali pia anatakiwa kuwa "Afisa Mwandamizi aliye katika nafasi ya uteuzi"; na Ibara ya 116(7) imeeleza vizuri kuwa ....

... Kwa madhumuni ya Ibara hii, maneno "Afisa Mwandamizi aliye katika nafasi ya uteuzi" maana yake ...
 
Kama nilivyoambatanisha ili kutokuvunja katiba Kwa kuwa Bashiru hakuwa mtumishi wa umma afisa wa kuteuliwa kama katiba inavyotaka hivyo rais alimteua awe Kwanza balozi kukidhi kigezo hicho ndipo awe katibu mkuu kiongozi.
Sio lazima katibu mkuu kiongozi awe balozi Ila ni lazima awe mtumishi wa umma wa nafasi za afisa wa kuteuliwa na Kwa kumteua awe balozi Kwanza imemwezesha kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.View attachment 1713377

Hivi alijiuzulu UDSM? Au kile chuo sio cha Umma ie kua kinampa sifa ya utumishi wa Umma? Nawaza tu
 
Back
Top Bottom