Cheo cha Balozi kama alichopewa Bashiru maana yake nini?

Mabobish

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
362
500
Wadau naombeni mwenye kufahamu ufafanuzi juu ya cheo alichotunukiwa Dr.Bashiru Ally sambamba na uteuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi. Binafsi sijaelewa kwamba huenda ni sharti ili uwe Katibu mkuu Kiongozi ni lazima uwe Balozi??

Nawasilisha kwa hoja si mapovu
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
15,650
2,000
Sababu kubwa ni katiba ilimtaka CS awe ni mwajiliwa serikalini, ila Bashiru hakuwa mwajiliwa
Mkuu katiba haina kipengele chochote kinachozungumzia sifa za mtu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi.

Katibu Mkuu Kiongozi ni zao la Sheria ya Utumishi wa Umma yaani The Public Service Act ya Mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marejeo mbalimbali hasa hasa 2016, 2018, 2019.

Sheria hii nayo haiweki sifa za mtu kuteuliwa kuwa katibu Kiongozi.

Kwa marejeo naiambatanisha nakala ya sheria husika hapa.
View attachment 1713338
 

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,373
2,000
Mkuu katiba haina kipengele chochote kinachozungumzia sifa za mtu kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu kiongozi.

Katibu Mkuu Kiongozi ni zao la Sheria ya Utumishi wa Umma yaani The Public Service Act ya Mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marejeo mbalimbali hasa hasa 2016, 2018, 2019.

Sheria hii nayo haiweki sifa za mtu kuteuliwa kuwa katibu Kiongozi.
Unajaribu kusisitiza nini hapa ukizingatia swali la mtoa mada?
 

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
787
1,000
Government Machinery inayomsaidia Rais kufanya kazi hawajui wanachofanya?
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
804
1,000
Khee!! Ina maana Bashiru kapewa ubalozi?! Kisa na mkasa?! Ina maana mtu hawezi Chief Secretary bila kuwa balozi?!
 

BonT

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
804
1,000
Huu ndio ukosoaji usiokuwa wa staha aliozungumza Rais.
Sasa ni wapi hapo alipokosa staha?! Acheni haya mambo ya kulea lea maujinga ya viongozi ya kutaka waonekane miungu watu! Yeye mwenyewe mbona huwa haongei lugha za staha tena hadharani?! Au kwavile yeye ni rais ndo anaweza kuwaambia watu hadharani "bakini na mimavi yenu" lakini raia kusema "akili za mteuzi" ndo uvunjwaji wa heshima?
 

dindilichuma

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
1,389
2,000
Kama nilivyoambatanisha ili kutokuvunja katiba Kwa kuwa Bashiru hakuwa mtumishi wa umma afisa wa kuteuliwa kama katiba inavyotaka hivyo rais alimteua awe Kwanza balozi kukidhi kigezo hicho ndipo awe katibu mkuu kiongozi.
Sio lazima katibu mkuu kiongozi awe balozi Ila ni lazima awe mtumishi wa umma wa nafasi za afisa wa kuteuliwa na Kwa kumteua awe balozi Kwanza imemwezesha kukidhi vigezo vya kuteuliwa kuwa katibu mkuu kiongozi.
JamiiForums1654712309.jpg
 

nra2303

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
2,939
2,000
Ubalozi huo ni wa heshima tu,japo kua chief secretary naona ni bado sana panatakiwa mtu wa kumuambia rais ukweli na kuweza kumkatalia pia kwy baathi ya mambo! Huyu hataweza ametolewa jalalani huyo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom